Hii sio fact, hayo ni maoni yako.
Sote tunajua duniani kote umeme wa maji sio jambo la kudumu, kadri muda unavyokwenda na mabadiliko ya tabia nchi basi na nguvu ya kuzalisha umeme kwa kutumia maji inapungua.
Upande wa pili, kuzalisha umeme kwa kutumia maji kuna kwenda sambamba na uharibifu ya ikologia ya viumbe hai.
Jambo moja kuu kuhusu umeme wa maji ni cheaper but limited. Gharama iko kwenye kuwekeza zaidi kuliko uendeshaji wake lakini hawezi kuzalisha zaidi ya kiwango cha juu kilichotegemewa.
Asante sana mkuu, hata hiyo dhana kuwa umeme wa maji ni nafuu sio kweli, maana kabla ya umeme huu wa gas na mafuta mazito, tulikuwa tunatumia umeme wa maji. Mbona bado katika nchi za Afrika mashariki umeme kwetu ulikuwa ghali? Kwa sasa kwenye umeme huu wa maji hakuna mwenye uhakika kuwa ni fedha za ndani, kama hata fedha za ujenzi hakuna mwenye uhakika kuwa ni fedha za ndani, kuna uhakika gani kuwa umeme huo wa maji utakuwa bei nafuu?
Sina tatizo na maelezo yako mazuri, ila wakati tunaambiwa umeme wa gas ndio sahihi maana hiyo gas tutaitumia zaidi ya miaka 50, huyu anayetekeleza umeme wa maji alikuwa waziri kwenye serikali hiyo hiyo, mbona hakupinga? Wakati ule Utetezi wa umeme wa maji dhidi ya gas, tuliambiwa matatizo ni mabadiliko ya tabia nchi. Je baada ya utawala kubadili hayo mabadiliko ya tabia nchi yameboreka? Kama mtu aliweza kukalia kimya upotoshaji ule, unaweza kumuamini vipi sasa kwenye hili?
JPM ni mwanasayansi mzuri sana, je uanasayansi wake ulianza baada ya mkataba wa umeme wa gas? Mbona hakuyajadili hayo huko nyuma kwenye vikao vya gas? Sisi hatupingi lolote, bali hatukubali lolote bila maelezo ya kina, tumeshaumwa na nyoka. Hatuna imani na Magu wala chochote cha kwake, angekuwa mtu muadilifu angejitenga na huo wizi wa kwenye gas. Toka amaeingia madaraka hakuna uchaguzi wowote umefanyika kwa uadilifu, kama mtu anaweza kuchezea uchaguzi wa nchi, uadilifu anautoa wapi?
Mkuu swala la uchaguzi tuliache kwanza tutalileta baadae. Kama ulisikia hotuba ya JPM Dodoma 2015 baada ya kuapishwa utaelewa maana yake ya kukaa kimya. JPM alikuwa anayajua maovu yooooote na madili yoote hadi kwenye hotuba yake alisema watu walikuwa wanafungulia mabwawa ya maji kusababisha mgao wa umeme. Ila Kama Waziri wa ujenzi angebadili nini!?, Wengi wanakurupukaga kwa kuhama chama kumbe ndo wanapotea. Vita inapiganwa humohumo. We unaamini mapapa ya nchi hii yasiyogusika kipindi kile akina Kinana,Makamba,Seth, Rugemalila, Manji,Mengi, Patel nk yangenywea!???... Unajua jinsi gani yalishikilia wizara zote na uchumi wa nchi?.. turudi kwenye mada. Angemkemea JK kuhusu gesi nini kingetokea!??.. Je angekuwa bado ana chance ya kurekebisha aliyorekebisha awamu hii au angeishia kuondolewa kwenye uwaziri na kubaki huko chini wizarani,na pengine Membe au Makamba akawa Raisi 2015, tembo zikaendelea kulia,mateja yakaongezeka hadi watoto wa sekondari. Hebu ruhusu kufikiri nje ya fikra zako za kipinzani mkuu..
Hutakiwi usome post zangu maana utaugua wendawazimu. Post zangu ni pasua kichwa, nakushauri achana nazo kabisa. Naona uko na id zako mbili, ile ya tatu mpya nayo umeamua kuikaushia?

Uko sahihi sana na hoja yako naiona katika uwanda mpana sana. Sasa tuje kwenye uhalisia, je unataka kusema hakuna uwezo wa kuhoji ama kuzuia uovu wowote bila kuwa rais? Je ingetokea asiwe rais, tungeendelea kupigwa kwa muda gani? Wtf na yeye anatupiga sasa, lakini watu wanamkalia kimya kisa ni rais? Huo mfano wangu wa uchaguzi nimeutoa kwasababu kinachofanyika sasa ni kwasababu rais anaweza kufanya lolote, kama hilo kundi lililotupiga bila kufanywa lolote, kwakuwa lilikuwa na kinga ya rais mpigaji.
Hakuna mtu muadilifu kisha akawa hataki uwazi, ukiona mtu hataki uwazi, inabidi ujitoe ufahamu kumuamini. Katiba ni kipimo cha kiongozi muadilifu, je yeye anakubali kufanya kazi kwa katiba ya wananchi, ni wazi hayuko tayari, mtu wa aina hiyo unaweza kuweka imani yako kwake vipi? Au hapa unaleta mambo ya muwamba ngozi?

Kwa vile hii ni mada technical, yaani ni mada ya kitaalam, naomba kuanza bandiko hili kwa elimu kidogo kwa members wenzangu ambao sio wataalam wa mambo ya power na energy.
Watu wanadhani siasa ni kusimama tuu majukwaani na kupiga domo, issues yoyote yenye impact kubwa kwa taifa ni siasa, hivyo hivyo zozote zinazohusu utilities, maji, umeme, gesi, mafuta, na public transport ni siasa, na kwa nchi zinazotegemea mkate kama chakula kikuu, issue yoyote. ya mkate ni siasa! kuna nchi inayotegemea mkate kama chakula chake kikuu, bei ya mkate ilipanda kwa thumuni tuu!, wananchi waliingia barabarani na serikali ilipinduliwa!. Hivyo issues za Umeme sio habari mchanganyiko ni siasa!
Kwa vile tumeelezwa umeme wa Stigler ukikamilika utatosha na ziada kuuzwa nje!, Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani Desemba 14, 2020 akiwa katika ziara ya kukagua ujenzi wa Mradi mkubwa wa kufua umeme wa Megawati 2115 kwa njia ya maji wa Julius Nyerere, amesema inatarajiwa kwa mwaka 2023 mahitaji ya umeme Nchini yakaongezeka kwa zaidi ya mara mbili mpaka kufikia megawati 2,770.
"Leo hii mahitaji kwa siku ni megawati 1,177.20. Kukamilika kwa mradi huu wa Julius Nyerere kutaongeza megawati 3,973 ambazo zitatumika katika shuguli za maendeleo ya kiuchumi na kijamii hivyo tunahitaji umeme wa kutosha, utakaobaki tutawauzia majirani zetu" amesema Dkt. Kalemani.
Leo asubuhi, nimesoma mahali kuwa Tanesco imesaini mikataba mipya 6 ya PPA (Power Purchase Agreements) koka kwa wazalishaji binafsi IPPs (Independent Power Producers ) wapya 6, ili kununua megawati 19.16 na kuziingiza kwenye gridi ya taifa, ndani ya miezi 18 ijayo, Jee huu sio aina mpya ya ufisadi mpya wa kisasa kama ulivyokuwa ufisadi wa Richmond, Dowans na IPTL?!.
By Inès Magoum - Published on December 14 2020 / Modified on December 14 2020
Six Independent Power Producers (IPPs) have just concluded power purchase agreements with the Tanzania Electric Supply Company (TANESCO). These private companies are developing renewable energy projects in Tanzania with a total capacity of 19.16 MW.
The state-owned Tanzania Electric Supply Company (TANESCO) is signing power purchase agreements (PPAs) with six independent power producers (IPPs) that are developing several renewable energy projects in Tanzania. TANESCO agrees to purchase 19.16 MW of electricity, under the supervision of the Energy and Water Regulatory Authority (EWURA) of Tanzania.
Among the selected IPPs is Nishati Lutheran Investment, which is implementing a 36-kW hydropower project at the Ijangala Falls in Makete. Similarly, Madope Hydro is implementing the 1.7 MW Madope Hydroelectric Project on the Madope River. Luponde Hydro is also signing a PPA with Tanesco for its Luponde hydroelectric project (9 kW) on the Luhololo River in Njombe. Lung’ali Natural Resources, which is implementing the Maguta hydroelectric project (1.2 MW) on the Lukosi River Falls in Kilolo, will sell its production to the utility.
Commercial operation in 18 months
The other IPP selected is NextGen Solawazi which is working on a 5 MW hydropower project in the Kigoma Special Economic Zone. SSI Energy Tanzania, which is currently building a 10 MWp solar power plant in Kahama, will also sell its production to Tanesco. According to the public company, the six private companies will have to start marketing their production within 18 months.
In the meantime, TANESCO is developing other electricity projects in Tanzania. In this way, TANESCO is supporting the Tanzanian government’s policy of achieving a 75% electrification rate by 2035. Among its projects is the construction of the Rumakali and Ruhudji hydroelectric power plants which will have capacities of 222 MW and 358 MW respectively. In July 2020, TANESCO selected Multiconsult Norge AS, a Norwegian engineering consulting firm, to provide consulting services for the two projects.
My Take:
Japo mimi ni mwandishi wa habari, na sasa nimeisha staafu rasmi, lakini kwa vile kazi ya uandishi iko kwenye damu, hivyo ikitokea habari inahitaji ufuatiliaji, mimi nitaiweka tuu humu jf, wahariri watakao iona it's newsworthy, watatuma waandishi wao kuifuatilia, au waandishi watakaona ni habari, wataifuatilia, mimi nitakuwa nimetimiza wajibu wangu kwa jamii, ila ikitokea kweli ukawa ni ufisadi mwingine, utakuja kujulikana mwaka 2025 kabla ya uchaguzi ujao, nitakachokifanya ni kuwakumbusha tuu kuwa tulinusa, tukasikia harufu, tukauliza, na hayo ndio matokeo, ila pia, sio kila unaposikia harufu ya ufisadi ni ufisadi, harufu nyingine ni harufu tuu na hakuna ufisadi wowote, vitu vingine ni ukosefu tuu wa transparency, kama zile Bilioni 1.5 kwenye ripoti fulani ya CAG, watu wakadhani ni ufisadi, ikaja kukutikana hakuna ufisadi wowote.
Maswali ni haya.
Kwanza maendeleo yoyote ya ujenzi wa mioundo mbinu wa umeme wa maji, ni maendeleo, endelevu, hivyo wakati Watanzania tukiusubiri huu umeme wa Stigler kuingizwa kwenye gridi ya Taifa, hakuna ubaya kwa Tanesco kuendelea kununua umeme toka kwa wazalishaji binafsi waliopo, kwa vile kuna wazalishaji wengi na mikataba imesimamishwa, kwa nini Tanesco wasiendelee nao na badala yake wanasani mikataba na wazalishaji wapya?. What is so special na hawa wapya, wakati wa zamani wapo, mikataba imesitishwa na wengine wametushitaki kwa kuvunja mikataba yao?
Kama umeme wa Stigler, unatosha, hizi PPA's 6 mpya zinazosainiwa sasa ni za nini?.
Kule nyuma tulivunja mkataba wa Dowans kwa tuhuma za ufisadi wa kulipishwa capacity charge kubwa na Tanesco kununua umeme wa bei juu toka kwa hawa IPPs na kuuza kwa bei ya chini!, Jee this time kwenye hii mikataba mipya jee Tanesco wananunua kwa bei gani per unit na kuuza kwa bei gani, tusije kuwa tunatwanga maji kwenye kinu?
Baada ya kuvunjwa kwa mkataba wa Dowans, tulishitakiwa, tukashindwa kesi, tukadaiwa fidia iliyotwa Tozo ya Dowans, waheshimiwa wetu kule Bunge, wakajiapisha kwa maneno kama "over my dead body!" hatulipi! did you know what happened?....we paid every single cent kimya kimya na umeme ukapandishwa bei, Watanzania wote kwa ujumla wetu, tukafidia. Kitu cha ajabu sana katika hili, kampuni ile ile ya Dowans tuliovunja nayo mkataba, ikajibadili jina kujiita Simbion, mitambo ile ile, capacity charge ile ile, na mkataba ule ule, ikaingia tena mkataba na Tanesco, na tukakawa tunawalipa hadi JPM alipoingia, akaukataa ujinga huu, ndipo mkataba wa Simbion ukasitishwa na mpaka sasa kesi iko mahakamani, sijui tumefikia wapi! Kawa haya ndio mambo ya Tanesco na hizi PPA's zake, vipi hizi PPA's sita mpya are they clean?, transparent?.
Kuna wakati kule nyuma, Tanesco ilikuwa inaelemewa na madeni ya umeme wa hawa PPA's na situation ya Tanesco kwa sasa ikoje hadi kuendelea kununua umeme kwa hawa wazalishaji binafsi, ili Tanesco ipate faida ni lazima inunue kwa bei ya jini na kuuza kwa bei ya juu, sasa kama Tanesco haina uwezo wa kuzalisha umeme wa kutosha, kwa nini hao wazalishaji binafsi wasiruhusiwe kuuza umeme wao direct kwa watumia kwa bei ya chini, wananchi ndio wafaidike?.
Japo tunaelezwa Stigler ikikamilika Tanzania tutakuwa na umeme wa kutosha na ziada kuuza nje. Hawa jamaa wanasema "In the meantime, TANESCO is developing other electricity projects in Tanzania. In this way, TANESCO is supporting the Tanzanian government’s policy of achieving a 75% electrification rate by 2035", wakimaanisha huo mwaka 2035, Tanzania ndio tutafikisha 75% ya mahitaji yetu ya umeme!, sasa nani anasema kweli?, jee ni kweli tutajitosheleza na ziada kuuza nje, au tutajitosheleza kwa mahitaji ya sasa kwasabu bado hajaweza ku electrify nchi nzima, hivyo hiyo ziada tutakayouza nje, tutauza huku baadhi ya vijiji vyetu havina umeme kwasababu hatuna miondombinu ya kutosha ku i electrify nchi nzima?. Which is which?.
Wanabodi, Mimi ni mdau mkubwa wa maonyesho ya Saba Saba, kwenye Saba Saba ya Mwaka huu, nimetembelea Banda la Wakala wa Nishati Vijijini, REA kwenye maonyesho hayo, nikazungumza Mwenyekiti wa Bodi ya REA, Mkurugenzi Mtendaji, Wajumbe wa Bodi, Menejimenti na wadau wa REA kuhusu kinachofanywa na...
www.jamiiforums.com
Paskali
Update
Habari yenyewe
TANESCO yasaini mkataba wa kununua umeme kwa wazalishaji wadogo
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limeingia mkataba wa kununua umeme kutoka kwa wazalishaji wadogo wa kampuni sita binafsi, utakaoingia moja kwa moja kwenye kwenye gridi ya Taifa na kutumika katika maeneo mbalimbali Nchini.
Akizungumza katika hafla fupi ya kusaini mikataba kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Meneja Mwandamizi Uwekezaji, Mhandisi Costa Rubagumya alisema wawekezaji hao wamekidhi vigezo kwa mujibu wa kanuni zilizoidhinishwa na EWURA.
"Kwa mujibu wa kanuni zinazosimamia uendelezaji wa miradi midogo ya kuzalisha umeme, inaitaka TANESCO kuingia mikataba na wazalishaji umeme wadogo kwenye maeneo ambayo gridi ya Taifa bado haijafika", alisema Mhandisi Rubagumya.
Aliainisha vigezo vingine ni maeneo ambayo yanatatizo la umeme mdogo ili kuimarisha ubora wa umeme na kigezo kingine ni maeneo ya usambazaji umeme ambapo njia za umeme za TANESCO ni ndefu hivyo kusababisha upotevu wa umeme.
Mhandisi Costa alizitaja kampuni hizo kuwa ni, Kahama Solar Power Project MW 10.0, Kigoma Solar Power MW 5.0, Nishati Lutheran (DKK) Investment Ltd MW 0.36.
Makampuni mengine ni, Madope Hydropower MW 1.7, Luponde Hydropower MW 0.9 na Maguta Hydropower MW 1.2.
Wakizungumza Kwa niaba ya Wazalishaji wadogo wa umeme, Padre Luciano Mpoma na Nicholas Richardson wameishukuru Serikali kupitia TANESCO kwa kukubali kufanya nao biashara ya umeme.
Waliongeza kuwa safari ilikuwa ni ndefu lakini hatimaye wamekuwa na furaha kwani lengo la Serikali ni kuhakikisha nishati ya umeme inamgusa kila mwananchi.
Makampuni hayo yanatakiwa kuanza kuiuzia TANESCO umeme ndani ya miezi 18 kuanzia leo Disemba 08, 2020.
Hili swala haliitaji hata technical ability kuelewa kwamba kuna ulazima au hakuna ulazima wa Tanesco kuingia huo mkataba.
Kwanza kabisa tukumbuke Nyerere Hydropower inatarajiwa kukamilika 2022 incase of any delay watanzania wanatarajia kunufaika na hizo 2115Mega watss kuanzia mwaka 2022 au 2023 kama itachelewa sana.
Cha kujiuliza wakati tunangoja mradi kukamilika hapa katikati tunaishije???Ndio maana mkataba ukawa 18months tuki expect kabla kufikia 2022 mambo yatakuwa sawa.
Unajua wakati mwingine jamani Tanzania tuwe tunasema UKWELI kwa kuwa UKWELI tu utatuweka huru.
Hivi ni kweli kwamba mradi wa umeme wa Nyerere Hydroelectric utakuwa umekamilika na kuwashwa mwaka 2023? Mimi siyo mwanasayansi, lakini huwa nasoma na kuelewa. Mradi wa Mtera wa HEP ulitumia takribani miaka 7 kukamilika, Na huo haukuwa mradi mkubwa saaaana kama ulivyo wa Nyerere HEP. Je, ni ukweli kufika 2023 Bwana la Maji, litakuwa limekamikika, mitambo ya kufua umeme itakuwa imefungwa, serviceline zitakuwa zimejengwa na umeme utakuwa umewashwa?
My take
Ninaomba watanzania tuache mbwembwe za siasa tuwe realistic katika mipango yetu.
Kwa mantiki hiyo ndiyo maana TANESCO bado inahitaji kununua umeme toka vyanzo vingine kwa kuwa technically wanajua haiwezekani Nyerere HEP project itakamilika ndani ya miaka 4. Kama mradi huu utakamilika na kuanzia kutoa huduma inayokusudiwa tuhesabu miaka 7 hadi 10 (2027 hadi 2030).
Pascal umedadavua vizuri sana kuhusu suala hili. Halihitaji elimu ya ufundi umeme bali logic thinking ya mtu ye yote mwenye akili ya kutosha. Akili ya namna hiyo haipatikani chuoni bali mtu huzaliwa nayo. Tanesco hawataweza kujitokeza humu kutoa a convicing reason kwa hicho walichokifanya; cha kuanza kununua umeme kwa hawa wazalishaji wadogo wadogo kwa bei wanayoijua wao halafu kutuuzia sisi kwa lazima kwa bei wanayopanga wao! Bahati mbaya kwa forum hii ya Jf pekee sidhani kama serikali itaiona na kuipa uzito inayostahili. Ungalimtumia mmoja wapo wa wabunge wetu (chagua mbunge ye yote machachari hasa wa upinzani ikiwezekana) kulifikisha bungeni kuihoji serikali kuhusu jambo hili, ninaamini serikali itavunja mikataba hiyo na baadhi ya watendaji wa Tanesco watatumbuliwa. Halima Mdee ni mmojawapo ya wabunge wangaliofaa kwa kazi kama hiyo.
Ni ukweli ulio wazi kwamba:
1. Kwenye grid yetu ya taifa kwa sasa tuna umeme wa MW 1,650. Matumizi yetu ya sasa ni wastani wa MW 1,100. Kwa hivyo hadi sasa tuna ziada ya MW takribani 550 ambazo ziko iddle kwenye grid yetu ya taifa zikisubiri wawekezaji kwenye viwanda, umeme vijijini na kadhalika. Na hapo Kinyerezi upanuzi unaendelea wa kupata MW 300 zaidi hivi karibuni.
2. Hivyo hizo MW 19 kutoka kwa wazalishaji wadogo wadogo kwenye grid yetu ya taifa hazihitajiki. Tanesco itakuwa inawalipa hao watu mabillioni ya pesa kwa kitu ambacho haikihitaji. Pesa hizo ilitakiwa kuitumia kujenga miundo mbinu ya kusambaza hizo MW 550 ambazo ziko iddle kwenye grid ya taifa. Tanesco inapaswa kupunguza bei yake ya umeme ili iweze kuziuza hizo MW 550 zilizo iddle kwenye grid. Kwa sababu ya bei mbaya ya umeme wa tanesco wengi wetu tulishazima majiko yetu ya umeme yenye oven, grill and 4 plates na badala yake tunatumia mikaa. Hizo bei zao wakizipunguza majiko yetu tutawasha na wao watapata pesa kutoka kwenye huo umeme waliokaa nao iddle.
2. Haihitaji akili ya ziada kujua kuwa hicho walichofanya ni kutengeneza uchochoro wa ufisadi kuturudisha tulikotoka kwa akina iptl, simbion nk.
3. JPM kuwaambia wawa support wazalishaji wadogo haikumaanisha waununue umeme wanaouzalisha. Kuna wazalishaji na wasambazaji wa maji wadogo wadogo, wasambazaji wa cable tv stations etc. Wanatakiwa kuwa supported. Hawa wazalishaji wadogo wa umeme wanatakiwa wausambaze kwa wateja wao moja kwa moja. Mtu unaamua utumie umeme wa tanesco au wa mjasiliamali fulani. Mtu anatakiwa aamue atumie mtandao wa simu wa tigo au vodacom au tccl. Atumie king'amuzi cha azam, tbc au star tv etc Serikali inachopaswa kuwapa wajasiliamali hao ni technical support ie kuwawezesha kiufundi, si kununua bidhaa yao. Serikali jukumu lake ni kuhakikisha hizo bidhaa kutoka kwa wajasiliamali hao zinaviwango unaokubalika na ni salama kwa wateja wao. Serikali kazi yake ni kukusanya kodi stahiliki kutoka kwa wajasiliamali hawa.
4. Wazalishaji hawa wadogo wadogo wamekuwapo miaka mingi tu nawamekuwa na wateja maeneo yao ambayo tanesco ilikuwa haijafika. Kwa mfano katika kijiji changu miaka kama 30 iliyopita jamaa mmoja alikuja na generator kubwa ya umeme kama zile.zinazotumika mahospitalini kama standbye generator ambazo zina uwezo wa kuwasha mashine kubwa kubwa za mahospitali kama za X-ray na CT scans ambazo hutumia umeme mwingi. Jamaa huyu aliifunga generator hiyo kijijini na kuweza kuwasambazia umeme wanakijiji wote kwa sababu matumizi yao ni hasa kwa ajili ya taa tu usiku ambazo hazitumii umeme mwingi. Wanakijiji hao walikuwa wakimlipa kiasi fulani cha pesa kila mwezi ambazonzilimuwezesha kuishi vizuri. Ujio wa umeme wa REA umemuharibia biashara yake kwani umeme wa REA bei yake ni ndogo. Hivyo atafurahi sana kama tanesco watakuwa wanaununua huo umeme wake na kuuuza kupitia grid ya taifa. Kama ni hivyo wote tukubaliwe kuwauzia huu umeme mdogo mdogo ambao tunaweza kuuzalisha majumbani kwetu.
5. Tanesco isitake kuwa a tanzania national electricity purchasing and supplying company. Inakiwa iwe a tanzania national electricity generating and supply company. Sisi ndiyo tutakao purchase huo imeme kutoka kwao au kwa mzalishaji mwingine ye yote tutayeona anatufaa. Tanesco wanapaswa kushindana kibiashara na wazalishaji wengine binafsi wa umeme.
Uko sahihi sana na hoja yako naiona katika uwanda mpana sana. Sasa tuje kwenye uhalisia, je unataka kusema hakuna uwezo wa kuhoji ama kuzuia uovu wowote bila kuwa rais? Je ingetokea asiwe rais, tungeendelea kupigwa kwa muda gani? Wtf na yeye anatupiga sasa, lakini watu wanamkalia kimya kisa ni rais? Huo mfano wangu wa uchaguzi nimeutoa kwasababu kinachofanyika sasa ni kwasababu rais anaweza kufanya lolote, kama hilo kundi lililotupiga bila kufanywa lolote, kwakuwa lilikuwa na kinga ya rais mpigaji.
Hakuna mtu muadilifu kisha akawa hataki uwazi, ukiona mtu hataki uwazi, inabidi ujitoe ufahamu kumuamini. Katiba ni kipimo cha kiongozi muadilifu, je yeye anakubali kufanya kazi kwa katiba ya wananchi, ni wazi hayuko tayari, mtu wa aina hiyo unaweza kuweka imani yako kwake vipi? Au hapa unaleta mambo ya muwamba ngozi?
Mkuu Kuna Mambo mengi sana mmekaririshwa tu, mfano Katiba mpya,sijui tume huru ya uchaguzi,demokrasia etc. Matatizo ya nchi za Africa karibu zote hasa za watu weusi ni yaleyale. Matatizo ya watu weusi waliobakia nje ya Afrika ni yaleyale karibu nchi zote kuanzia USA, Brazil,Papua New Guinea,Jamaica etc. Turudi Afrika mashariki. Mnadai Kenya Wana tume huru na katiba mpya mbona kabla ya uchaguzi uliopita kiongozi wa tume ya uchaguzi aliokotwa kafa na kidole gumba cha kutumika kwenye mfumo wa fingerprint kimekatwa!?.. Africa ni umafia tu. Ndo maana wengine tunaamini kwenye watu sio vyama. Hata uweke katiba ipi,tume ipi, mfumo upi as long as ni hizi nchi zetu za watu weusi kama kiongozi aliyepo sio mkali Mambo ni yaleyale. Mimi hutakaa uniaminishe eti Chadema ikiingia madarakani maisha ya watanzania yatabadilika. NEVER. WHY!??.. Hulka ya wanaoongoza ni ile (Selfish,roho mbaya,njaa,asili ya umaskini,majivuno, ulimbukeni nk) na wanaoongozwa hivyo hivyo(njaa,umaskini, ujinga, kukosa Elimu,kupenda ngono,kuzaana hovyo nk). Hata ije CDM,CUF,ACT,CHAUMA as long as viongozi ni weusi na wanaoongozwa ni weusi NO CHANGES. So, wengine tunamuona angalau JPM ana moyo wa kukemea na kumaanisha. Sasa kumuamini au kutomuamini inabaki kwa mtu binafsi. Kama dini vile.

Nimecheka kwa nguvu huu utetezi wako. Tunataka katiba mpya sio ili cdm iingie madarakani, bali tunataka anayeingia madarakani awe ni yule anayekubalika na wengi. Hatutegemei kupata viongozi malaika, bali tunataka mifumo madhubuti. Kwenye hiyo katiba ya Kenya ni kweli hakuna malaika, ila mifumo yao ina afadhali kuliko hapa kwetu. Sisi wengine sio waumini wa ukali wa mtu, bali uimara wa mifumo na taasisi imara. Magu anakemea kwa double standard, kiasi kwamba inageuka kuwa ni mtu anayeongozwa na chuki binafsi na visasi. Lakini ingekuwa kuna mifumo imara tungeona bunge likifanya kazi yake kwa mujibu wa sheria, na mahakama ingetekeleza wajibu wake, na wala mahakama zisingetumika kama sehemu ya kukomoa watu wasiopendwa na watawala.
Hutakiwi usome post zangu maana utaugua wendawazimu. Post zangu ni pasua kichwa, nakushauri achana nazo kabisa. Naona uko na id zako mbili, ile ya tatu mpya nayo umeamua kuikaushia?
Kwa nini unaishi kama mganga wa kienyeji karne hii ya science na teknolojia? Unaishi kwa kubashiri na kupiga ramli? Jikite kwenye mada husika huku ukiweka post zenye mashiko,sio pumba ambazo hazina mbele wala nyuma.
Unajua wakati mwingine jamani Tanzania tuwe tunasema UKWELI kwa kuwa UKWELI tu utatuweka huru.
Hivi ni kweli kwamba mradi wa umeme wa Nyerere Hydroelectric utakuwa umekamilika na kuwashwa mwaka 2023? Mimi siyo mwanasayansi, lakini huwa nasoma na kuelewa. Mradi wa Mtera wa HEP ulitumia takribani miaka 7 kukamilika, Na huo haukuwa mradi mkubwa saaaana kama ulivyo wa Nyerere HEP. Je, ni ukweli kufika 2023 Bwana la Maji, litakuwa limekamikika, mitambo ya kufua umeme itakuwa imefungwa, serviceline zitakuwa zimejengwa na umeme utakuwa umewashwa?
My take
Ninaomba watanzania tuache mbwembwe za siasa tuwe realistic katika mipango yetu.
Kwa mantiki hiyo ndiyo maana TANESCO bado inahitaji kununua umeme toka vyanzo vingine kwa kuwa technically wanajua haiwezekani Nyerere HEP project itakamilika ndani ya miaka 4. Kama mradi huu utakamilika na kuanzia kutoa huduma inayokusudiwa tuhesabu miaka 7 hadi 10 (2027 hadi 2030).
Kijana tuliza munkari na utafakari kabla ya kuchambua mambo, nini kinachokufanya uproject kuwa huu mradi wa JNHEP utachelewa kuisha? Wakati Mtera inajengwa, je tulikuwa na utashi wa kisiasa kama leo hii? Maana kama tunge kuwa na good political will toka mwazo huu mradi ungekamilika hata miaka 30 iliyopita.
Usituletee mifano ya kitoto wakati sisi ni watu wazima. Kujenga Hdro plant hakuna complication kama unavyodhania, zaidi ya kutengeneza tunnels za kupitishia maji kuyachepusha, kutengeneza bwawa na kusimika power house. Jambo ambalo mpaka sasa linaenda vizuri maana wameshaanza harakati za kuchepusha maji kutengeneza bwawa.
Lakini ninachotaka kukuambia ni kuwa utashi wa kisiasa na kuwa na viongozi makini wanaosimamia mapato ya taifa ndio suruhu ya kukamilisha miradi kama hii, na hili linawezekana. Kwa hiyo usiseme huu mradi hauwezi kukamilika ndani ya wakati.
Mkuu nisamehe kwa kuchelewa kukujibu majukumu mengi. Tukirudi kwenye swali lako ni kwamba kipindi cha nyuma ishu nyingi zilikuwa zinaanzishwa ili watu wapige pesa, mfano mzuri benki ya Standard Chartered HongKong imetumiwa Sana kutukopesha ili watu wapige pesa bila kujali huko mbele itakuwaje, na waliweka mikataba tata sana ambayo kuivunja ni ngumu. Sababu ya pili umeme wa gesi una limit. Gesi inaisha ardhini na ina mwisho wake kabisa. Kadiri unavyoitumia ndo inavyopungua ardhini. Ni Kama mtungi wa Kg45 jikoni kwako inavyopungua kadri unavyoitumia,sema huko ardhini ni Kama mtungi mkubwa sana, so ukiwekeza $bil.6.5 huna uhakika Kama zitarudi gesi haijaisha ardhini. Gesi ni natural reserve ambayo composition yake inachukua muda mrefu sana. Lakini Stigler Gorge inategemea maji kwa 95% au zaidi na ukifatilia umeme wa maji bado ni wa uhakika Sana tofauti na gesi. JPM ni mwanasayansi mzuri sana na anayajua haya yote na wameshayajadili, tatizo wengi humu wamekaa mkao wa kupinga lolote atakalofanya. Sijui Kama nimeeleweka vizuri mkuu.
Aisee, kweli mmekunywa yamini ya kupinga!!!!
====
Hata hivyo, tupe sababu za nguvu ya uzalishaji wa umeme kwa njia ya maji upungua kama ukarabati wenye mpagilio na ulinzi wa chanzo cha maji hayo vikifanyika?
1. Kwenye grid yetu ya taifa kwa sasa tuna umeme wa MW 1,650. Matumizi yetu ya sasa ni wastani wa MW 1,100. Kwa hivyo hadi sasa tuna ziada ya MW takribani 550 ambazo ziko iddle kwenye grid yetu ya taifa zikisubiri wawekezaji kwenye viwanda, umeme vijijini na kadhalika. Na hapo Kinyerezi upanuzi unaendelea wa kupata MW 300 zaidi hivi karibuni.
Tutofautishe installed/capacity au generated energy capacity na delivered energy capacity. Umeme unaozalishwa siyo wote unamfikia mlaji/mteja. Lazima ujue kuna capacity factor ina husika hapo. Yaani capacity factor ni uwiano wa matumizi na uzalishaji wa umeme kwa muda maalumu waweza kuwa kwa mwezi ama mwaka. Vyanzo/miradi ya umeme ina capacity factor tofauti. Umeme wa Maji ukiwa na capacity factor ya juu.
Tatizo la P siku hizi ni kukosa msimamo!! (Unafiki) tulishasema ccm ni majizi!! yeye akaanza kutetea!! leo amekosa teuzi. amekuja na mada ya umeme!! anaweza kuwa sahihi!! lakini watu hawatamuamini tokokana na tabia yake ya kukosa msimamo!!
Ya Kigoma ipo solar panel ipo karibu na airport ni mradi wa mzungu mtanzania ununuzi wa umeme huu utakuwa faraja kwa watu wa kigoma baada ya kutumia umeme wa majenereta
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.