Siasa za Tanzania: Ukabila na Ukanda sasa rasmi, mwanzo wa kuanguka umoja wa Kitaifa-Uchaguzi wa CCM umedhihirisha!

Siasa za Tanzania: Ukabila na Ukanda sasa rasmi, mwanzo wa kuanguka umoja wa Kitaifa-Uchaguzi wa CCM umedhihirisha!

masopakyindi

Platinum Member
Joined
Jul 5, 2011
Posts
18,207
Reaction score
13,839
Sisi tulio makabila madogo na tulio pembezoni, tulionya sana katika miaka y karibuni juu ya kujitokeza vashiri vya Ukanda, Udini na Ukabila katika siasa za nchi.

Sasa zimeanza kujitokeza dhahiri na kwa kila mtu kujionea kwa macho yake yanayoendelea nchini.

Kama kuna kielelezo kinajitokeza ili kila mtu akione ni uchaguzi wa CCM kwa kuwania viti vya NEC.

Kwa princile ya wengi wape basi nchi hii itatawaliwa na watu toka pande fulani tu za nchi.

Tunajua mambo haya kuanzia uchaguzi huu, tulianza na "Mitandao" Awamu ya Tatu na NNe, na Awamu ya Tano ndio ikawa funga kazi, Mwenyekiti wa CCM aliyekuwepo na Rais vile vile alipendelea wazi wazi "wale waliomchagua".

Kama tulikuwa tunaisikia tu Apartheid kwa makaburu -yaani maendeleo ni kwa majimbo fulani tu, sasa laana hii ipo nchini.

The writing is on the walll, umoja wa kitaifa umeanza kupata nyufa.
IMG-20221216-WA0024.jpg
 
Uchaguzi wa NEC ulikuwaje kikabila? Wajumbe si walitoka pande mbali mbali za nchi na Kwa uwiano Sawa kiuwakilishi, sasa wamependelewa kivip? Tukubali tu kuwa kuna kanda zpo vzuri katika kilimo, kuna kanda zipo vizur katika biashara na kuna kanda zipo vizuri katika siasa!
 
Hao wanojisifu wapo wengi, watashangaa, wanaoamua Rais wa Tanzania awe nani ni kamati kuu ya CCM chini ya Rais na wazee kama Kikwete, wao ndio wanaoamua wakate jina la nani waache jina la nani
Lowassa alinunua 80% ya wajumbe wote, lakini kamati kuu ikamchinjia mbali

Nyie mnaojisifia mpo wengi tumieni wingi wenu kupata katiba mpya itakayowapa nguvu wananchi kuchagua kiongozi wanayemtaka, hapo ndio mtaweza kutumia huo wingi wenu kuwa kura, ama nchi itakuwa chini ya Familia chache tu
 
Hao wanojisifu wapo wengi, watashangaa, wanaoamua Rais wa Tanzania awe nani ni kamati kuu ya CCM chini ya Rais na wazee kama Kikwete....
Wewe na huyo kiwete wako ndio mtakaoshangaa. Nyie mmekua kina nani mtuamulie waTanzania mtu wa kutuongoza?

Wakati jina la Maembe binamu yake huyo kiwete linakatwa 2015 mpaka rais anakua JPM huyo kiwete alikua hajaanza hizo shughuli za kuamua nani anakua rais Tz? Nyie subirini tu tunawaangalia tunachekea pembeni
 
kanda zipo vizuri katika siasa!
Ukanda wa pwani uko vizuri kisiasa. Kanda nyingine mtaburuzwa mpk mtaita maji "mma".

Huyo Nyerere mwenyewe alitoka uzanakini huko na kukimbilia kuomba msaada wa wazee wa Pwani ktk harakati zake.

Akina Abdallah Hanga, mzee Sykes, Bibi TIti Mohammed, n.k ni baadhi tu ya majina ya watu wa Pwani waliomsaidia Nyerere ktk mapambano.
 
Hao wanojisifu wapo wengi, watashangaa, wanaoamua Rais wa Tanzania awe nani ni kamati kuu ya CCM chini ya Rais na wazee kama Kikwete, wao ndio wanaoamua wakate jina la nani waache jina la nani
Lowassa alinunua 80% ya wajumbe wote, lakini kamati kuu ikamchinjia mbali

Nyie mnaojisifia mpo wengi tumieni wingi wenu kupata katiba mpya itakayowapa nguvu wananchi kuchagua kiongozi wanayemtaka, hapo ndio mtaweza kutumia huo wingi wenu kuwa kura, ama nchi itakuwa chini ya Familia chache tu
Chambua mada vizuri, hapo hakuna ulichojibu! Mwenye Uzi anaonya juu ya ukanda, Kwa jinsi ulivyojaribu kuchangia mkuu, hujatoa tahadhari juu ya hao wanaokata majina ya wagombea bila wao kuweka hofu juu ya wajumbe wenye kupiga kura zao na huku wakiwa wanafahamiana kupitia uwingi wao ndani ya Nec,

Unadhani watamuacha salama anayekata majina kisa eti jina llililopata kura nyingi ni la kabila Fulani,

Mambo yakiwa ni ya kikabila, tegemea mkono utatembea vizuri tu hukohuko kwenye nec
 
Asante mkuu.
Kuna watu wanajidai hawalioni hilo tatixo alimradi wanafaidika kwa wingi wao.

CCM isipokuwa makini ,itajitengenezea matatizo ambayo hitaweza kuyatatua siku za usoni.
Ukabila, Ukanda ni lazima vitaimaliza CCM.
 
Chambua mada vizuri, hapo hakuna ulichojibu! Mwenye Uzi anaonya juu ya ukanda, Kwa jinsi ulivyojaribu kuchangia mkuu, hujatoa tahadhari juu ya hao wanaokata majina ya wagombea bila wao kuweka hofu juu ya wajumbe wenye kupiga kura zao na huku wakiwa wanafahamiana kupitia uwingi wao ndani ya Nec,

Unadhani watamuacha salama anayekata majina kisa eti jina llililopata kura nyingi ni la kabila Fulani,

Mambo yakiwa ni ya kikabila, tegemea mkono utatembea vizuri tu hukohuko kwenye nec
Kwani watafanyaje? Kwani wale wafuasi wa Lowasa walifanyaje!

We hujui hata wananchi hawana muda na hizo siasa, wao watakachoambiwa na serikali ndio wanashika, sasa upo kwenye chama ujaribu kuleta uasi uone

Kamuulize Ndugai na Bashiru
 
Ukandamizwaji kwenye chama ndio chimbuko la uasi, usijivunie hilo mkuu
 
Ukandamizwaji kwenye chama ndio chimbuko la uasi, usijivunie hilo mkuu
Mimi sijivunii, naongea uhalisia ulivyo.
Kwa katiba ya CCM ilivyo, na Katiba ya nchi ilivyo na wananchi wa Tanzania ambao interest yao kuu ni mpira wa simba na yanga na udaku,
Hakuna mtu anayeweza kuitikisa serikali kwa sasa na miaka mingi ijayo, hata awe na umaarufu gani

Nikuulize swali simple tu, Magufuli alipofariki, na kuacha maswali mengi, kuna mtu hata mmoja alijaribu kuhoji? Kama Rais aliyekuwa na nguvu vile alifariki kwa mazingira yale na hakuna aliyehoji, kipi kikubwa zaidi watakachohoji?
 
Kama nawe umeliona Hilo,

Katiba mbovu ndo imeleta nyufa hizo.

Tuungane pamoja kumpambania KATIBA mpya itokanayo na Rasimu alosimamia Judge WARIOBA.

Aamen.
 
Back
Top Bottom