Siasa zetu za vyama zimefika saturation point kwa CHADEMA

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
64,960
Reaction score
111,265
Ilianza NCCR ikapotea CUF wakachukua nafasi yao CUF nayo ikapotea CHADEMA ikachukua nafasi ila kwa tulipofika sasa mabadiliko yatapatikana kupitia CHADEMA au hayatapatikana kabisa. Hakuna dalili kuna chama kitakachoweza kuchukua nafasi ya CHADEMA kutoka miongoni mwa vyama vilivyopo au hata chama kipya kitakachoanzishwa, ACT walijaribu wakashindwa vibaya na wameishia kuwa chama za Zanzibar zaidi, CHAUMMA nao walijaribu wakaangukia pia.

Ikiwa CHADEMA itapotea au itafutwa na dola kuna uwezekano mkubwa watu wakaachana na siasa za vyama kabisa.
 
Vyama vingi vimo kwenye mikono ya CCM operatives wanaovaa sare za wapinzani.
 
Upinzani wa kweli utatoka ndani ya ccm yenyewe!! Nukuru frm Nyerere
 
Chadema ni hatari kwasasa nadhani hata tiss wale wenyewe achana na wale chawa. Mbowe kama kashindwa kukipasua hakuna atakayeweza tena fikiria tu mwenyekiti mbowe ana zaidi ya miaka 30 ndani ya chama na hela anayo lakini kwa uroho wake alitaka kukiharibu chama lakini kashindwa
 
HAPANA last resort itakuwa ni vita vya msituni ...and this is coming soon unless wahuni wa ccm wanatokewa na Roho Mtakatifu
 
Nakubaliana na wewe. Watawala watakuwa wamefanya kosa kubwa sana kuifuta chadema. Even God knows. People are tired. Si kwamba watu wanaipenda chadema. Ni kwamba tuu wanakubaliana na hoja zao nyingi. Bahati mbaya, wanasiasa/watawala wengi bado wanaongozwa na siasa za mazoea. Mfumo wa sasa wa CCM hauwezi kuendana na matakwa ya watanzania walio wengi. Hata wao wanajua. Ndo maana wanatumia nguvu kubwa kujenga na kulinda hofu kuliko kuliko kutenda haki.
 
Ina maana Chadema ndio sura ya upinzani Tanzania kwa sasa?.

kwanini watawala wapambane kuizuia Chadema wakati nchi bado inahitaji hizo nguvu kujijenga ?..
 
HAPANA last resort itakuwa ni vita vya msituni ...and this is coming soon unless wahuni wa ccm wanatokewa na Roho Mtakatifu
Hii ni hatari sana, kuna kiongozi wa UWT anasema anatamani kupoteza wapinzani!
 
Chadema ni Imani,hakuna wa kuifuata Chadema.
 
Eti saturation point😁😁
 
Vyama vya upinzani vimeshagota mwisho wa uwezo wao chini ya mfumo huu wa sasa.

CHADEMA haiwezi kukua zaidi ya hapa na wala haiwezi kushuka chini ya hapa bila kuua dhana nzima ya upinzani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…