Siasa za Tanzania, Shilingi ya Tanzania na Maisha ya Watanzania

Ndugu ukishaanza kusema hivi Tanzania hatuwezi kujenga sijui kununua tayari umeshafeli na ndio sababu mojawapo iliyotufikisha hapa kwa kukosa watu wenye maarifa..

Serikali haiwezi kufanya biashara ndugu,ukitaka watu waliokariri makaratasi wafanye biashara utaishia kupata hasara , nadhani tuna mifano mingi ila wa hivi karibuni ni korosho zilivyoharibiwa soko kwa serikali kujifanya wananunua na kupeleka malori ya Jeshi..

Jambo la muhimu ni kujenga mazingira wezeshi kama barabara,umeme na maji,taasisi wezeshi za serikali sio udhibiti tuu,kuacha urasimu na mlundikano wa Kodi lukuki na mwisho kuwa na malengo specific na yanayopimika na rasilimali zielekezwe huko sio kufanya mambo kiujumla jumla Bora liende.
 
Kama Nyerere na uzalendo wake wote ule alishindwa! Basi hakuna mwingine atakayeweza!

Labda atokee Nyerere mwingine (Nyerere Junior) mwenye maono na akili mara mbili ya zile za Nyerere Senior, hakika mambo yatakuwa bam bam.
Uzalendo mbuzi na kutumia rasilimali watu na mali eti kukomboa wengine badala ya kuwekeza kwenye elimu ya watu wake..

Huyo uliyemtaja na sera zake za kijamaa ni moja ya waliochangia kukuza ujinga na kuifanya jamii kusubiria serikali Kwa kila kitu na kulalamika.
 
Binafsi nilishasema moja ya Rais wa hovyo tuliowahi kumpata ni huyo mnaemuita JPM..

Sio tuu kwamba hakutekeleza hiyo miradi hata 50% bali mingi ya hiyo miradi ni useless na liability kwa Nchi..
 
Mpe Pongezi Kuna Mazuri Yake Pia Hao Wanaosema JPM muongo hata Wao Ni Waongo .

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Mwalimu aachwe
 
Ana zigo lake la lawama,anaweza kutetewa kidogo kwa sababu tuu hakujilimbikizia ila haiondoi ukweli kwamba aliasisi Taifa la wapiga poroja na kulaumu kuliko kuwa wabunifu.
Labda zigo litupiwe CCM
 
Tusiogope kukopa panapo hitajika
 
Shillingi 1 ya kenya ni sawa na 20.5tsh mwananchi wa chini akiwa na15ksh ambayo ni sawa na 300tsh anauwezo wa kupata kikombe cha chai na makande maisha yakasogea,kwa upande wa bongo hali ni tofauti...
Kenya wake mbele na serious kuliko kwetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…