Zanzibar 2020 Siasa za Zanzibar: Hongera Dr. Mwinyi Kwa Ushindi wa Kishindo, Maalim Makamo wa I, Mteue Balozi Amina Salum Ally Awe Makamo wa II, Utoe Sare Sare Maua

Watasema wewe ni kibaraka wa CCM, wana hasira za kugaragazwa kwa Lissu na Mbowe!
Mbona tuliwaonya wakatutukana, lakini tuliyosema yamekuwa; Lissu ameshindwa kufikia kura za Dr Slaa na pia wamepata wabunge less than 10. Chadema wabishi hawataki kujifunza toka kwa legents wa jf
 
Suala la muungano utazeeka na uta r.i..p bila kuguswa kwani linashughulikiwa kistaarabu na kindugu.Punguza mihemuko
 
Maalim Seif hakuna kupokea nafasi yoyote labda upokee wewe na Pascal .
 
Ndugu Pascalli inaonekana unapenda sana kuongelea Zanzibar. Sisi wazanzibari hatumtaki Mwinyi wala CCM. Na kwa mara hii tumeonyesha wazi kuwa zanzibar CCM haipo. Mumetuletea jeshi la Burundi kuja kupinduwa matakwa ya wazanzibari na mumempa Mwinyi 76%. Kwa hizo hesabu zenu munataka serikali ya umoja wa kitaifa na maridhiano. Ni watu wa kushangaza. Mumetuuwa na kutupiga na mapaka dakika hii majeshi wako mitaani wanatupiga. Yote mumefanya halafu munataka nini?.Ni wazi kuwa maisha ya wananchi wetu hamuyathamini. Sisi hatuna haja kukaa mezani na watu wasio na heshima. watu ambao mikono yao imejaa damu za waznzibari. warudisheni viongozi wetu muliowateka na kuwaadhibu. Watoto wetu mumewapiga kwa kuwa wameikataa CCM . Uonevu huu utakwisha lini?.
 
Hivi makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar huteuliwa na Rais au ni tako la sheria kwamba aliyeshika nafasi ya pili ndiye makamu wa kwanza?
Mkuu Manjagata , sheria inasema chama kilichoshika nafasi ya pili, kutatoa makomo wa rais. Hivyo Rais wa Zanzibar anakiandikia ACT, kipendekeze jina la mtu wa kuteuliwa kuwa Makamu, kisha rais Mwinyi anamteua.

Baada ya uteuzi, rais Mwinyi anakaa na makamu wote wawili kupendekeza majina ya watu wa kuteuliwa mawaziri, upinzani wakitoka 6. ACT Wazalendo haina hao watu, hivyo Mwinyi atapewa majina na Maalim Seif, kisha, watateuliwa.
P
 
Mkuu Falconer , kwanza Wanzanzibari poleni sana kwa madhila yaliyowakuta. Vijana wenu wengi wameachiwa jana.

Mwinyi ni muungwana na mstaarabu, mpeni ushirikiano atawaunisha Wazanzibari, atatibu vidonda vya uchaguzi na kuwafuta machozi. Kwa damu zilizomwaika, atatibu tuu makovu kupunguza machungu.

Punguzeni hasira, machungu yatawapoa.
P
 
Nawaomba tu ACT wakubali yaishe ili wakaweke watu wao kule kwenye serikali. Kwa mfano kwenye tume ya uchaguzi lazima wakashinikize kuwe na wateule wanaotoka upinzani. Kama hili CCM watalikataa maanake hiyo siyo serikali ya umoja wa kitaifa!
 
Vyeo huwa havitolewi kama pole au rambirambi ingekuwa hivyo Lisu amgeshinda uraisi kwa kupewa kura za pole kwa kupigwa risasi

Hakuna vyeo vya kumpa Maalim SEIF kama pole
 
Hamna jambo baya kama ulikuwa mtu wa kusimamia haki n ukweli na unaona maovu n kukaa kimya kama hayapo vile ila mungu huwa hamfichi mtu na haki huwa ina chelewa tu ila inafika
 
Amegeuka kuwa wakala wa shetani.
Kwa yaliyofanyika uchaguzi huu , Bora ukae kimya kuliko kuja na mabandiko Kama haya ya Pascal ,huku ukijua ,ukisikia na kuona watuwalivyouawa , jeruhiwa , pigwa hadharani na chama Cha magaidi CCM bill aibu mchana kweupe kisa madaraka ,kila siku huwa nawaambia CCM hawamjui Mungu Wana mungu wso mwenge Nyamrunda , mmeamini sasa kwa waliyoyatenda , mtu mwenye kuabudu Mungu hawezi hata siku moja kufanya walichofanya CCM kwenye uchaguzi huu.
 
Asante, tatizo kubwa kwa ndugu zetu wa CCM , ni kujifanya kama yule ndege anaitwa mbuni. Mbuni akizidiwa hutia kichwa chake mchangani akidhani kuwa maadamu hamuoni adui yake , adui naye hamuoni hatimae huliwa. CCM , baada ya kutumia silaha za kivita na kuuwa wapinzani wanataka maridhiano. Maridhiano hayawezekani bila kutenda haki. Ingelikuwa wanafuata katiba isingelifika hapa. Kwanini muibe kura wakati tuna serika ya kitaifa?. Sasa munabembeleza tuwe pamoja wakati mulipoleta Jeshi hamukufikiria kama tutahitaji kuwa barazani pamoja?. Dunia ya kutumia nguvu dhidi ya raia ilipitwa na wakati. Sasa hivi tusubiri akina Sirro , Mamabo sasa, Awadhi na wakuu walio amrisha kuuwawa kwa raia wakajibu kwa walio wafanyia raia wa nchi hii. Kesi na ushahidi tumekwisha peleka na bado wanaendelea kudhalilisha watu. Usiku wa kuamkia leo walikuwepo kijijini pemba na kupiga watu majumbani mwao. Wanadhani wakifanya vituko pemba dunia haioni. Kila wanachofanya kimewekwa kwenye faili na kukabidhiwa kwa prosecutor wa ICC. Tungekuwa tumenyamaza lakini na wao hawatakuwa na raha maisha yao.
 
Suala la muungano utazeeka na uta r.i..p bila kuguswa kwani linashughulikiwa kistaarabu na kindugu.Punguza mihemuko
Umetoa maone yako vizur ila mwisho unasema mm nina mihemuko. SAWA.
BORA ushambulie hoja sio mtu .
 
Wanabodi, kiukweli kabisa jf inasaidia sana. Kufuatia ushauri huu kwa Maalim Seif, ameukubali, na haya ndio matokeo ya ushauri huu!.
Huu sasa ndio uamuzi wa busara, sio kususa tuu bila mpango.
Asiyekubali kushindwa sio mshindani, if you can't get what you want, just take what you get!, and if you can't beat them, join them!.
Hatimaye ACT Wazalendo sasa wamekubali matokeo, sio tuu watapokea kidogo walichopata, bali pia wata wa join them kwenye kuunda SUK.
Hongera sana ACT, hizi ndio siasa za kweli.
P
 
Kazi ya kuelekea kwenye chaguzi bila fujo ianze,
Wafanye uchunguzi kwa yaliyotokea , wakamatwe wahusika na wafunguliwe mashtaka, na walioonewa wapewe haki zao zinazostahiki.
ukitaka kuuwa nyani usimtizame machoni, wajaribu Sana kutowa elimu ya uraia , sio mmoja raia zaidi ya mwengine aidha kwa nasaba yake au anafahamiana na nani au ukubwa wake .....
Laa sivyo nahofia haya mambo yataendelea mpaka raia wachoke na waseme liwalo na liwe.
 
Wewe nakuona kama mtu muovu hapa JF na hata siku nikisikia umepatwa na baya kutoka kwa hao unaowatetea hapa JF, hakika sitokuhurumia wala kukupa pole.

Umekosa utu kwa kiwango cha kutisha na ni mtu hatari sana wewe.
damn!
 
Huo ushindi wa kishindo tena umetokea wapi? uchaguzi ilikuwa ni funika kombe mwanaharam apite au na wewe kasumba zinakusumbua?
 
Huu sasa ndio uamuzi wa busara, sio kususa tuu bila mpango.
Asiyekubali kushindwa sio mshindani, if you can't get what you want, just take what you get!, and if you can't beat them, join them!.
Hatimaye ACT Wazalendo sasa wamekubali matokeo, sio tuu watapokea kidogo walichopata, bali pia wata wa join them kwenye kuunda SUK.
Wana jf, tujifunze kuukubali ukweli jinsi ulivyo, hakuna mkate mgumu mbele ya chai!. Maalim Seif at 77, has everything to gain and nothing to lose.
Hongera Dr. Mwinyi kwa uteuzi huu.
Hongera Maalim Seif kwa kuitanguliza mbele Zanzibar.
Hongera sana ACT Wazalendo for doing the right thing na sasa hizi ndio siasa za kweli za maendeleo, na sio kususa susa bila manufaa yoyote.
P
 
Hizi sasa ndio siasa za ukweli. Sio zile siasa za kususa susa. Wakati Chadema wanaendelea kushupaza shingo, wenzao, wamepiga bao la kisigino.
Naendelea kusisitiza, "if you can't get what you want, then what you get". Yaani usipopata kile kikubwa unachokitaka, pokea hata kidogo ulicho patina!.
Na kwenye mapambano ya kupigania kitu, "if you can't beat them, join them". ACT Wazalendo wameipambania Zanzibar kwa kupigana na CCM, they couldn't beat them, now they have joined them.

Hongera sana ACT Wazalendo kwa kujitambua, hongera sana rais wa Zanzibar, Dr. Hussein Mwinyi kwa kuwa muungwana kama baba yako.
Mungu Ibariki Zanzibar
Mungu Ibariki Tanzania..
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…