Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
- Thread starter
- #61
Statarea,Nawewe ni mfia dini kiasi hicho pamoja na kuwa na umri mkubwa?
Ikitokea ukaitwa gaidi, mbaguzi n.k utakataa?
Unafahamu yakwamba taratibu na mafundisho mengi (si yote) ya kiislamu yanabagua na kuwakandamiza wasio waisilamu?
Mfano Mwisilamu nduguye ni mwisilamu hili lilitokea hata Chuo kikuu cha Garisa, pili nimefatilia post zako nyingi zinazohusu dini yako ni dhahiri unahekima ila ni mbaguzi mkubwa kwa wasio waislamu, kuna mtu anaitwa Faizafoxy nimepitia kidogo post zake mama yangu huyu ni Mbaguzi, na nikatili sana dhidi ya dini zingine
Mkuu badilisheni hayo mafundisho image yenu kwa jamii itasafishika
Unaandika ukiwa umeghadhibika.
Ili mjadala uwe na tija na wasomaji pamoja na wachangiaji wanufaike
na mjadal kubwa kwanza ni adabu.
Kuheshimiana.
Ikiwa mchango wako umejaa ''name calling,'' unakuwa tayari ushajitoa
maana.
Utapuuzwa.
Hakuna apendae kusoma kelele na jeuri.
Sasa umechanganya mambo mengi katika post yako.
Kwanza kunishambulia binafsi.
Mjadala hauendeshwi hivyo.
Muhimu ni kutoa hoja.
Umegusa mafunzo ya Uislam ambayo huyajui.
Lakini kubwa hili somo wewe hujapatapo kulisoma na hivyo kulifahamu.
Umeshika kalamu na kuandika huku kichwa kimejaa hasira.
Tuanze na hili la ugaidi na nakuomba usome niliyopata kuandika kwani
kwanza umfahamu huyo unaejadiliananae na pili utalijua somo lenyewe:
Mohamed Said: ISLAM, TERRORISM AND AFRICAN DEVELOPMENT
Ukishasoma hii paper sasa reja hapa barazani na unayotaka kusema na
baada ya hapo tutaendelea na hayo mengine ya ubaguzi ili tupate kumjua
nani mbaguzi katika nchi yetu.