Siasa zinatufanya tumkufuru Mungu hata kuhusu corona

Siasa zinatufanya tumkufuru Mungu hata kuhusu corona

Tila-lila2

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2019
Posts
652
Reaction score
1,058
Wengine tuliofiwa na Ndugu tokana na gonjwa hili la Covid 19 ndiyo tunajua machungu yake. Serikali yetu, naapa mbele za Mungu Wetu, ilipoamua kusimamisha kupima maambukizi ilificha mengi. Halijaisha juma moja nina uhakika na kifo cha Ndugu yangu mwingine kuwa kilisababishwa na corona. Ni kweli maambukizi yawezekana yamepungua kutokana na hatua zilizochukuliwa na zinachochukuliwa na kila mmoja wetu hapa nchini na binadamu wote duniani.

Lakini tusimkufuru Mungu na kuwabeza wale wanaochukua tahadhari kama Spika Job Ndugai. Tena inawezekana kabisa Job Ndugai anaijua afya yake ilivyo na hivyo basi hata ka-corona virus kamoja tu kanaweza msababishia mengine. So anapovaa barakoa anatakiwa kupongezwa.

Tusimkufuru Mungu tuendelee kuchukua tahadhari kama kawaida, corona bado ipo na inaua!
 
Weka vyeti vya vifo vya hao ndugu zako waliokufa kwa Covid-19. Vinginevyo ni uzandiki.
 
Hadi unauwa ndugu zako kisa uonekane kuna corona ,nani anajari sasa wewe kufiwa wafe wote tu nani hajawahi kufiwa humu
 
Back
Top Bottom