Siasa za visasi: Rwanda yapandisha ushuru kwa magari ya mizigo yanayotokea Tanzania

Status
Not open for further replies.
Wana Jamiii

Nipo hapa Rusumo mpakani mwa Tanzania na Rwanda.....siamini ninachokiona machoni mwangu....kuanzia jana tarehe 1/09/2013 serekali ya Rwanda imeongeza ushuru wa barabara ( ROAD TOLL) kwa magari yote ya Mizigo ( Fuel and Dry Cargo) yenye plate numbers za Tanzania kutoka USD 152 mpaka USD 500 kwa kila gari.

Kwa taarifa ambazo sio rasmi kwa siku magari ya mizigo takribani 300 yanavuka hapa mpakani, na zaidi ya asilimia 95% ya magari hayo zina plate numbers za Tanzania.

Wanajamii hii ina madhara gani kwa uchumi wa Tanzania kwani akili ya harakaharaka hii ni some sort of Protectionism ila kwa mbali inaweza ikawa ni muendelezo wa chokochoko.

Hapo maana yake ni kwamba hataki magari ya Tanzania yaende Rwanda. Magari ya Kenya kupitia Uganda yatachukua nafasi. mambo ndio yanaanza kidogo kidogo. Acha waende zao Kenya ili tupate akili ya kuendeleza reli ya kati. mengi ya magari hayo ni wakubwa wenyewe na hilo Kagame analijua.
 
Wana Jamiii

Nipo hapa Rusumo mpakani mwa Tanzania na Rwanda.....siamini ninachokiona machoni mwangu....kuanzia jana tarehe 1/09/2013 serekali ya Rwanda imeongeza ushuru wa barabara ( ROAD TOLL) kwa magari yote ya Mizigo ( Fuel and Dry Cargo) yenye plate numbers za Tanzania kutoka USD 152 mpaka USD 500 kwa kila gari.

Kwa taarifa ambazo sio rasmi kwa siku magari ya mizigo takribani 300 yanavuka hapa mpakani, na zaidi ya asilimia 95% ya magari hayo zina plate numbers za Tanzania.

Wanajamii hii ina madhara gani kwa uchumi wa Tanzania kwani akili ya harakaharaka hii ni some sort of Protectionism ila kwa mbali inaweza ikawa ni muendelezo wa chokochoko.

Umejiunga leo leo JF halafu unakuja na kigongo namna hii? Ngoja wanaojua waingie humu watupatie taarifa za uhakika.
 
Hivi Rwanda inaingiza mizigo kiasi gani hadi iwe ishu kale ni kanchi sawa na zanzibar tu
 
RAISI WETU MPENDWA Dr. JAKAYA MRISHO KIKWETE TUKO NAWE RAISI WETU.

TUPE RUKSA TUPIGE HADI KIGALI NA KUCHUKUA NCHI YETU YA RWANDA. RWANDA IMEINGILIWA NA CHAWA NA KUNGUNI ANAYEJIITA KAGAME.

TUSIISHIE MPAKANI NA KONGO TU, BALI PIGA HATA CHUMBANI KWAKE HADI AKIMBIE KUJIFICHA HUKO KAMPALA, NA HUKO TUTAMPATA TU KUNGUNI HUYO KAGAME.
 
akili nyingi hupunguzamaarifa, naona jamaa PK katika mipango ya kulazimisha kete ya mombasa anajikaanga kwa mafuta yake mwenyewe, na tusubiri kuona mwisho wa hili..
 
Hii sasa noma... dola 500 per day * 300 trucks = dola 150,000... Ina maana kwa wastani kwa mwezi, kama hali ikiendelea hivi, wanaweza ku-make around 4mil dolla.... Kazi ipo...
 
kikwete alivyokua anaongea dharau mlichekelea.
mnazani vita ni kushikiana mtutu pekee???

mkuu, hapa hakuna cha vita wala nini isipokuwa Kagame anajiongezea idadi ya maadui
 
Rwanda ikiwa ni nchi huru inayoendeshwa kwa mujibu wa katiba ina haki ya kufanya maamuzi bila idhini ya nchi nyingine yoyote. Ninavyomuelewa Rais Kagame ni mtu makini sana kwenye utawala wake. Hataki masihara hasa kwenye masuala ya utawala bora. Huo uamuzi ni haki yao kwa sababu zao kwa nchi yao. Msitake kumpangia Rais wa nchi nyingine vigezo ili tu kuwafurahisha ninyi/sisi. Wao watakuwa wamepanau na kupima ni athari gani chanya na hasi za kuweka hiyo kodi. Kwanza hao wamiliki wa hayo malori hapa kwetu ndio watuhumiwa wakubwa wa kuzorotesha kufufuliwa na kuendelezwa kwa reli hapa kwetu.

Cha kushangaza kuna watu mnawakingia kifua. Kama mna uchungu sana na uchumi wa nchi hii basi kemeeni na hiyo alleged sabotage on the railroad company. Siungi mkono kuongezwa kwa ushuru selectively like that (as a man who believes in capitalism I hold strong reservations over selective taxation) but I respect Rwanda's sovereign right to determine their own tax structure.
 
Ndugu mzigo wa RW na UG unaopitia Dar port hata kabala ya ugomvi na mkakati wa KKK ni less than 2% ya overall transit cargo!
 
Taarifa yako haijakamilika. Haujasema kuwa magari ya rwanda yanayoingia tanzania yamekuwa yakitozwa hiyo dola 500 for many years. Wamejaribu ku plead serikali yenu ipunguze ili hiyo gharama iendane na za nchi nyingine wanachama wa East Africa. Tanzania walikuwa wanajishebedua.

Mkuu weka tofauti kando kaka, Hii ni business usifanye mchezo. Mwanzoni walikuwa wakitoza 150 USD per truck sasa wameongeza mpaka 500USD kwa magari ya TZ pekee, Ya nchi zingine wanachaji hiyohiyo 150usd. Sasa inaonekana hujui hali ipoje kaka.

Ngoja nikuitie jamaa zangu kwa majibu zaidi Ritz ZeMarcopolo chama R.B etc
 
Last edited by a moderator:
Kagame amepandwa na msongo wa mawazo baada ya kukatwa mirija yake kule Kongo,

Ataliangamiza taifa lake tukisema tujibu wito wa jihadi na krusaidi dhidi yake
 
Mkuu usiwe na shaka, hizo ni hasira za mkizi tuu. PK anawatwisha mzigo wananchi wake, huo ni uamzi wa kisiasa zaidi sio technical. Nimesikiliza Times FM, Kwamba magari ya nchi zingine ushuru haujapanda ila ya TZ umepanda 3 times.

Rule of the game lazima itaaply tuu na hapo ndoo PK atakubali.(kama wewe ni mfanya biashara hope unaelewa ninaposema RULE OF THE GAME). Hilo ongezeko effect zake ataziona mda si mrefu sana.

cc ZeMarcopolo

Kwa hili haongezi gharama kwa watu wake ila faida kwa mwenye gari inapungua au inaondoka kabisa. Lengo lake ni kulazimisha waagizaji mizigo watumie bandari ya Mombasa badala ya Dar es Salaam. Watapata msukosuko kwa muda tu then wakianza kupitia Mombasa mambo yatatulia.

Ina maana gani kwetu? Tuboreshe reli ya kati. Hao wenye malori ndio walikuwa wanahujumu reli ya kati isifanye kazi au isiboreshwe. Tena wengi wao ni wakubwa haohao.
 
Uliona wapi chura kuwa na hasira kuwa ng'ombe asinywe maji! sana sana asipojificha mbali anakanyagiwa mbali, na maji yatanywewa bila shida!
 
akili nyingi hupunguzamaarifa, naona jamaa PK katika mipango ya kulazimisha kete ya mombasa anajikaanga kwa mafuta yake mwenyewe, na tusubiri kuona mwisho wa hili..

Mkuu, mwisho wa siku ni kuwakaanga wananchi wake. wafanyabiashara hawawezi kushindwa kulipa hiyo dola 500 isipokuwa lazima watafute pa kufidia kiasi hicho
 
Rwanda ikiwa ni nchi huru inayoendeshwa kwa mujibu wa katiba ina haki ya kufanya maamuzi bila idhini ya nchi nyingine yoyote. Ninavyomuelewa Rais Kagame ni mtu makini sana kwenye utawala wake. Hataki masihara hasa kwenye masuala ya utawala bora. Huo uamuzi ni haki yao kwa sababu zao kwa nchi yao. Msitake kumpangia Rais wa nchi nyingine vigezo ili tu kuwafurahisha ninyi/sisi. Wao watakuwa wamepanau na kupima ni athari gani chanya na hasi za kuweka hiyo kodi. Kwanza hao wamiliki wa hayo malori hapa kwetu ndio watuhumiwa wakubwa wa kuzorotesha kufufuliwa na kuendelezwa kwa reli hapa kwetu.

Cha kushangaza kuna watu mnawakingia kifua. Kama mna uchungu sana na uchumi wa nchi hii basi kemeeni na hiyo alleged sabotage on the railroad company. Siungi mkono kuongezwa kwa ushuru selectively like that (as a man who believes in capitalism I hold strong reservations over selective taxation) but I respect Rwanda's sovereign right to determine their own tax structure.

Mkuu, nakushukuru sana hapo kwenye RED. Nimepiga sana kelele kuhusu hilo hata kabla ya ugomvi kati ya JK na PK. labda hii itakuwa " a blessing in disguise" Hao wakubwa ndio wenye malori hayo jamani. Kuna wakati bwana mkubwa aliingiza malori 50 na hakulipa ushuru. Mbona yatafumuka mengi.
 
kwa hili haongezi gharama kwa watu wake ila faida kwa mwenye gari inapungua au inaondoka kabisa. Lengo lake ni kulazimisha waagizaji mizigo watumie bandari ya mombasa badala ya dar es salaam. Watapata msukosuko kwa muda tu then wakianza kupitia mombasa mambo yatatulia.

Ina maana gani kwetu? Tuboreshe reli ya kati. Hao wenye malori ndio walikuwa wanahujumu reli ya kati isifanye kazi au isiboreshwe. Tena wengi wao ni wakubwa haohao.

hili la reli nakubaliana na wewe, sijui ni mizigo mingi kiasi gani ilikuwa inapita hapa kwetu na ina tija kiasi gani cha kufanya watu wahamaki na hako kanchi kasikoenea hata kwenye kiganja cha mkono.
 
Kwa hili haongezi gharama kwa watu wake ila faida kwa mwenye gari inapungua au inaondoka kabisa. Lengo lake ni kulazimisha waagizaji mizigo watumie bandari ya Mombasa badala ya Dar es Salaam. Watapata msukosuko kwa muda tu then wakianza kupitia Mombasa mambo yatatulia.

Ina maana gani kwetu? Tuboreshe reli ya kati. Hao wenye malori ndio walikuwa wanahujumu reli ya kati isifanye kazi au isiboreshwe. Tena wengi wao ni wakubwa haohao.

Haya kaka, kwa upande wetu hapa TZ kitu tulichokosea ni hao wasimamizi kuwa wamiliki wa bandari kavu, haohao ndo wanamakampuni ya usafirishaji. But tusilaumu sana hali ishatokea sasa hivi ni kujipanga tuu hali itarudi kama mwanzo na mombasa port tutabit tuu endapo seriousness itakuwepo kwa watendaji.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom