Odhiambo cairo
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 15,989
- 22,078
Nani kaomba lockdown ?!Serikali haina hela ya kupambana na Covid ipasavyo. Wakifanya lockdown watu watakufa njaa, uchumi utaporomoka na hali ya amani inaweza kupotea, wakiwapa takwimu za kweli za jinsi ya huu ugonjwa ulivyosambaa chanjo zilizotolewa msaada hazitatosha maana wengi watazitaka na hela za kununua chanjo hakuna. Matibabu ya wagonjwa wa Covid ni gharama sana, hospitali zinaelemewa. Ndiyo maana unaona yanayoendelea sasa hivi.
Angalau wawe wakweli. Kwani mwanzo ni serikali hii hii iliyokataa swala la Corona na kuibatiza jina la "changamoto ya upumuaji" . Lakini ghafla ni hawa hawa wanaimiza chanjo za Corona leo !!. Ukweli uko wapi na tusimamie lipi ?!