Siasa za msikiti Uingereza

Siasa za msikiti Uingereza

Hivi ndugu zetu Wakristo mbona huwa mnajisahau sana. Tatizo kama hili la Udom liliwahi tokea pale chuo cha Diplomasia Kurasini
Pale ilionekana kuna harufu za udini, waislam walikionekana wengi kuliko wakristo ikaundwa tume kwenda kuchunguza hilo
Bahati mbaya ile tume wajumbe wote walikuwa wakristo
Hatuwezi ku justify ubaguzi kwa kutumia ubaguzi hata siku moja na haya ndio naona yanatokea NSSF na UDOM Hizi ni taasisi za wasomi na ziko kisomi zaidi hivyo hata approach zao za kutatua matatizo yao inapaswa yawe ya kisomi zaidi
Vitu vinavyoonekana vidogo vidogo kama hivi ndio hujenga matukio kama yale ya Rwanda

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeishi Uingereza kwenye mji mmoja unaitwa Cardiff ambao ni mji mdogo ulioko Wales na kwa kawaida kwa Waingereza watu wa Wales wanadharaulika wanaonekana washamba.

Neil Kinnock alipata kugombea kutaka kuwa Waziri Mkuu wa Uingereza na yeye ni Mwelshi.

Siku moja kaingia mwalimu wetu mmoja yeye ni kutoka England anaitwa Brown Thomas akamsema kwa ubaya sana Kinnock, ‘’Ati na huyu nae anataka kuwa Waziri Mkuu wa Uingereza. Nani atampigia kura Mwelish?’’

Kwa sababu hii na dharau hii mimi nilipokwenda kupiga kura nilimpigia Neil Kinnock wa Labour Party lakini hakushinda aliyeshinda alikuwa John Major wa Conservative.

Najua msomaji wangu unashangaa vipi huyu mtu kutoka Kariakoo apige kura Uingereza?

Naam nimepiga kura. Uingereza sheria yao ni kuwa ukiwa ni mlipaji kodi haijaslishi kama ni mwananchi au mgeni unaweza kupiga kura.

Mbunge wangu mgombea alinifata nyumbani kwangu Column Road kwa adabu zote kuomba kura yangu.

Msikiti wa mtaani kwangu ni jengo ambalo hapo zamani lilikuwa kanisa lakini kwa kuwa watu walikuwa hawaendi kuabudu Wakristo wa sehemu ile wakaamua kuliweka gazetini kutangaza kuuza kanisa lao.

Hapo wakatokea Waislam wakalinunua kanisa lile na kuligeuza kuwa msikiti.

Hivi ndivyo ilivyotokea kwa msikiti huu Darul Isra kuwa katikati ya makazi ambayo wengi wa wakazi ni Wakristo.

Kwa muda wote nilioishi eneo lile sikupata kuhisi uadui wowote kutoka kwa hawa Waingereza kuwa walikuwa na chuki na msikiti ule.

Tatizo lilikuwa moja tu.

Barabara ya kuingia msikitini ilikuwa inakataza kuegesha magari kwa sababu ya ufinyu wa barabara.

Siku ya Ijumaa wanafunzi wengi wanakuja msikitini kwa ajili ya sala ya Ijumaa na baadhi yao ni vijana wanafunzi kutoka ncbi za Kiarabu ni wanafunzi lakini wana magari mazuri tu na lazima waje na magari yao na watayaegesha hapa mtaani na trafiki watakuja na kuweka tiketi.

Hawajali fedha wanazo wanalipa faini.

Ikatokea baada ya kurudi Tanzania nilirudi tena Cardiff nikitokea London na nikaenda Darul Isra msikitini kwangu kwa zaamani.

Safari hii nikapewa habari nyingine ya kufurahisha kuwa msikiti ule umenunua kanisa lingine na kuna mpango wa kulikarabati kuligeuza msikiti lakini kwa wakati ule lile kanisa wakilitumia kama bohari ya kuwekea vitu.

Nimekwenda Tilbury Port huu ni mji nje ya London na ni bandari.

Siku za nyuma bandari hii ilikuwa na biashara kubwa lakini wakati wa Magret Thatcher uchumi ulibadilika na bandari hii ikapoteza umuhimu wake.

Wengi wa wakazi wa mji ule mdogo walikuwa wafanyakazi wa bandari na baada ya bandari kukosa biashara na kazi kuwa haba wafanyakazi wengi walipoteza ajira kwa hiyo wakahama mji.

Niliingia Tilbury mchana kwa treni.

Nilipata mshtuko mkubwa sana.

Mji mzima hakuna mtu anaeonekana barabarani wala gari kupita.

Maduka ya mtaa mzima mkubwa wenyewe wanaita ‘’High Street,’’ yamefungwa lakini matangazo yapo yakitangaza biashara tofauti.

Unatembea barabarani unasikia sauti ya kiatu chako kinapogonga lami ya barabara.
Tilbury ni ‘’ghost town,’’ mji uliohamwa na katika masiaha yangu yote sijapatapo kuona kitu kama hiki.

Inabidi wenyeji waliobakia wakuelekeze mahali ambapo unaweza kwenda kula chakula sehemu inaitwa Stella Maris, hii ni mfano wa huku kwetu wa Mission to Seaman sehemu ambayo zimewekwa maalum kwa kuwahudumia mabaharia kwa malazi na chakula.

Eid Kubwa imenikuta katika mji huu na hakuna msikiti lakini nimefahamishwa kuwa Waislam wapo ingawa hawana msikiti.

Wenyeji wakanieleza kuwa katikati ya mji kuna shule ya msingi ambayo hapo ndiyo Sala ya Eid huswaliwa ndani ya darasa.

Hapo ndipo niliposwali Sala ya Eid na wengi wa Waislam walikuwa Wahindi.

Miaka mingi ikapita siku moja nikajikuta niko Maryland, Washington DC Amerika na Ijumaa imefika.
Mwenyeji wangu Dr. Harith Ghassany akanichukua twende kusali.

Haikunipitikia kuwa sehemu ile hakuna msikiti na hivyo ndivyo ilivyokuwa.
Hapakuwa na msikiti.

Dr. Ghassany alinichukua John Hopkins University na tuliswali ndani ya moja ya madarasa ya chuo hicho.

Tanzania nchi ambayo Waislam ni umma mkubwa kuna chuki dhidi ya Uislam kupelekea kuvunjwa misikiti...

Swali la kujiuliza ni nchi yetu nani kaifikisha hapa?
Nini chanzo cha uadui huu.

Leo mnaona fahari kununua makanisa na kuyabadili kua misikiti. Usichekelee hilo ni fundisho mnapewa na pia muujue ukristo ni dini ya kweli isio Na tabu WALA Shari wala roho ya ugaidi WALA chuki .Mfano Papa ameenda arabuni lengo niku uaminisha ulimwengu kuwa ukristo ni dini Bora.
 
Hapa kisa ni kukataa kufaulisha, kufundisha dini au kuwa muislamu?
Sniper,
Upendo hauwezi kuwepo katika dhulma.
Soma kisa hiki hapo chini upate picha ya haya ninayokueleza:
Mohamed Said: Mwalimu Athmani Khalfani Mrindoko Mwalimu wa Shule ya Msingi Lwande Kosa Lake Kusomesha Wanafunzi Qur'an na Kukataa Kuchakachua Mitihani

View attachment 997252
Mwalimu Athmani Khalfan Mrindoko Mwalimu wa Shule ya Msingi Lwande

Mwalimu Athmani Khalfani Mrindoko ni mwalimu wa shule ya msingi Lwande moja ya vijiji vilivyoshambuliwa kwa tuhuma za ugaidi.

Mwalimu Athmani ni mwalimu mwajiriwa na serikali kusomesha masomo ya kisekula lakini kwa mapenzi yake katika Uislam kwa kuwa walimu wa somo la dini ya Kiislam Shule za Msingi hakuna yeye hujitolea kuwasomesha wanafunzi hawa na kuwatungia mitihani.

Kisa chake ni kisa cha kusikititisha na kuhuzunisha.

Siku za nyuma Mwalimu Athmani alifatwa na walimu wenzake akaelezwa kuwa imetoka amri juu kuwa walimu washirikiane kuwafaulisha watoto darasa la saba kwa kuwakokotolea wanafunzi majibu ya mtihani wa mwisho wa darasa la saba ili kunyanyua ufaulu wa shule na hatimaye wilaya.

Mwalimu Athmani akakataa hili kwa misingi ya Uislam kuwa hicho kitendo ni ghushi yaani udanganyifu.
Udanganyifu huu ukakwama na sababu ni yeye Mwalimu Athmani.

Hapa ndipo zilipoanza chuki dhidi yake.

Sasa lilipotokea sakata la Lwande askari waliovamia kijiji kwa madai ya kupambana na Al Shabab Mwalimu Athmani akakamatwa, kupigwa na kufunguliwa kesi ya kujeruhi Mahakama ya Handeni.

Mwalimu Athmani sasa hivi ni masikini.

Alipoachiwa gerezani kwa dhamana alikuta nyumba yake imevunjwa na vitu vyake vyote vimeibiwa.

Huyu ndiye ''gaidi'' anaeshirikiana na Al Shabab.

Mwalimu muadilifu anaesomesha watoto kitabu cha Allah.

Mwalimu Athmani Khalfan Mrindoko ''Al Shabab wa Kufikirika.''

Haya ni machache.
Yapo mengi katika dhulma hii ya kumfanya mtu akabubujikwa na machozi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nikionacho hapa hao wazee walikua na upendo na Mwl Nyerere sio na wa Kristo. coz hawakumsapoti nyerere juu ya mambo ya kanisa na hapo ndipo naanza kupata hisia za kwanini shule za kiisilamu ufaulu wao ni mdogo, nyerere alikua kichwa hapo nani mwingine angesimama kudai uhuru kwa wasomi.
Khan said:
Waislamu mna uwezo finyu sana wa kufikiri, Mnalalama kama mtoto wa kambo, Mnaikumbatia tamaduni ya kigeni (Uislamu) Kuliko utu au ubinadamu, Waislamu hamuaminiki, waislamu ni Magaidi, watu ambao hawana utu, Watu ambao huwezi kuwa na amani kuishi nao, watu wanaoonesha ubaguzi wa kidini wazi wazi! "Waislamu", Achana na tukio tu la Dodoma, Kuna haja ya waislamu kubomolewa Misikiti yao yote..
Khan,
Umeandika kwa hasira nyingi sana.
Ndipo ninapouliza hizi chuki nini sababu na chanzo cheke.

Historia ya udugu iliyowekwa na wazee wetu ni nani kaifuta?

WAISLAM WALIKUWA NA MAPENZI MAKUBWA NA BABA WA TAIFA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE

Hii ndiyo historia yetu ya mapenzi baina yetu. Baba wa Taifa yuko katikati ya Waislam waliomkaribisha Dar es Salaam 1952 wakamchagua kuwa kiongozi wa TAA 1953, 1954 wakaunda TANU Nyerere akiwa rais na 1955 wakamfungia safari ya UNO. Huu uadui na kuwanyanyapaa na kuwabagua Waislam nini chimbuko lake na imesababishwa na nini na nani muhusika? Kuna mtu anaeweza kutoa majibu?

1547697413953-png.996785


Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere akiwa kashikwa mkono na Mzee Mshume Kiyate kulia na kushoto kashikwa na Mzee Max Mbwana na Mwinjuma Mwinyikambi. Mwalimu Nyerere kazungukwa na Waislam. Udugu na mshikamano huu umepoteaje? Je, kulikuwa na watu waliokuwa hawafurahishwi na umoja huu? Ni nani hawa? Picha hii ni Uchaguzi Mkuu 1962.

Hawa akina mama wa Kiislam ndiyo walikuwa wanachama wa mwanzo wa TANU 1954. Kulia ni Bi. Tatu bint Mzee akifuatiwa na Bi. Titi Mohamed. Kushoto wa kwanza ni Bi. Chiku bint Said Kisusa (mke wa Shariff Attas) wakimsindikiza Mwalimu Nyerere Uwanja wa ndege safari ya kwanza UNO 1955.
Idd Faiz huyo hapo aliyevaa kanzu, koti na tarbush kulia kwa Nyerere akimsindikiza safari ya UNO 1955.

1547697514425-png.996788


1547697592314-png.996790



1547697743316-png.996791


Kushoto Idd Faiz Mafungo, Sheikh Mohamed Ramiya, Saadan Abdu
Kandoro na Haruna Taratibu, Dodoma 1955. Huyu Idd Faiz ndiye
aliyekuwa mkusanyaji fedha za safari ya Mwalimu Nyerere UNO 1955
ni huyo hapo chini kulia kwa Mwalimu Nyerere aliyevaa kanzu, koti na
tarbush.

1547744875055-png.997514

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Halafu tunapozungumzia muislamu au mkristo hivi hawa watu tunawafaham kwa vigezo gani, au majina tuu. Kama ni hivyo basi jibu la swali lako ni hili, anayetufikisha huku unapopaona tunabaguana ni yule aliyetutaka tuachane na majina yetu ya asili ya mwafrica na kuanza kutumia majina ya asili ya warabu na wazungu. Ambaye ni hizi DINI.. lakini tukiyaangalia maisha nje ya dini amini nakuambia bado hatujaanza hata robo ya chuki zakubaguana kutokana na maisha yetu ya kila siku.

kwangu sina muisilamu wala mkristo mi namjua mtanzania tuu hao wengine wabaguanao sijui kuchukiana na wanaoumizwa na hao wote nadhi watakua ni wafuasi wa wazungu na waarabu tuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kwa utafiti mdogo wa nilikoishi na kusoma.

chanzo cha uadui ni picha mbovu juu ya uislam walionayo wakristu vichwani mwao.
hili limesababishwa na vitu nane


1}mahubiri ya chuki na uongo juu ya uislam baina ya wakristu.

wakristu huwa wanaelimishana wao kwa wao juu ya uislam,hapa wanalishana matango pori,uislam dini ya majini,ugaidi,mara mtume alioa mtoto wa miaka tisa mbakaji,waislam ni watu wa vurugu,waswahili.
mfano kuna kanisa hapa la kilokole jamaa huwa wanazima mic jamaa anaanza kuongelea kuwa uislam ni ugaidi,jamaa akitoka nnje anakausha kama sio yeye,na anaowahubiria humo wengi wao ni wanafunzi.


2}vyombo vya habari.
magazeti,redio za ndani ya Tanzania na runinga za nnje zimechafua sana taswira ya uislam

3}elimu juu ya uislam.
Elimu ya Tanzania haina hata sub topic ya dini,mkristo hapa anakua empty set chochote anachopewa juu ya uislam anameza.
mkristu wa Tanzania hajui kabisa kilichomo ndani ya Qurani,zaidi ni yale mahubiri ni kitabu cha majini

4]Islamophobes
hawa wanachuki tu bila sababu.


5]Tabia mbovu za mtu mwenye jina la kiislam.


6]Siasa

7}Shetani

8}Hofu


hayo ni kwa uelewa wangu mdogo nilionao.
Hivi wewe ushawahi kwenda Kanisa lolote ukakuta Wakristo wananaizungumzia dini ya mbakaji Muhammad?

misikitini huko sina haja ya kuuliza kwani Koran yenyewe inaeleza habari zetu
 
Baada ya miaka 50 ulaya yote itakua Islamic continent. Wenzetu wengi wanaelekea huko toka Middle East na North Africa na idadi yetu haitopungua kamwe. Inshaallah

Sent using Jamii Forums mobile app
Ulaya wakiwa waislamu wote wewe mmakua utafaidika na nini au ndio mmeambiwa mtaenda mbinguni?
 
Siyo tu Tanzania, nchi nyingi za Africa ni wafia dini...

Ila huko dini zilipotoka au kuanzia hawana shida wala habari...


Cc: mahondaw
 
Hivi ni makanisa mangapi nayo yamevunjwa kwa sababu hizohizo lkn watu wamekaa kimya na hawalalamiki hovyo? Unajua hii ndio maana mnaonekana nyie ni watu wa lawama tu.
 
Back
Top Bottom