DOKEZO Siasa Zetu: Watoto wa wanachama wa CHADEMA wasimamishwa Shule Nkasi kwa maelekezo ya Mkuu wa Wilaya na amri ya mwalimu Mkuu

DOKEZO Siasa Zetu: Watoto wa wanachama wa CHADEMA wasimamishwa Shule Nkasi kwa maelekezo ya Mkuu wa Wilaya na amri ya mwalimu Mkuu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Fukuza watoto wote na ikiwezekana mtendaji nae awafukuze kijijini mtu anayemtoa mtoto wako ujinga ni mtu wa kumheshimu sana barua inalalamika kuwa wazazi wamewatukana walimu alafu mnasingizia Chadema... Shame on you wote mnaoshabikia ujinga huu
 
Huu ubaguzi tuukemee kwa nguvu zote,huu ushetani unaanza taratibu lakini tusipokemea kuna siku mtu atanyimwa matibabu,kisa huna kadi ya chama fulani
 
Tatizo hapa tunajaribu kuspeculate kauli ya mzazi...

Hakuna aliyeleta kauli ya mzazi hapa ili tuijadili bila kuegemea upande, japo wenzangu mnatumia hisia kufanya hitimisho...

Hakuna sheria inayoruhusu mwanafunzi afukuzwe shule kwasababu mzazi wake ni mpinzani...

Hivyo ni ngumu kuamini mwalimu mkuu hana akili ya kulijua hilo...
Naomba nikuelewe, unataka kusema kuwa yako maneno ambayo kama ni kweli wazazi wa hao watoto waliyatamka kwenye kampeni basi hatua iliyochukliwa dhidi ya hao watoto ni sahihi, really?

Kama hilo ndilo dai lako basi natamka bayana kuwa wewe pamoja na wote wale wanaokuunga mkono au wana fikra kama zako ni binadamu tu kwa umbo na si kwa, hulka, utu, akili na matendo!

Watanzania wanatekwa, wanateswa na wanauawa halafu anatokea nyakubonga anaunga mkono watoto wadogo kuadhibiwa kwa sababu tu ya matamshi ya wazazi kwenye kampeni, really?

Hivi mtu kama nyakubonga asiye na huruma hadi kwa watoto wadogo kwa kauli tu za wazazi wao, atakuwa na huruma gani kwa hao wazazi kama atahisi wanahoji na kukosoa utendaji wake serikalini?
 
Naomba nikuelewe, unataka kusema kuwa yako maneno ambayo kama ni kweli wazazi wa hao watoto waliyatamka kwenye kampeni basi hatua iliyochukliwa dhidi ya hao watoto ni sahihi, really?

Kama hilo ndilo dai lako basi natamka bayana kuwa wewe pamoja na wote wale wanaokuunga mkono au wana fikra kama zako ni binadamu tu kwa umbo na si kwa, hulka, utu, akili na matendo!

Watanzania wanatekwa, wanateswa na wanauawa halafu anatokea nyakubonga anaunga mkono watoto wadogo wanyimwe haki yao kwa sababu tu ya matamshi ya wazazi kwenye kampeni, really?

Hivi mtu kama nyakubonga asiye na huruma hadi kwa watoto wadogo kwa kauli tu za wazazi wao, atakuwa na huruma gani kwa hao wazazi kama atahisi wanahoji na kukosoa utendaji wake serikalini?
Japo umefika mbali ngoja nikujibu tu...

Na japo hatujui mzazi aliwatamkia maneno gani walimu hao ambao kimsingi wana wapambania watoto kwenye mazingira magumu sana ili kuwaondolea ujinga...

Tufanye kauli ya mzazi kwa walimu wa shule hiyo ilikua inawafanya walimu waonekane duni na hawana uwezo wowote wa kufundisha!...

Ni vibaya kumwambia mzazi awatafutie shule nyingine watoto wake?

Watoto wa mzazi anayebeza walimu na kuwaona si chochote huoni wana haki ya kutafutiwa shule nyingine ili wakakutane na walimu mahili?
 
Una uhakika walimu wote ni Makada au ni hisia tu?
Mbona umechagua walimu vipi wakurugenzi wenyewe umekubali kuwa ni makada siyo!

Ndiyo ni vibaya kwa sababu hizi;

Mosi, hakuna sheria, kanuni wala utaratibu wa kumfukuza mtoto kwa kigezo hicho.

Hatujaona taratibu za kinidhamu kufuatwa ktk kumsimamisha mwanafunzi, kuna barua ya kienyeji mno.

Ni haki ya mzazi kukosoa pale ambapo hajaridhishwa na huduma ya mtumishi yeyote (si lazima mwl tu).

Mwisho mtumishi yeyote hana mamalaka ya kumfungia mwananchi na hasa mwanafunzi huduma y kijamii kwa matakwa yake binafsi.
 
Tusubiri uchunguzi wa Mkenda.
 
Nilifika Salama kiongozi safari yangu,

Genge la wahuni sio CCM tu ni mchanganyiko wa watu wengi.

Raisi Samia ni weak na asie na sifa ya nafasi aliyonayo (yeye kajikita kuteua watu wa usalama na wenye kujua tiktakata) za ndani ya CCM kumlindia uraisi wake.

Lakini hana leadership qualities ya kuelewa mambo yanayoendelea uraiani ni jukumu lake kuyatatua (the woman is incompetent).

Shida ni kwamba watu wanacheza game la hatari kumchafua, hawa watu hawathamini maisha ya watu. Wengine anaawaamini mwenyewe huyo mama.

Kawatoa wale walinzi wenye sifa ya kulinda ya nchi, na kuweka watu ambao hawana sifa ya ulinzi wa nchi kwa maslahi yake (shida hao aliowaweka wanamaslahi mengine).

Ni shida
ChoiceVariable Lucas Mwashambwa mnaamini hili ?
 
Gentleman,
ukileta ukaidi kwenye kutii sheria bila shuruti, au kuleta siasa zako za kichochezi, Polisi tanzania hawawezi kukuchelewesha hata sekunde moja kuleta fujo au vurugu miongoni mwa wananchi wastaarabu. Fanya siasa kisataarabu.

ukiletwa mahakamani,
hakuna huruma wala aibu utahukumiwa kulingana na makosa yako bila kujali kisingizio cha kutokujua sheria :BASED:
Kwahiyo hao watoto hawakutii sheria bila shuruti.
Kumbuka jaji mkuu mstaafu alipokutana na Magufuri ikulu alisema, "mheshimiwa hakuna kitu kinachotupa wakati mgumu kama vimemo vya kutoa hukumu".
 
Siasa zisifanye hadi kuwatukana waalimu wa shule wanaosoma watoto maana wao wanakaa nao muda wote wakati wa masomo kulingana na mzazi kutokuwa na Imani na waalimu. Waalimu wamefanya jambo la busara kuwarudisha watoto kwa wazazi ili mzazi apeleke watoto shule atakayokuwa na Imani na waalimu ... Mbona ni jambo la busara waalimu wamefanya na wameandika na barua inajieleza shule zipo nyingi ..
Pale wenye akili wakikataa kuwa waalimu,mwisho watoto wao hufundishwa na wajinga.

Nadhani na wewe ni Mwalimu mpumbavu ndani ya nchi hii,hakuna tabaka la watumishi wapumbavu na Nyumbu kama waalimu.
 
Kwahiyo hao watoto hawakutii sheria bila shuruti.
Kumbuka jaji mkuu mstaafu alipokutana na Magufuri ikulu alisema, "mheshimiwa hakuna kitu kinachotupa wakati mgumu kama vimemo vya kutoa hukumu".
ukikiuka utaratibu au sheria utawajibishwa ipasavyo tu,

kwani wewe nani gentleman? utaratibu na sheria havizingatii huo ushirikiana gentleman 🐒
 
Pale wenye akili wakikataa kuwa waalimu,mwisho watoto wao hufundishwa na wajinga.

Nadhani na wewe ni Mwalimu mpumbavu ndani ya nchi hii,hakuna tabaka la watumishi wapumbavu na Nyumbu kama waalimu.
Tengua kauli, sijawai kuwa mwalimu Wala sijawahi kuwa sehemu ya maisha yangu Mmeruhusu wajinga wasimamie sehemu nyeti mnamlaumu nani mwalimu kufanya maamuzi ya kijinga. Mmemuonesha anaweza kuwa sehemu ya kuwaweka kwenye maamuzi naye anajiona ni sehemu ya maamuzi. Kinyango mkichonge ninyi halafu mkiogope ...
 
Tusubiri uchunguzi wa Mkenda.
Siyo tusubiri, nenda kaone huko tayari moto umeshamwakia mkuu wa shule na sababu ndo kama hizo nilizokupa, hakukuwa na tatatibu, lakini pia kashawela wazi afisa elimu siasa zisichanganywe na utoaji wa huduma.
 
Tunahitaji kuwapa uongozi watu wenye akili nzuri badala ya machawa kuanzia ujumbe wa mtaa/kijiji hadi taifa na taasisi zote za Uma zikiwemo shule, hospitali,... Vinginevyo shida na migawanyiko itaongezeka. Wapuuzi wasipewe nafasi, wanaharibu.
 
I stayed in school for good 20 years, what are you talking about....
Ualimu this that, hiyo shule ni yake
Kiinglish chako kinaakisi kukaa maelezo yako. Ufundishaji ni uongozi na watendaji wote, si majengo na miundombinu iliyopo.
 
DC ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya...

Kama mzazi alitoa kauli za vitisho, walimu wana haki ya kumshirikisha DC...

Nashauri tunapokuwa kwenye mikutano ya kisiasa tujifunze kuchagua maneno ya kuongea...

Walimu si wanasiasa, na hivyo hawana ngozi ngumu za kuvumilia kauli za kisiasa...

Wao kila kauli wanaweza kuichukulia katika uzito unaostahili...

Hivyo kama mzazi alitamka maneno makali kisiasa,

Yaani hakumaanisha alichokisema (maana hii ndio siasa ya Tanzania)akaombe radhi.
Lakini viongozi wako wameagiza watoto warudi shuleni na walimu kuchukuliwa hatua zi kiutumishi! Mihemuko ya kisiasa kudhani watapewa vyeo imefanya file zao ziwe zito!
 
Back
Top Bottom