Siasa zetu za vyama zimefika saturation point kwa CHADEMA

Siasa zetu za vyama zimefika saturation point kwa CHADEMA

Muda umefika kwa Chadema kubadilisha matumizi ya "nyomi" inayojaza mikutano yao ya hadhara.

Waielekeze sasa hiyo "nyomi"direct kwenye harakati za kuikomboa nchi, kuishinikiza serikali kuleta mabadiliko ikiwemo Lissu kuachiwa huru bila masharti yoyote.

Muda wa kufurahia "nyomi" kwenye mikutano ya hadhara Chadema umeshapita, hili sio jambo geni tena.
 
Hii ni hatari sana, kuna kiongozi wa UWT anasema anatamani kupoteza wapinzani!
Huyo kidampa atapotea yeye kabla ya upinzani kupotea.

Nyerere alinusurika mapinduzi ya kijeshi 1964 kutokana na askari wazawa kuona uonevu katika mgawanyo wa vyeo .

Baada ya Nyerere kufuta vyama vingi 1965 alibakia yeye na chaguzi za chama kimoja za kiinimacho wa picha yake na kivuli haikumsaidia.

1970 alinusurika kupinduliwa.

1982 ndege ya Tanzania ilitekwa na kubadilishwa uelekeo na wateka nyara wakitaka Nyerere ajiuzulu kutokana na ugumu wa maisha.

Mwaka 1982 hiyo hiyo wale wanajashi akina Hanspope na kundi lake walitaka tena kumpindua Nyerere huku sababu kubwa ni ugumu wa maisha na upatikanaji wa bidhaa za mahitaji ya msingi kua adimu baada ya vita vya Kagera.

Hii inatupa picha kwamba hata upinzani wa vyama usipokuwepo sio suluhisho kwa serikali dhalimu kutawala watu kwa mabavu na amri bali unaweza kutokea upinzani mwingine usio wa chama wala mrengo bali kikundi cha watu wakidai maslahi ya nchi yarekebishwe.

Hivyo huyu kidampa Chatanda afahamu na ajibidiishe kusoma historia kua mapinduzi hayaletwi na chama bali pale watu watakapochoshwa na ugumu wa maisha, ufisadi ,uonevu watachukua hatua na ndio maana mapinduzi yote hayo hayakua na mrengo wa chama chochote na pengine kama sio wale jamaa kulewa siku chache kabla wangefanikisha walichopanga.
 
Hiyo siku ni ipi? ccm yenyewe haijiwezi ndio itaweza kujiundia project?
Mwambie kuwa kilikuwa kilinge cha ccm ila sio sasa wambea wote wamekimbia bado wawili wakubwa wanafahamika na wameachwa maksudi na hawaji pata nafasi kubwa
 
Ilianza NCCR ikapotea CUF wakachukua nafasi yao CUF nayo ikapotea CHADEMA ikachukua nafasi ila kwa tulipofika sasa mabadiliko yatapatikana kupitia CHADEMA au hayatapatikana kabisa. Hakuna dalili Kuna chama kitakachoweza kuchukua nafasi ya CHADEMA kutoka miongoni mwa vyama vilivyopo au hata chama kipya kitakachoanzishwa, ACT waliojaribu wakashindwa vibaya na wameishia kuwa chama za Zanzibar zaidi, CHAUMMA nao waliojaribu wakaangukia pia.

Ikiwa CHADEMA itapotea au itafutwa na dola kuna uwezekano mkubwa watu wakaachana na siasa za vyama kabisa.
Sidhani kama kitatokea chama kingine Cha upinzani chenye nguvu kama Chadema, waendelee kujipanga vzr maana mpaka sasa washaishinda nguvu, CCM huo ndo ukweli.

Password ya mwisho kabisa kuindoa CCM madarakani ni vyombo vya Dola. Chadema wakifanikiwa kuivunja hiyo password basi kazi kwisha.sasa ni namna Gani wataifungua hiyo password Mimi sijui
 
Sina tatizo na ulichoandika hapa; ila nadhani kuna umuhimu wa kuiwekea 'focus' hiyo inayoitwa CCM wakati huu zaidi ya hivi vyama vingine; hasa hasa CHADEMA.

Kwanza nikukumbushe kama umesahau haraka namna hiyo: CHADEMA ,Magufuli alinuia kuiua moja kwa moja kwa mabavu na pesa; akashindwa. Samia nusra aimalize kwa ulaghai wake mwingi kwa kumnunua Mbowe na chama kiujumla; kakumbana na kisiki.

Kwa hiyo jaribu kuitazama kitofauti kabisa CHADEMA iliyopo, tofauti na hiyo mifano mingine uliyoitumia kujenga hoja zako..

CCM iliyokuwa inafanya yote hayo yaliyowapata akina CUF; NCCR, n.k., haipo tena. Hii nayo ni hoja unayotakiwa kuichukulia maanani.

Vyombo wanavyotumia, kama hao wasajili; mahakama, polisi, na hata serikali kutenga fungu la kuwashughulikia wapinzani, hata wao wanabadilika, hawatakuwa walewale waliotumiwa katika nyakati hizo ulizozitaja wewe.

WaTanzania, na hatma ya nchi yao, huwezi tena kuwaweka pembeni na kufikiri wataendelea tu kuwa watazamaji. Hawa ndio watakaoiokoa CHADEMA isiangukie kwenye hiyo mifano uliyoitumia hapa.

CHADEMA HAIFUTIKI, na wala HAIFI tena ndani ya jamii ya kiTanzania.
 
Sidhani kama kitatokea chama kingine Cha upinzani chenye nguvu kama Chadema, waendelee kujipanga vzr maana mpaka sasa washaishinda nguvu, CCM huo ndo ukweli.

Password ya mwisho kabisa kuindoa CCM madarakani ni vyombo vya Dola. Chadema wakifanikiwa kuivunja hiyo password basi kazi kwisha.sasa ni namna Gani wataifungua hiyo password Mimi sijui
Hiyo 'password" ndiyo wanayoishikilia WaTanzania kwa makini sana wakati huu.
 
Back
Top Bottom