The Sunk Cost Fallacy
JF-Expert Member
- Dec 1, 2021
- 19,582
- 14,167
Ndugu ukishaanza kusema hivi Tanzania hatuwezi kujenga sijui kununua tayari umeshafeli na ndio sababu mojawapo iliyotufikisha hapa kwa kukosa watu wenye maarifa..Habari wana JF
Nimejaribu kufuatilia kwa undani sana suala la shilingi ya Tanzania ukilinganisha na dollar pendwa ya Kimarekani ,kwanza tumsikilize huyu kiongozi kuhusu shilingi ya Unguja.
View attachment 2210979
Kama umsikia kwa Umakini kipindi hicho Shilingi 1 ilikuwa na thamani sana kulinganisha na Sasa, Lakini pia Ukipitia WORLD DATA ATLAS utagundua kwama miaka ya 1971 utagundua Shilingi zetu 7.1 ilikuwa sawa na dollar 1 ya kimarekani tofauti na sasa ambapo hiyo dollar 1 tunainunua kwa zaidi ya shilingi 2200.
Nimejiuliza sana kwanini imepanda kwa kasi kubwa hivyo Nikagundua Sababu kubwa ni kwamba HATUUZI NJE ,nikajiuliza tena ina maana hatuna vitu tunavyoweza uza Nje? Nikagundua pia tunavyo vingi mno.
Nikawaza pia sababu ni nini? Ni CCM au Watanzania wote nikabaki sina jibu
Hivi Wana JF Tanzania hatuweza jenga viwanda vya kutengeneza Nguo ,watu wakalima Pamba wakainua maisha yao Tukauza Nguo Nje?
Hivi wana JF Tanzania hatuwezi kusomesha watu na kujenga viwanda tukaprocess madini tuliyonayo tukauza vitu vitokanavyo na madini nje?
Hivi wana JF Tanzania hatuwezi imarisha Sekta ya Uvuvi kwa kununua vifaa vya Kisasa na kuwa muuzaji Mkubwa wa Samaki Nje?
Hivi Tanzania Hatuwezi jenga Viwanda vya Sukari ,na wananchi wetu wakalima miwa wakauza wakainua maisha yao na tukauza sukari Nje?
Hivi Tanzania hatuwezi jenga viwanda vya kusindika, watu wakalima mazao tukauza vyakula kwenye makopo
Hivi Tanzania hatuwezi jenga miundombinu mizuri, tukachimba tukauza Gesi Nje?
Hivi Tanzania Hatuwezi kuwa Muuzaji mkubwa wa umeme Africa Mashariki na kati kwa kutumia Gesi Tuliyonayo ,mito na bahari?
Hivi Tanzania hatuwezi jenga Bandari Kubwa sana tukawa wapokeaji mizigo wakubwa kwa Nchi zote zinazo tuzunguka?
Mwisho kabisa hivi hawa viongozi wetu huwa Tunawatoa wapi wanaopiga makofi hata kwenye hamna ,wananchi wanakufa kwa kukosa matibabu kwenye nchi yenye kila kitu? Kwanini Watanzania tuishi maisha magumu kwenye nchi yenye kila kitu?
Mi nadhani kuna haja ya kuwa na katiba ambayo mtu akiteuliwa ana akichaguliwa kuwa kiongozi anawaza mara mbili mara tatu ndio anakubali na hapa sio suala la kulaumu CCM kwa kuwepo kipindi chote hicho ila hao viongozi huwa tuna wachagua wenyewe.
Serikali haiwezi kufanya biashara ndugu,ukitaka watu waliokariri makaratasi wafanye biashara utaishia kupata hasara , nadhani tuna mifano mingi ila wa hivi karibuni ni korosho zilivyoharibiwa soko kwa serikali kujifanya wananunua na kupeleka malori ya Jeshi..
Jambo la muhimu ni kujenga mazingira wezeshi kama barabara,umeme na maji,taasisi wezeshi za serikali sio udhibiti tuu,kuacha urasimu na mlundikano wa Kodi lukuki na mwisho kuwa na malengo specific na yanayopimika na rasilimali zielekezwe huko sio kufanya mambo kiujumla jumla Bora liende.