Siasa za Umeme: Kwa vile Umeme wa Stigler's utatosha na ziada kuuza nje. Je, TANESCO kusaini PPA mpya 6 toka kwa 6 IPPs, sio ufisadi mpya wa kisasa?


Rais huyu alikuwa waziri kwenye serikali iliyokuwa inatuimbisha umeme wa gas kama wendawazimu, mbona hakugoma wakati ule kuwa tunaingia kwenye umeme wa bei ghali? Kwahiyo hiyo $6.5 ya umeme wa maji, kama ingeingizwa kwenye gas tusingepata hizo 2,115mg?

Jitahidi za kuambiwa uchanganye na zako. Unapoona miradi mingine mchepuko huku kukiwa na mradi mkubwa unaodanganywa ni pesa za ndani, kisha wachina wanaitwa, ujue unaingizwa town.
 
Itategemea TANESCO wanauziwa kwa kiasi gani? Kama ni chini ya market price na ni sawa huu umeme ukaunganishwa kwenye grid ya Taifa.

Huu umeme unatoka kwenye clean, green, renewable and sustainable sources. If it make financial, economiical and enviromental sense then more people should be encouraged to do similar thing.

Nchi nyingi tu zinafanya hivyo. Familia, watu binafsi wenye solar panels kwenye paa kwenye nyumba zao wanaunganishwa na kuuza spare capacity kwenye national grid.

Matumizi ya umeme yanategemewa to double ndani ya miaka mitano na kuongezeka zaidi ndani ya miaka 20 -30 ukizingatia kwamba Tanzania population inakadiliwa kufika zaidi 137m ndani ya muda huo

Viwanda, kilimo cha kisasa, makazi, SGR, trams, electric cars, majengo ya ofisi n.k yatahitaji umeme mwingi zaidi.

Umeme wa ziada utauzwa kwa majirani kama Uganda, DRC, Malawi, Zambia, Burundi, Rwanda.
 
Hao wazalishaji wadogo walikuwepo muda mrefu lakini tanesco na serikali zilizopita zilikuwa haziwapi umuhimi unaostahili.
Cha muhimu wawe na gharama rafiki sio kama zile zilizokuwa kwenye mikataba iliyopita ambazo nyingi zilikuwa za mwelekeo wa kifisadi
 
Niliwahi kusema kuwa; ogopa sana serikali inayopenda kufanya mambo kwa vificho na usiri, kuna mabaya sana inaficha ndio maana kila kitu ni siri. Awamu hii ikiisha 'yatakayoibuka' ndio mtabaki midomo wazi.
 

Ukitaka kujua unaingizwa mjini kirahisi, angalia hii hesabu. Tulikopa $1.2b ili kujenga bomba la gas toka Mtwara mpaka Dar na kuna vinu vinavyozalisha 300mg+ mpaka sasa. Je $6.5b ingeingizwa kwenye umeme wa gas ambao tayari bomba lipo, tusingepata umeme mwingi zaidi ya hiyo 2,115mg iliyoingizwa kwenye umeme wa SG? Fuatilia vizuri kama huu mradi wa umeme wa SG upo kwenye mpango kazi wa TANESCO. Unapoona watu wananajisi uchaguzi, ujue lengo hasa ni kuwa na bunge kibogoyo, ambalo halitakuwa na uwezo wa kuhoji huo upigaji.
 
Yaani Paskali licha ya huo mradi wa Mwl Nyerere hujamsikia Magufuli juzi anatafuta mkopo wa kujenga mitambo mingine Njombe yenye uwezo wa kuzalisha megawatt zaidi ya 300?
Mahitaji ya umeme yanakuwa kwa kasi na huwezi kujiwekea limit..(chukua Ethiopia kama case study)
Hata hivyo hizi kampuni ni za wazalendo sio za waleeee.
 
Paskali, Vyanzo vya umeme mbali mbali vitahitajika ili kukidhi matumizi ya mwananchi.
Sera ya Umeme karibu maeneo mbali mbali duniani ni Umeme wa uhakika usiokatikakatika,umeme nafuu,umeme utokanao na vyanzo pendwa kwa mazingira.

Kwa matumizi ya nyumbani,mataifa kionambali kwa sasa yanafagilia nyumba ziezekwe kwa mabati yenye solar.Hii ndio suruhisho la kukwepa black-out ya jumla kwenye makazi ya watu.
Sio muda mrefu tutashuhudia magari yanayotumia battery badala ya engine ya mafuta.Lakini battery hizo zinahitaji charge itokanayo na umeme.Ni wazi itahitajika umeme mwingi kutosheleza mahitaji ya magari.

Kwa vile Tanesco imejikita kuzalisha umeme wa mitambo mikubwa,ni bora kampuni nyingine zikashindana na Tanesco kutoa huduma ya umeme nafuu hasa pale Tanesco anaposhindwa kuwafikia walengwa.
Lakini isije ikageuka sungura akamwinda mbwa mwitu.Songas ni mfano hai.
 

Tanzania tuna vyanzo vingi vya umeme na bado hatujaanza kuvitumia ipasavyo,tukienda kwenye umeme wa maji haimaanishi tumeachana na gesi kuna mambo mengi ya kihandisi(ufundi) na kiuchumi tunaangalia.

Mfano mwaka 2008, 4,414 GWh ya umeme wa gridi ilizalishwa nchini Tanzania, kati ya hiyo 2,655 GWh kutoka umeme wa maji, 1600 GWh kutoka gesi asilia, 119 GWh kutoka makaa ya mawe na 40 GWh kutoka mafuta ya petroli. Jumla ya uwezo uliowekwa ulifikia MW 1,219, ambapo MW 561 ilikuwa umeme wa maji na nguvu ya mafuta ya 658 MW. Uwezo uliowekwa mnamo 2019 ulikuwa 1565.72MW yenye hydro 573.70MW, gesi asilia 892.72MW, mafuta ya kioevu 88.80MW na biomass 10.50MW [Wizara ya Nishati Juni 2020].

Kufikia sasa 73.2% ya mijini na 24.5% ya maeneo ya vijijini wamepatiwa umeme [Wakala wa Nishati Vijijini Aprili 2020].

Matumizi ya umeme wa gas ile tuliyokuwa tunaimbishwa uchumi wa gas kama wendawazimu yameishia wapi?
 

Tunashukuru kwa huu umahiri wako wa kutaja mahitaji ya umeme hapa nchini kwa sasa, na muda kidogo ujao. Kabla ya Magufuli kuingia madarakani wakati huo yeye akiwa waziri, kuna wimbo almanusura tuwe vichaa wa umeme wa gas sijui uchumi wa gas. Mbwembwe za washangiliaji wa wakati huo ilikuwa ni kwamba bomba la gas lazima lifike Dar taka tusitake, hadi watu wa Mtwara wakapoteza maisha kwenye slogan iliyokuwa ikisema inatoka ama haitoki. Wanaoshabikia umeme wa maji wa sasa ndio waliokuwa wanapaza sauti za juu kuwa tutapata umeme wa 5,000m hadi kuuza nje ya nchi.

Cha ajabu kaingia rais aliyekuwa anaimbisha kwaya ya umeme wa gas wa 5,000mg, anaanza na mradi mdogo wa kufua umeme wa maji 2,115mg waliosema gas ndio yenyewe kwani maji tatizo ni mabadiliko ya tabia nchi! Ujenzi wa bomba la gas mpaka kufika Dar tulikopa $1.2 ambapo Zito alisema bado bei hiyo tumepigwa, na akatoloewa kebehi zote. Ukitaka kujua watanzania tunaonekana wajinga na viongozi wa ccm, tunaachana na umeme wa gas wa kuzalisha 5,000mg, kisha tunakopa $6.5 kuingiza kwenye umeme wa maji wenye tatizo la mabadiliko ya tabia nchi wa 2,115mg!

Kundi linalofanya utapeli huu, ni kundi lilelile la 5,000mg za umeme wa gas, lakini hili limekuja likiwa limejipodoa na kuvaa vazi la uzalendo! Je kama sio tunachezewa shere na hili kundi la wezi wa kura, tungeingiza hizo $6.5 kwenye gas ambayo miundombinu iko tayari, tusingepata umeme mwingi zaidi ya huo wa maji wa 2,115mg? Kwa mujibu wa mtiririko wako na hayo mahitaji, hata umeme wa SG ukikamilika, bado mahitaji yanazidi, ama wameacha nafasi ya serikali nyingine ikiingia kwa wizi wa kura, wapate sehemu ya ulaji kwa kuanzisha miradi mingine ya umeme?
 
Upo ukweli P katika bandiko lako hili.

Ni kama mto Ruvu tu, unaona ni kama unanyooka hivi, halafu badaye ni kama unaruudi tena nyuma.

Tanzania ni nchi ya ajabu, kunamahali tunaweza kuamua kupiga hatua, halafu Wakati mwingine mara turudi nyuma tena!
Waache tu Tanesco waendelee na mipango yao ila wasiguse nyaya za mkuu. Kutalipuka.
 

Hili wazo lako la TANESCO kupata mshindani ni wazo zuri sana, lakini kwa hizi nchi zilizo na mizizi ya kikomunisti na utawala wa chama kimoja, usishangae TANESCO maana ni taasisi ya umma ikiendesha ushindani wa biashara dhidi ya makampuni binafsi, kwa mtindo wa ccm dhidi ya vyama vya upinzani. Unaweza kushuhudia aina chafu sana ya ushindani kwenye soko la umeme.
 

Ulichofanya hapa ni umahiri wa kutaja MW katika sehemu mbalimbali, na hukuwa na haja ya kutaja mifano ya zamani, wakati tulishafikia suluhisho la nishati kuwa ni umeme wa gas, ambao tungepata 5,000mw. Kuna haja gani ya kuonyesha umahiri wa kutaja hivyo vyanzo wakati 5,000mg kwenye umeme wa gas tungemaliza mahitaji yetu wangalau kwa 20yrs to come? Sitaki unizungushe zungushe kama sina ufahamu wowote, je tungeingiza hizo $6.5b kwenye umeme wa gas, tusingepata umeme mwingi zaidi ya 2,115mw. Sitaki maelezo nje ya hapo fullstop.
 
TANZANIA KUFUNGUWA SHIIRIKA LA KAZALISHA UMEME NA KUJENGA NJIA ZAKO ZA KUSAFIRISHA NA KUUSAMBAZA UMEME NA KUUZA KWA WATEJA NI RUKSA, RUKSA, RUKSA

Hawapati faida kwenye umeme, na uwekezaji ni mkubwa na ni ghali. Lakini hawataki kupigwa kwa kuuziwa umeme Ambo wao wanauona ni ghali .
 
Hapana mkuu,umefika mbali sana kufikiria kuwa kuna pesa nyingi zilizofujwa katika hili.Lakini kama unakumbuka mamlaka husika waliotoa ufafanuzi wa kina juu ya hatma ya Gas ya kule Mtwara.Pesa walizokopa zilitumika kwenye mambo mengi ta kulipa watafiti wa kimataifa, na maandalizi ya awali . Suala hili lipo wazi kabsa na watu wengi wanafaham.
Je,haukusikia ufafanuzi juu ya hili mkuu ??
 

Kwa post hii uko sawa kabisa. Sasa nijibu hiki nitakachokuuliza kwenye hii post. Tunawekeza $6.5b kwenye bwawa la SG kufua umeme wa 2,115mw. Lakini kabla ya awamu hii tulikuwa na umeme wa gas ambao tayari bomba liko hapa Dar. Kwenye ujenzi wa hilo bomba hadi Dar tulikopa $1.2b na tunazalisha zaidi ya 300mw mpaka sasa. Je ni kwanini tunawekeza $,6.5 kwenye mradi mpya wa maji ambao tuliambiwa tatizo ni mabadiliko ya tabia nchi, tuache kuwekeza kwenye umeme wa gas ambao tayari tumekopa $1.2b, na miundombinu imekamilika? Je hizo $6.5n tusingepata umeme mwingi zaidi ya hizo 2,115mw? Nahitaji majibu hapo kwani siasa haina nafasi hapo.
 

Mkuu ninajua huna majibu kwa nilichosema, ila nilitaka kukuonyesha kuwa huwa unashabikia mambo marahisi. Kama $1.2 zilitumika kulipa watafiti, kujenga bomba mpaka hapa Dar na zinazalisha umeme 300mw+ mpaka sasa. Je $6.5b iliyoingizwa kwenye bwawa la SG zingeingizwa kwenye gas ambapo tayari miundombinu imekamilika, tusingepata umeme mwingi zaidi ya 2,115mw? Huo unaoita ufafanuzi kutoka mamlaka husika ungekuwa nao ungeutoa, lakini kwakuwa umejikita kwenye siasa nyepesi, ndio maana unasema sikusikia ufafanuzi?

Kwa taarifa yako huu sio uzi wa kwanza kuhusu sakata la umeme, na mara zote hakuna majibu stahiki zaidi ya porojo. Ukiachia ww, kuna wenzako zaidi ya mmoja huku ndani nimewauliza swali kama ww, lakini hakuna hata mmoja mwenye jibu zaidi ya kupotea. Na watu wa mamlaka husika, huu uzi wanaouna kama walivyoona nyingine lakini wakapotelea mbali, na waliojaribu kujibu waliishia kuleta vioja. Ukitaka kujua ni kuingizwa mjini, ukienda kwenye vikao vya ccm nenda kahoji mambo haya, hutapata majibu, na ukilazimisha kupata majibu uwaambie kabisa ndugu zako ukifa uzikwe wapi.
 

Hoja yako ni nini hapa Gerald?
 
Mkuu Pascal mi naona Tanesco wako sahihi kabisa. Hiyo total ya 3700MW unaiona kubwa lakini ni ndogo mno. South Africa total ni 58000MW, Misri total ni 24000MW. Ethiopia bwawa lao moja tu litatoa. MW 6000!.. bwawa la Three gorge la China linazalisha Mw 29,000.

Tunahitaji umeme toka vyanzo vyote tunavyoweza kupata. Nimewahi andika hapa kuwa tuzalishe kupitia microhydro dams. Tuzalishe umeme nchi nzima. Tuwe hata na installed capacity ya 10, 000MW. Viwanda huwa vinafuata umeme wa uhakika na wa bei rahisi. Nasikia chai kutoka EA nyingi inaenda kuwa processed Egypt sababu hiyo ya umeme. Viwanda vingi vinawekwa South sababu hiyo.
Nashauri Tanesco wahamasishe watu binafsi wengi zaidi kuzalisha umeme na wao wasiwe na mizengwe wakati wa kununua na kulipana.
 
kwamba niwambie nitazikwa wapi๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚..
Pamoja katika ujenzi wa taifa.goja nitafte fact 100% then nakuja hapa tena.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ