DOKEZO Siasa Zetu: Watoto wa wanachama wa CHADEMA wasimamishwa Shule Nkasi kwa maelekezo ya Mkuu wa Wilaya na amri ya mwalimu Mkuu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Fukuza watoto wote na ikiwezekana mtendaji nae awafukuze kijijini mtu anayemtoa mtoto wako ujinga ni mtu wa kumheshimu sana barua inalalamika kuwa wazazi wamewatukana walimu alafu mnasingizia Chadema... Shame on you wote mnaoshabikia ujinga huu
 
Huu ubaguzi tuukemee kwa nguvu zote,huu ushetani unaanza taratibu lakini tusipokemea kuna siku mtu atanyimwa matibabu,kisa huna kadi ya chama fulani
 
Naomba nikuelewe, unataka kusema kuwa yako maneno ambayo kama ni kweli wazazi wa hao watoto waliyatamka kwenye kampeni basi hatua iliyochukliwa dhidi ya hao watoto ni sahihi, really?

Kama hilo ndilo dai lako basi natamka bayana kuwa wewe pamoja na wote wale wanaokuunga mkono au wana fikra kama zako ni binadamu tu kwa umbo na si kwa, hulka, utu, akili na matendo!

Watanzania wanatekwa, wanateswa na wanauawa halafu anatokea nyakubonga anaunga mkono watoto wadogo kuadhibiwa kwa sababu tu ya matamshi ya wazazi kwenye kampeni, really?

Hivi mtu kama nyakubonga asiye na huruma hadi kwa watoto wadogo kwa kauli tu za wazazi wao, atakuwa na huruma gani kwa hao wazazi kama atahisi wanahoji na kukosoa utendaji wake serikalini?
 
Japo umefika mbali ngoja nikujibu tu...

Na japo hatujui mzazi aliwatamkia maneno gani walimu hao ambao kimsingi wana wapambania watoto kwenye mazingira magumu sana ili kuwaondolea ujinga...

Tufanye kauli ya mzazi kwa walimu wa shule hiyo ilikua inawafanya walimu waonekane duni na hawana uwezo wowote wa kufundisha!...

Ni vibaya kumwambia mzazi awatafutie shule nyingine watoto wake?

Watoto wa mzazi anayebeza walimu na kuwaona si chochote huoni wana haki ya kutafutiwa shule nyingine ili wakakutane na walimu mahili?
 
Una uhakika walimu wote ni Makada au ni hisia tu?
Mbona umechagua walimu vipi wakurugenzi wenyewe umekubali kuwa ni makada siyo!
Ndiyo ni vibaya kwa sababu hizi;

Mosi, hakuna sheria, kanuni wala utaratibu wa kumfukuza mtoto kwa kigezo hicho.

Hatujaona taratibu za kinidhamu kufuatwa ktk kumsimamisha mwanafunzi, kuna barua ya kienyeji mno.

Ni haki ya mzazi kukosoa pale ambapo hajaridhishwa na huduma ya mtumishi yeyote (si lazima mwl tu).

Mwisho mtumishi yeyote hana mamalaka ya kumfungia mwananchi na hasa mwanafunzi huduma y kijamii kwa matakwa yake binafsi.
 
Tusubiri uchunguzi wa Mkenda.
 
ChoiceVariable Lucas Mwashambwa mnaamini hili ?
 
Kwahiyo hao watoto hawakutii sheria bila shuruti.
Kumbuka jaji mkuu mstaafu alipokutana na Magufuri ikulu alisema, "mheshimiwa hakuna kitu kinachotupa wakati mgumu kama vimemo vya kutoa hukumu".
 
Pale wenye akili wakikataa kuwa waalimu,mwisho watoto wao hufundishwa na wajinga.

Nadhani na wewe ni Mwalimu mpumbavu ndani ya nchi hii,hakuna tabaka la watumishi wapumbavu na Nyumbu kama waalimu.
 
Kwahiyo hao watoto hawakutii sheria bila shuruti.
Kumbuka jaji mkuu mstaafu alipokutana na Magufuri ikulu alisema, "mheshimiwa hakuna kitu kinachotupa wakati mgumu kama vimemo vya kutoa hukumu".
ukikiuka utaratibu au sheria utawajibishwa ipasavyo tu,

kwani wewe nani gentleman? utaratibu na sheria havizingatii huo ushirikiana gentleman 🐒
 
Pale wenye akili wakikataa kuwa waalimu,mwisho watoto wao hufundishwa na wajinga.

Nadhani na wewe ni Mwalimu mpumbavu ndani ya nchi hii,hakuna tabaka la watumishi wapumbavu na Nyumbu kama waalimu.
Tengua kauli, sijawai kuwa mwalimu Wala sijawahi kuwa sehemu ya maisha yangu Mmeruhusu wajinga wasimamie sehemu nyeti mnamlaumu nani mwalimu kufanya maamuzi ya kijinga. Mmemuonesha anaweza kuwa sehemu ya kuwaweka kwenye maamuzi naye anajiona ni sehemu ya maamuzi. Kinyango mkichonge ninyi halafu mkiogope ...
 
Tusubiri uchunguzi wa Mkenda.
Siyo tusubiri, nenda kaone huko tayari moto umeshamwakia mkuu wa shule na sababu ndo kama hizo nilizokupa, hakukuwa na tatatibu, lakini pia kashawela wazi afisa elimu siasa zisichanganywe na utoaji wa huduma.
 
Tunahitaji kuwapa uongozi watu wenye akili nzuri badala ya machawa kuanzia ujumbe wa mtaa/kijiji hadi taifa na taasisi zote za Uma zikiwemo shule, hospitali,... Vinginevyo shida na migawanyiko itaongezeka. Wapuuzi wasipewe nafasi, wanaharibu.
 
I stayed in school for good 20 years, what are you talking about....
Ualimu this that, hiyo shule ni yake
Kiinglish chako kinaakisi kukaa maelezo yako. Ufundishaji ni uongozi na watendaji wote, si majengo na miundombinu iliyopo.
 
Lakini viongozi wako wameagiza watoto warudi shuleni na walimu kuchukuliwa hatua zi kiutumishi! Mihemuko ya kisiasa kudhani watapewa vyeo imefanya file zao ziwe zito!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…