DOKEZO Siasa Zetu: Watoto wa wanachama wa CHADEMA wasimamishwa Shule Nkasi kwa maelekezo ya Mkuu wa Wilaya na amri ya mwalimu Mkuu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Ndiko tunakoelekea huku.Alianza Magufuri sasa haya madhara yamekomaa nchi nzima mwisho na madaktari na manesi hawatawahudia wagonjwa ambao ni wafuasi wa Chadema.
 
CCM inaelekea siku zake za mwisho. Vitu kama hivi ni lazima vitoke, hamtakiwi kusikitika.

Chama kikubwa kama CCM kinafanya move ya kitoto kama hii. Tuwe wakweli chama kinapotia mengi sana.
Uko sahihi haya ni maelekezo kutoka kwenye taasisi hiyo ya chama kongwe.
 
Huko CCM mbona kuna mambo ya kipumbavu sana.
 
Utaambuwa "amri imetoka juu".
 
Sababu uliyotaja haiko kwenye barua uliyoambatanisha...

Umetunga sababu sio?

Hapo nimesoma, sababu si baba yao kuwa Chadema bali kauli zake juu ya walimu wa shule hiyo...

Ungetuwekea hapa hiyo kauli aliyoitoa huyo bwana hapa ili tuijadili.
We jifunze kujiongeza, kauli zilizotolewa na mzazi ni wakati wa uchaguzi akiwatuhumu walimu kutokuwa na imani nao ktk kusimamia uchaguzi. Hauoni uwiano hapa?
 
Infact you do not have writing skills! but you can speak fluent english by look of it!

My advice, try to use one language Swahili or English in a single post ili watu waelewe.
 
We jifunze kujiongeza, kauli zilizotolewa na mzazi ni wakati wa uchaguzi akiwatuhumu walimu kutokuwa na imani nao ktk kusimamia uchaguzi. Hauoni uwiano hapa?
Ndio maana nimeshauri kauli ya mzazi iwekwe mezani tuijadili
 
Hi
Hivi uko sawa kweli, kama mwl hana ngozi ngumu kisiasa kwa nini akubali kusimamia uchaguzi lakini pia akiwa ni kada wa chama hicho Cha ccm. Yaonekana kuwa mzazi na mwl msimamizi walikwazana ktk kutoaminiana kisiasa. Kwa akili yako suala hili linakwendaje kwa watoto.
 
Hii ni vita imetangazwa na Serikali kwa ushirika na CCM wapinzani huko mliko muelewe hamna mama wala baba wala serikali ya kuwatetea.
 
Ndio maana nimeshauri kauli ya mzazi iwekwe mezani tuijadili
Barua hiyo iliyopo inajitosheleza kupata muktadha wa malumbano ya mzazi na walimu, na kwa namna yoyote ktk muktdha huo wa uchaguzi haitoi nafasi hata kidogo ya mambo hayo kuhamishiwa kwa watoto.
 
Kwamba yanayoendelea nchini kwa Sasa chanzo siyo Magufuli ?
 
Ni lini wasimamizi wa uchaguzi walianza kuwa makada wa chama?

Na kama tatizo ilikuwa wasimamizi wa uchaguzi, huyo mzazi alipaswa kujua pale hawakwenda kama walimu bali wasimamizi wa uchaguzi...

Ambapo kisheria huwa wako neutral hawana Chama cha siasa...

Kama mzazi hana imani na walimu, alipaswa akaongee kwenye vikao vya wazazi...
 
Akosee mzazi aadhibiwe mtoto! Hao walimu wana kiwango gani cha Elimu?
 
Kipindi cha Magufuli watu hawakupigwa risasi mbele ya wake zao na watoto wao (ushenzi gani huo).
Unaongea nini wewe, unasahau Lissu kumwagiwa mvua ya risasi au mwenyekiti wa chadema Hananasif aliyekatwa mapanga mbele ya mke wake au diwani wa chadema huko moro aliyepigwa risasi mbele ya mkewe

, but then he is not involved on the decisions which were made to exclude innocent kids because of their parents political affiliations.
He's responsible because there's something called precedence that some inhumane actions are now new normal. That's why we implicate JPM as a perpetrator of all this nonsense.
 
Sasa hivi watu hao hao wanauwa bila ya soni kumchafua Samia.

CCM kupora chaguzi hakuna anaeweza wabishia, lakini haya mauaji ni genge la wahuni wengine.
Sasa kwanini samia asiwakamate ili wasimchafue? Yaani mtu anatekwa hadharani alafu serikali haichukui hatua alafu unadai ni "watu wanamchafua"??

This is typical CCM mindset always looking for a scapegoat
 
Kama ni mwl taifa tuna safari ndefu. Kwamba wasimamizi siyo makada! Unajielewa wewe ? Kwa ukada wake ndiyo maana alishindwa kuwa neutral akaishia kukwazana mzazi. Ama mzazi kutokuwa na Imani na mwl ni haki yake kama haridhishwi na utendaji wake na wala si kazi ya mwl kumfukuza mwanaye hakuna sheria ya hivi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…