Siasa za Umeme: Kwa vile Umeme wa Stigler's utatosha na ziada kuuza nje. Je, TANESCO kusaini PPA mpya 6 toka kwa 6 IPPs, sio ufisadi mpya wa kisasa?


Asante sana mkuu, hata hiyo dhana kuwa umeme wa maji ni nafuu sio kweli, maana kabla ya umeme huu wa gas na mafuta mazito, tulikuwa tunatumia umeme wa maji. Mbona bado katika nchi za Afrika mashariki umeme kwetu ulikuwa ghali? Kwa sasa kwenye umeme huu wa maji hakuna mwenye uhakika kuwa ni fedha za ndani, kama hata fedha za ujenzi hakuna mwenye uhakika kuwa ni fedha za ndani, kuna uhakika gani kuwa umeme huo wa maji utakuwa bei nafuu?
 
Mkuu swala la uchaguzi tuliache kwanza tutalileta baadae. Kama ulisikia hotuba ya JPM Dodoma 2015 baada ya kuapishwa utaelewa maana yake ya kukaa kimya. JPM alikuwa anayajua maovu yooooote na madili yoote hadi kwenye hotuba yake alisema watu walikuwa wanafungulia mabwawa ya maji kusababisha mgao wa umeme. Ila Kama Waziri wa ujenzi angebadili nini!?, Wengi wanakurupukaga kwa kuhama chama kumbe ndo wanapotea. Vita inapiganwa humohumo. We unaamini mapapa ya nchi hii yasiyogusika kipindi kile akina Kinana,Makamba,Seth, Rugemalila, Manji,Mengi, Patel nk yangenywea!???... Unajua jinsi gani yalishikilia wizara zote na uchumi wa nchi?.. turudi kwenye mada. Angemkemea JK kuhusu gesi nini kingetokea!??.. Je angekuwa bado ana chance ya kurekebisha aliyorekebisha awamu hii au angeishia kuondolewa kwenye uwaziri na kubaki huko chini wizarani,na pengine Membe au Makamba akawa Raisi 2015, tembo zikaendelea kulia,mateja yakaongezeka hadi watoto wa sekondari. Hebu ruhusu kufikiri nje ya fikra zako za kipinzani mkuu..
 

Uko sahihi sana na hoja yako naiona katika uwanda mpana sana. Sasa tuje kwenye uhalisia, je unataka kusema hakuna uwezo wa kuhoji ama kuzuia uovu wowote bila kuwa rais? Je ingetokea asiwe rais, tungeendelea kupigwa kwa muda gani? Wtf na yeye anatupiga sasa, lakini watu wanamkalia kimya kisa ni rais? Huo mfano wangu wa uchaguzi nimeutoa kwasababu kinachofanyika sasa ni kwasababu rais anaweza kufanya lolote, kama hilo kundi lililotupiga bila kufanywa lolote, kwakuwa lilikuwa na kinga ya rais mpigaji.

Hakuna mtu muadilifu kisha akawa hataki uwazi, ukiona mtu hataki uwazi, inabidi ujitoe ufahamu kumuamini. Katiba ni kipimo cha kiongozi muadilifu, je yeye anakubali kufanya kazi kwa katiba ya wananchi, ni wazi hayuko tayari, mtu wa aina hiyo unaweza kuweka imani yako kwake vipi? Au hapa unaleta mambo ya muwamba ngozi?
 
Kila mtu atajikuna pale anapoweza.
 
tusapoti vya NYUMBANI
 

Unajua wakati mwingine jamani Tanzania tuwe tunasema UKWELI kwa kuwa UKWELI tu utatuweka huru.

Hivi ni kweli kwamba mradi wa umeme wa Nyerere Hydroelectric utakuwa umekamilika na kuwashwa mwaka 2023? Mimi siyo mwanasayansi, lakini huwa nasoma na kuelewa. Mradi wa Mtera wa HEP ulitumia takribani miaka 7 kukamilika, Na huo haukuwa mradi mkubwa saaaana kama ulivyo wa Nyerere HEP. Je, ni ukweli kufika 2023 Bwana la Maji, litakuwa limekamikika, mitambo ya kufua umeme itakuwa imefungwa, serviceline zitakuwa zimejengwa na umeme utakuwa umewashwa?

My take
Ninaomba watanzania tuache mbwembwe za siasa tuwe realistic katika mipango yetu.

Kwa mantiki hiyo ndiyo maana TANESCO bado inahitaji kununua umeme toka vyanzo vingine kwa kuwa technically wanajua haiwezekani Nyerere HEP project itakamilika ndani ya miaka 4. Kama mradi huu utakamilika na kuanzia kutoa huduma inayokusudiwa tuhesabu miaka 7 hadi 10 (2027 hadi 2030).
 
Pascal umedadavua vizuri sana kuhusu suala hili. Halihitaji elimu ya ufundi umeme bali logic thinking ya mtu ye yote mwenye akili ya kutosha. Akili ya namna hiyo haipatikani chuoni bali mtu huzaliwa nayo. Tanesco hawataweza kujitokeza humu kutoa a convicing reason kwa hicho walichokifanya; cha kuanza kununua umeme kwa hawa wazalishaji wadogo wadogo kwa bei wanayoijua wao halafu kutuuzia sisi kwa lazima kwa bei wanayopanga wao! Bahati mbaya kwa forum hii ya Jf pekee sidhani kama serikali itaiona na kuipa uzito inayostahili. Ungalimtumia mmoja wapo wa wabunge wetu (chagua mbunge ye yote machachari hasa wa upinzani ikiwezekana) kulifikisha bungeni kuihoji serikali kuhusu jambo hili, ninaamini serikali itavunja mikataba hiyo na baadhi ya watendaji wa Tanesco watatumbuliwa. Halima Mdee ni mmojawapo ya wabunge wangaliofaa kwa kazi kama hiyo.

Ni ukweli ulio wazi kwamba:
1. Kwenye grid yetu ya taifa kwa sasa tuna umeme wa MW 1,650. Matumizi yetu ya sasa ni wastani wa MW 1,100. Kwa hivyo hadi sasa tuna ziada ya MW takribani 550 ambazo ziko iddle kwenye grid yetu ya taifa zikisubiri wawekezaji kwenye viwanda, umeme vijijini na kadhalika. Na hapo Kinyerezi upanuzi unaendelea wa kupata MW 300 zaidi hivi karibuni.

2. Hivyo hizo MW 19 kutoka kwa wazalishaji wadogo wadogo kwenye grid yetu ya taifa hazihitajiki. Tanesco itakuwa inawalipa hao watu mabillioni ya pesa kwa kitu ambacho haikihitaji. Pesa hizo ilitakiwa kuitumia kujenga miundo mbinu ya kusambaza hizo MW 550 ambazo ziko iddle kwenye grid ya taifa. Tanesco inapaswa kupunguza bei yake ya umeme ili iweze kuziuza hizo MW 550 zilizo iddle kwenye grid. Kwa sababu ya bei mbaya ya umeme wa tanesco wengi wetu tulishazima majiko yetu ya umeme yenye oven, grill and 4 plates na badala yake tunatumia mikaa. Hizo bei zao wakizipunguza majiko yetu tutawasha na wao watapata pesa kutoka kwenye huo umeme waliokaa nao iddle.

2. Haihitaji akili ya ziada kujua kuwa hicho walichofanya ni kutengeneza uchochoro wa ufisadi kuturudisha tulikotoka kwa akina iptl, simbion nk.

3. JPM kuwaambia wawa support wazalishaji wadogo haikumaanisha waununue umeme wanaouzalisha. Kuna wazalishaji na wasambazaji wa maji wadogo wadogo, wasambazaji wa cable tv stations etc. Wanatakiwa kuwa supported. Hawa wazalishaji wadogo wa umeme wanatakiwa wausambaze kwa wateja wao moja kwa moja. Mtu unaamua utumie umeme wa tanesco au wa mjasiliamali fulani. Mtu anatakiwa aamue atumie mtandao wa simu wa tigo au vodacom au tccl. Atumie king'amuzi cha azam, tbc au star tv etc Serikali inachopaswa kuwapa wajasiliamali hao ni technical support ie kuwawezesha kiufundi, si kununua bidhaa yao. Serikali jukumu lake ni kuhakikisha hizo bidhaa kutoka kwa wajasiliamali hao zinaviwango unaokubalika na ni salama kwa wateja wao. Serikali kazi yake ni kukusanya kodi stahiliki kutoka kwa wajasiliamali hawa.

4. Wazalishaji hawa wadogo wadogo wamekuwapo miaka mingi tu nawamekuwa na wateja maeneo yao ambayo tanesco ilikuwa haijafika. Kwa mfano katika kijiji changu miaka kama 30 iliyopita jamaa mmoja alikuja na generator kubwa ya umeme kama zile.zinazotumika mahospitalini kama standbye generator ambazo zina uwezo wa kuwasha mashine kubwa kubwa za mahospitali kama za X-ray na CT scans ambazo hutumia umeme mwingi. Jamaa huyu aliifunga generator hiyo kijijini na kuweza kuwasambazia umeme wanakijiji wote kwa sababu matumizi yao ni hasa kwa ajili ya taa tu usiku ambazo hazitumii umeme mwingi. Wanakijiji hao walikuwa wakimlipa kiasi fulani cha pesa kila mwezi ambazonzilimuwezesha kuishi vizuri. Ujio wa umeme wa REA umemuharibia biashara yake kwani umeme wa REA bei yake ni ndogo. Hivyo atafurahi sana kama tanesco watakuwa wanaununua huo umeme wake na kuuuza kupitia grid ya taifa. Kama ni hivyo wote tukubaliwe kuwauzia huu umeme mdogo mdogo ambao tunaweza kuuzalisha majumbani kwetu.

5. Tanesco isitake kuwa a tanzania national electricity purchasing and supplying company. Inakiwa iwe a tanzania national electricity generating and supply company. Sisi ndiyo tutakao purchase huo imeme kutoka kwao au kwa mzalishaji mwingine ye yote tutayeona anatufaa. Tanesco wanapaswa kushindana kibiashara na wazalishaji wengine binafsi wa umeme.
 
Mkuu Kuna Mambo mengi sana mmekaririshwa tu, mfano Katiba mpya,sijui tume huru ya uchaguzi,demokrasia etc. Matatizo ya nchi za Africa karibu zote hasa za watu weusi ni yaleyale. Matatizo ya watu weusi waliobakia nje ya Afrika ni yaleyale karibu nchi zote kuanzia USA, Brazil,Papua New Guinea,Jamaica etc. Turudi Afrika mashariki. Mnadai Kenya Wana tume huru na katiba mpya mbona kabla ya uchaguzi uliopita kiongozi wa tume ya uchaguzi aliokotwa kafa na kidole gumba cha kutumika kwenye mfumo wa fingerprint kimekatwa!?.. Africa ni umafia tu. Ndo maana wengine tunaamini kwenye watu sio vyama. Hata uweke katiba ipi,tume ipi, mfumo upi as long as ni hizi nchi zetu za watu weusi kama kiongozi aliyepo sio mkali Mambo ni yaleyale. Mimi hutakaa uniaminishe eti Chadema ikiingia madarakani maisha ya watanzania yatabadilika. NEVER. WHY!??.. Hulka ya wanaoongoza ni ile (Selfish,roho mbaya,njaa,asili ya umaskini,majivuno, ulimbukeni nk) na wanaoongozwa hivyo hivyo(njaa,umaskini, ujinga, kukosa Elimu,kupenda ngono,kuzaana hovyo nk). Hata ije CDM,CUF,ACT,CHAUMA as long as viongozi ni weusi na wanaoongozwa ni weusi NO CHANGES. So, wengine tunamuona angalau JPM ana moyo wa kukemea na kumaanisha. Sasa kumuamini au kutomuamini inabaki kwa mtu binafsi. Kama dini vile.
 

Nimecheka kwa nguvu huu utetezi wako. Tunataka katiba mpya sio ili cdm iingie madarakani, bali tunataka anayeingia madarakani awe ni yule anayekubalika na wengi. Hatutegemei kupata viongozi malaika, bali tunataka mifumo madhubuti. Kwenye hiyo katiba ya Kenya ni kweli hakuna malaika, ila mifumo yao ina afadhali kuliko hapa kwetu. Sisi wengine sio waumini wa ukali wa mtu, bali uimara wa mifumo na taasisi imara. Magu anakemea kwa double standard, kiasi kwamba inageuka kuwa ni mtu anayeongozwa na chuki binafsi na visasi. Lakini ingekuwa kuna mifumo imara tungeona bunge likifanya kazi yake kwa mujibu wa sheria, na mahakama ingetekeleza wajibu wake, na wala mahakama zisingetumika kama sehemu ya kukomoa watu wasiopendwa na watawala.
 
Hutakiwi usome post zangu maana utaugua wendawazimu. Post zangu ni pasua kichwa, nakushauri achana nazo kabisa. Naona uko na id zako mbili, ile ya tatu mpya nayo umeamua kuikaushia?
Kwa nini unaishi kama mganga wa kienyeji karne hii ya science na teknolojia? Unaishi kwa kubashiri na kupiga ramli? Jikite kwenye mada husika huku ukiweka post zenye mashiko,sio pumba ambazo hazina mbele wala nyuma.
 
Kijana tuliza munkari na utafakari kabla ya kuchambua mambo, nini kinachokufanya uproject kuwa huu mradi wa JNHEP utachelewa kuisha? Wakati Mtera inajengwa, je tulikuwa na utashi wa kisiasa kama leo hii? Maana kama tunge kuwa na good political will toka mwazo huu mradi ungekamilika hata miaka 30 iliyopita.

Usituletee mifano ya kitoto wakati sisi ni watu wazima. Kujenga Hdro plant hakuna complication kama unavyodhania, zaidi ya kutengeneza tunnels za kupitishia maji kuyachepusha, kutengeneza bwawa na kusimika power house. Jambo ambalo mpaka sasa linaenda vizuri maana wameshaanza harakati za kuchepusha maji kutengeneza bwawa.

Lakini ninachotaka kukuambia ni kuwa utashi wa kisiasa na kuwa na viongozi makini wanaosimamia mapato ya taifa ndio suruhu ya kukamilisha miradi kama hii, na hili linawezekana. Kwa hiyo usiseme huu mradi hauwezi kukamilika ndani ya wakati.
 
Dogo, usitumie nguvu nyingi sana na kukaza misuri kuelimisha watu wa namna hii.
 
Tutofautishe installed/capacity au generated energy capacity na delivered energy capacity. Umeme unaozalishwa siyo wote unamfikia mlaji/mteja. Lazima ujue kuna capacity factor ina husika hapo. Yaani capacity factor ni uwiano wa matumizi na uzalishaji wa umeme kwa muda maalumu waweza kuwa kwa mwezi ama mwaka. Vyanzo/miradi ya umeme ina capacity factor tofauti. Umeme wa Maji ukiwa na capacity factor ya juu.
 
Tatizo la P siku hizi ni kukosa msimamo!! (Unafiki) tulishasema ccm ni majizi!! yeye akaanza kutetea!! leo amekosa teuzi. amekuja na mada ya umeme!! anaweza kuwa sahihi!! lakini watu hawatamuamini tokokana na tabia yake ya kukosa msimamo!!
Asipotulia atakosa ukuu wa wilaya au ukatibu tawala wilaya utakaotangazwa soon mwakani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…