Sibonike
JF-Expert Member
- Dec 23, 2010
- 17,296
- 18,027
Wana Jamiii
Nipo hapa Rusumo mpakani mwa Tanzania na Rwanda.....siamini ninachokiona machoni mwangu....kuanzia jana tarehe 1/09/2013 serekali ya Rwanda imeongeza ushuru wa barabara ( ROAD TOLL) kwa magari yote ya Mizigo ( Fuel and Dry Cargo) yenye plate numbers za Tanzania kutoka USD 152 mpaka USD 500 kwa kila gari.
Kwa taarifa ambazo sio rasmi kwa siku magari ya mizigo takribani 300 yanavuka hapa mpakani, na zaidi ya asilimia 95% ya magari hayo zina plate numbers za Tanzania.
Wanajamii hii ina madhara gani kwa uchumi wa Tanzania kwani akili ya harakaharaka hii ni some sort of Protectionism ila kwa mbali inaweza ikawa ni muendelezo wa chokochoko.
Hapo maana yake ni kwamba hataki magari ya Tanzania yaende Rwanda. Magari ya Kenya kupitia Uganda yatachukua nafasi. mambo ndio yanaanza kidogo kidogo. Acha waende zao Kenya ili tupate akili ya kuendeleza reli ya kati. mengi ya magari hayo ni wakubwa wenyewe na hilo Kagame analijua.