#COVID19 Siasa za nchi yetu na wingi wa vifo mitaani

Nani kaomba lockdown ?!

Angalau wawe wakweli. Kwani mwanzo ni serikali hii hii iliyokataa swala la Corona na kuibatiza jina la "changamoto ya upumuaji" . Lakini ghafla ni hawa hawa wanaimiza chanjo za Corona leo !!. Ukweli uko wapi na tusimamie lipi ?!
 
Kweli kabisa,Sasa jamii ifanye nini iliiokoke?

Jamii inahitaji uongozi kuwakabili tuliowapa dhamana hawa wasio wajibika kwetu.

Wanadai kipaumbele ni kusimamisha uchumi, bila shaka wakimaanisha uchumi wao si wetu.

Uchumi wetu vipi wakati walioongezewa kodi na tozo ni sisi? Uchumi wetu vipi wakati sisi waathirika wa ugonjwa tunajigharimia wenyewe? Uchumi wetu vipi wakati sisi tumetelekezewa janga peke yetu?

Hawa ni lazima kuwakabili na kuwafahamisha na watuelewe wazi wazi kuwa tunataka:

1. Mpango mkakati unaoeleweka wa kupambana na ugonjwa huu.
2. Wapotoshaji wa ugonjwa huu katika kipindi chochote hawawezi kuwa makamanda wetu katika vita nao katika kipindi chochote.
3. Masuala ya ugonjwa huu yanapaswa kuwa ni kipaumbele hadi tutakapojiridhisha kwenye uelekeo wa ugonjwa wenyewe.
4. Masuala ya ugonjwa huu yakabadhiwe na kushughulikiwa na wataalamu husika wa mambo ya afya.

Ni lazima wenye dhamana wayajue haya na si vinginevyo.
 
Nimekuelewaa
 
Hahaaaaaa bora hata enzi za kujifukiza mara miambili hakukuwa na shida kama kipindi hiki cha chanjo
 
Wananchi wamegoma hawanahabari na Korona, hawataki kusikia wa kufuata maelekezo ya kujikinga na Korona, wao ni LIWALO NA LIWE.
 
Magonjwa Kama Asthma,Pneuonia,mafua ya kawaida yanalamishwa yawe Corona.
 
Dorothy yuko na shemejiye wanacheza kindumbwendumbwe.
 
Corona inakuzwa kuliko uhalisia,na JPM alituasa tuichukulia sawa na magonjwa mengine,hivyo hofu ipo kwa viongozi tu,watavaa Sana mibarakoa mpaka mioyo ipanuke.

Tuko kwenye kampeni ya kitaifa ya kulazimishana na kusukumiziana chanjo ya corona ili kuwa furahisha wafadhili akiwapo farm master.
 
Ipo mipango mingi ambayo ilikwisha andaliwa miaka mingi ya kuleta genocide,wala usimlaumu Gwajima naye kazaliwa kaikuta mipango hiyo ipo,na kama anaijua itakuwa bahati sana.Mkuu hivi kwa akili zako unadhani diabetes,cancers,HBP etc.chanjo chake nini hasa.Jiongeze mkuu,do your own research usitegemee kila kitu serikali ikufanyie.

By the way never think the government has your best interest at heart.
 
Hizi paranoia kuwa kuna watu walipanga kufanya genocide ni dalili za kichaa, au umeangalia movie kupita kiasi.
 
Aisee kweli vifo KWa Sasa vimeongezeka
 
Hakuna corona Tanzania,mwisho utakuwa mzuri tu.Mbona kwa Magufuli tulikuwa salama,iweje sasa mambo yabadilike ghafla,wachanjane wenyewe.
Kwa magufuli gani?
Mimi sijasema covid19 ipo,ila nimeomba ufafanuzi toka January kuna ongezeko la vifo na huyo magufuli alikuepo na yeye akafa kifo chenye utata kwetu sisi watanzania
 
Kawaida mbona hata Moro yasemekana mochari imejaa yaani hakuna nafasi tena.
 
Nipe maelekezo zaidi,ni akina nani hao na kwa faida ipi watapata
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…