Zanzibar 2020 Siasa za Zanzibar: Hongera Dr. Mwinyi Kwa Ushindi wa Kishindo, Maalim Makamo wa I, Mteue Balozi Amina Salum Ally Awe Makamo wa II, Utoe Sare Sare Maua

Mkuu Gavana,
Kwa faida ya wasiojua, wenyeji haswa wa asili ya Zanzibar ni Wabantu, Wakwezi na Wahadimu, Mtawala wa asili aliitwa Mwinyi Mkuu.

Mwinyi Mkuu akaomba msaada kwa Waarabu kumpiga Mreno, akamgeukia Mwinyi Mkuu, alichomfanya, hakuna ajuaye, bali mara ghafla Mwaka 1832, Sultan Seyyid Said akahamishia Sultanate yake toka Oman na kuihamishia Zanzibar, na kuvitwaa visiwa hivyo kama mali yake as if havina mwenyewe, mpaka ile January 12, 1964, wenyewe wenye Zanzibar yao, wakamfurusha kwenye yale Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Kipindi Sultan akitawala Zanzibar, hiki ndicho kilichofanyika, Angalizo: Kama una roho ndogo, naomba usifungue hii link, itakutoa machozi!

Ukiangalia Waarabu walivyotufanya, ndio utaelewa kwanini jamaa fulani huwa anashinda lakini hatangazwi na hapewi!.

P
 
Reactions: Ole

Wewe unasoma historia aliyokuandikia Nyerere, sisi tumeishi kwenye hiyo serikali mnayoiita ya ya mwarabu

Nilikuuliza maswali na hujajibu hata moja
Mwarabu aliivamia Zanzibar kijeshi kama Tanganyika akaweka jeshi la waarabu?
Mwarabu yupi alimpiga risasi mzanzibari japo mmoja?
Mwarabu yupi alichukuwa mali ya mzanzibari?
Lete jina la mzanzibari mmoja aliyewekwa jela na mwarabu kwa kesi ya kubambikizwa na mwarabu?
Lete ushahidi wa mwarabu wa kuvikalia kwa nguvu hivi visiwa. Na wapi huyo mwinyi mkuu au watu wake walijaribu kumpiga vita mwarabu au watu kufanya uasi au kumpinga kama tunavyoipinga Tanganyika kwa uvamizi wake leo?
 
Kama mwarabu lisu na lowasa ?
 
PASCAL
suala la GNU baina ya CCM na ACT wazalendo HALIPO
Maridhiano zanzibar SASA yanahitaji ujasiri mkubwa na kuangalia mbali sana.
Tumefika pahali wale wanotaka mabadiliko znz washaamini kuwa hawawezi kuyapata kwa njia za democracy .
Kama unaweza kushauri
1.Wambie wenye power waitishe kura ya maoni juu ya muungano.
2.kama hilo gumu kumeza warejeshe rasimu ya warioba at least.
Masuala ya usalama wa tanganyika
Nafasi ya TEC znz
Udugu baina ya watu wa mbande mbili na mengine mengiii Yanazungumzika
 
First thing first, kama tunakubaliana Wenyeji wa asili Zanzibar ni Wabantu kina Mwinyi Mkuu, na Mwarabu ni mtu wa kuja kutoka Oman, hebu tueleze aliweza vipi kuimiliki Zanzibar kuifanya mali yake?. Hata Mjerumani, kina Karl Peters waliandikiana mikataba na kina Chifu Mangungo wa Msovero, Sultan yeye visiwa vile aliviokota tuu kama kuokota Dodo chini ya muembe?.
Tuanzie hapa, halafu nitakupeleka mdogo mdogo hadi tutafika.
P
 
Reactions: Ole
As long as Zanzibar sio nchi, bali ni sehemu ya JMT, then usalama wa Zanzibar pia ni suala la muungano. Kama kuna mazungumzo yoyote then ni baada ya 2025!.
P
 
Nani alikuambia wabantu ni wenyeji wa zanzibar?

Wabantu ni nyinyi wenye tabia hizi chafu kutokufuata sheria zenu wenyewe, kuuwa ovyo ,na sijui kitu gani kinawapelekea kuzivamia nchi za wenzenu?
 
https://www.facebook.com/
 
Maalim hawezi kupewa cheo chochote kile. Huyu mzee ni fedhuli sana aende akakae na familia yake huko alikowaficha. Nchi haiwezi kumzawadia mtu ambaye amesababisha raia wengi kupoteza maisha yao kwa sababu ya tamaa zake binafsi.
 
Maalim hawezi kupewa cheo chochote kile. Huyu mzee ni fedhuli sana aende akakae na familia yake huko alikowaficha. Nchi haiwezi kumzawadia mtu ambaye amesababisha raia wengi kupoteza maisha yao kwa sababu ya tamaa zake binafsi.
Ndivyo katiba ilivyoandikwa hivyo ?na sheria za uchaguzi ndivyo zinavyosema hivyo?

Haovibaraka wenu ndio wanaozidi kuifisidi nchi. Mliachiwa nyinyii miaka 5 ,kipi mlichokifanyia nchi zaidi ya kuzidi kuirudisha nyuma miaka 200 kabla hata kuja hao mnaowaita waarabu. Umasikini umekithiri hasa kwa hao CCM ,kazi kuomba omba ovyo kwa njaa
 
Maoni hayapigwi rungu. Mimi nimetoa maoni yangu kuhusu kichwa cha habari. Katiba na sheria unasema wewe.
Kwani mimi nimekupiga rungu au nimekuuliza maswali?
Sasa jibu maswali au unaweza kwenda kukojoa na kulala
 
Typical JF style. You deserve to be ignored.
Typical Lumumba style. Hao vibaraka wa Tanganyika hawajui isipokuwa wizi, Sif Ali Idd ameiba na kujenga nyumba 37, Ali hassan Mwanyi Kachukuwa mashamba ya watu Kitope, na kule Morogoro kaiba ekari 60 000+
 
Kwani wazungu walitufanyaje ? Au hawakutufanya ? Amani Abeid yule alokuwa rais wa Zanzíbar, unamjua mama yake ? Salim Ahmed Salim nae ? Hao unosema wamejaa kwenye serikali ya mapinduzi.... ccm wapinzani hawawataki ila kusema turudi chama kimoja wanahisi watatengwa na dunia.
Nota Bené..... Hamna ukoloni mzuri hata siku moja ( Samora Machel alipokuwa Harare /Salisbury aliwahi kuisema kauli hii.)
Sultan alokuwa wa Oman ni Sayyid said , waliobakia wanawe hawakuwa Waoman bali waswahili, labda uwe unasema waswahili ni Wabantu watupu.
 
Makamu wa Kwanza wa rais ni pambo tu hana mamlaka wala nguvu yeyote ht akichukua labda km awinde posho n mshahara
 
Hamad hafai kuwa Makamo wa Rais tena; ni mroho wa madaraka sana. Iwapo Makamo wa rais lazima atoke pemva kwenye upinzani basi awe ni mtu tofauti kabisa, siyo Hamad.
 
Mkuu Bayyo , huwezi kuzuia watu kusema, tena kwenye machungu, watu walioumizwa kwa ndani, wakisema ndio wanapunguza machungu, hivyo ni rukhsa kunitumia mimi kupunguzia machungu.
P
Hivi makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar huteuliwa na Rais au ni tako la sheria kwamba aliyeshika nafasi ya pili ndiye makamu wa kwanza?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…