Siasa za msikiti Uingereza

Statarea,
Unaandika ukiwa umeghadhibika.

Ili mjadala uwe na tija na wasomaji pamoja na wachangiaji wanufaike
na mjadal kubwa kwanza ni adabu.

Kuheshimiana.

Ikiwa mchango wako umejaa ''name calling,'' unakuwa tayari ushajitoa
maana.

Utapuuzwa.
Hakuna apendae kusoma kelele na jeuri.

Sasa umechanganya mambo mengi katika post yako.
Kwanza kunishambulia binafsi.

Mjadala hauendeshwi hivyo.
Muhimu ni kutoa hoja.

Umegusa mafunzo ya Uislam ambayo huyajui.
Lakini kubwa hili somo wewe hujapatapo kulisoma na hivyo kulifahamu.

Umeshika kalamu na kuandika huku kichwa kimejaa hasira.

Tuanze na hili la ugaidi na nakuomba usome niliyopata kuandika kwani
kwanza umfahamu huyo unaejadiliananae na pili utalijua somo lenyewe:

Mohamed Said: ISLAM, TERRORISM AND AFRICAN DEVELOPMENT

Ukishasoma hii paper sasa reja hapa barazani na unayotaka kusema na
baada ya hapo tutaendelea na hayo mengine ya ubaguzi ili tupate kumjua
nani mbaguzi katika nchi yetu.
 
Waislamu ni watu wa ajabu sana.

Mbona hamuelezi sababu ya kuvunjwa kwa huo msikiti.Mnajifanya kujua sana haki zenu na mara zote nyie ndiyo huonewa.

Hapo UDOM kuna makanisa yamejengwa??
Sababu wanasema Sie waislamu tumemroga VC aliyefariki hapo majuzi.

Na wale watumishi wote 11 walohamishwa wapo ktk uongozi wa jumuia ya waislam UDOM

Hii ndio sababu zote unazosikia ni kuweka mambo sawa tu.
 

You always look smart,well educated but your religion and chauvinistic sense has clouded your judgement on many agenda! You were not supposed to issue a one side sad story while leaving the whole facts for the demolition of that Mosque in Dodoma.
Ungeweza kuchambua vema lakini umeacha kwa makusudi ili kuchochea ionekane waislam wanaonewa!
Unafanya dhambi mbaya sana! Ifta berat iyasanuul.
 
Makundi ya kigaidi kama alshabab ndio yamesababisha. Na wanachama wake wengi wanatoka misikitini. Kwahiyo nibora kuivuja wakose pa kukutania kupanga mipango yao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waislamu ni watu wa ajabu sana.

Mbona hamuelezi sababu ya kuvunjwa kwa huo msikiti.Mnajifanya kujua sana haki zenu na mara zote nyie ndiyo huonewa.

Hapo UDOM kuna makanisa yamejengwa??

The Book,
Haya ni mambo ya kuwekwa hadharani yakajadiliwa kuwa tumefikaje
hapa kuwa leo tuna tatizo kama hili?

Haya si mambo ya huyu anaandika hivi mwenzake anajibu vile.
Serikali iache kuogopa tatizo hili kwa kutegemea kuwa litajiondoa lenyewe.

Waulizwe Wakristo ni asilimia ngapi ya Waislam iwepo hapo UDOM na kwengine
ili ionekana hakuna udini?

Tukipata jibu la swali hili hapo ndipo tutaanzia kuondoa huu udini unaolalamikiwa
na Wakristo.

Sasa hivi UDOM Wakristo katika uongozi ni 88.6% na Waislam ni 11.4%.

Swali, hivi ndivyo UDOM inavyoondoa udini?
 
UDOM ni chuo cha serekali mabo ya misikiti au kanisa hayana nafasi.Eka 11 sehemu ya chuo zinatolewa kienyeji kwaajili ya msikiti ???????.Hivi UDOM ni mali ya BAKWATA au Serekali !.

Mimi nisingeshangaa ikiwa msikiti ungepewa kiwanja cha 20 kwa 40 lakini eka 11 duh hivi waTanzania nani kawaloga.KKKT ,Anglican na Catholic wakiomba eka 11kila mmoja Udom itakuwa uwanja wa dini na si chuo kikuu.Uongozi uliopita enzi za Kikwete ulielemea dini sana na haya ndio madhara yake.
 


Kwahiyo wewe kazi yako ni kuanglia asilimia za uongozi kwa kigezo cha dini ?.
 
Mleta mada unawazungumziaje wakristo wanaopata adha, taabu na manyanyaso kutoka upande wenu hasa Zanzibar wakati wa mifungo yenu

Maana bandiko lako linaonyesha ni waislamu wanaonyanyasika kwa kuleta matukio ya 98 nk lkn tumeshuhudia waziwazi padri kapigwa risasi, kamwagiwa tindikali na wakristo wakipigwa hadharani wakipata chakula wakati wa mfungo lkn haya unajitia upofu

Sishabikii ubaguzi Ila jaribu kubalance story yako na siyo kutaka kuonyesha ni waislamu pekee wanaonewa nchi hii.
 
Neno unyanyasaji,inatakiwa ipewe maana yake halisi
Mfano
Zanzibar,imeweka sheria na kanuni zake kuwa,Haifai mtu kuonekanwa anakula mchana wa Ramadhan au kunywa
Kama kula au kunywa,Basi fanya ukiwa kwako au sehemu usioonekanwa na watu

Iwapo utavunja sheria hii
Ukahukumiwa,Basi hapa hatusemi kuwa umenyanyaswa
Bali tutasema,Sheria imefuata Mkondo wake

Lkn
Kama Sheria hakuna,kisha ukakatazwa au kupigwa au kubezwa na mfano wake,
Hapa maana halisi ya unyanyasaji,itapata hadhi ya kusemwa na kuchukuliwa
Sent using Jamii Forums mobile app
 
ama jambo la kupigwa Risasi kwa Padri
na raia tu,
Hili Uislam unakemea vikali,na hata Sheria zetu za nchi,inakemea vikali

Aliefanya kitendo hicho cha kikatili,lazima atafutwe na Sheria ifuate mkondo wake

Hakuna anaependa Dhulma ikiwa mtu ana akili timamu
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kisha
Tuwe waadilifu katika maandishi yetu
Je!Kwa hapo Znz,ni Wakristo tu ndio wanakatazwa kula mchana wa Ramadhaan au hata Waislam wenyewe?!

Na
hao wanaopigwa na kushitakiwa,ni Wakristo tu au hata Waislam?!!

Nitasubiri majibu yako katika Hili Chief

Barikiwa sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hiyo hiyo sheria imetoa uhalali wa mtu yeyote kumuadhibu atendaye hilo kosa acha habari zako wewe Kwa hiyo wewe moyoni mwako huwa unafarijika sana ukiona wenzako wanavyomharass kwa kumpiga in the name of sheria na kanuni mkristo anapopata chakula

Mbona ya padri kapigwa risasi na kamwagiwa tindikali hujajibu au nayo ni kanuni na sheria huko Zanzibar?
 
Soma nilichokiandika vzr

Sheria inahukumu Muislam na asie kuwa Muislam
Ama raia kuchukua Sheria mkononi na kuamua kuadhibu,hili halihalalishi kosa lake!!!

Bali atakuwa mtuhumiwa namba moja kwa kukosea Sheria

Kwa ufupi tu
Usihukumu watu kwa matendo ya baadhi,kwa nia zao chafu
Shukran Chief
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani wanaajiri kwa vigezo gani?
 
kuna kitu cha kujifunza hapo..
 
Sio kweli mimi hivi sasa naandika message niko Muscat, Oman hamna shida yoyote wakristo wapo na wana makanisa yao wanatekeleza ibada zao bila ya shida yoyote
Huku huwa tunapumzika ijumaa na jumamosi jumapili tunapiga mzigo kama kawa hivyo kama wewe ni mkristo unataka kwenda kanisani jumapili una option aidha unaomba kutokuja kabisa au unachelewa kuja ukipitia kanisani kwanza na kazi zinaenda vzuri
Yaani katika public life hakuna kitu kinaweza kukufanya ujisikie kubaguliwa labda uwe na inferiority complex uwe mtu wa kujishtukia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…