Sidanganyiki - Leo ndio mnajua Tanzania inahitaji katiba mpya?

katiba mpya Tanzania haikuanza kuzungumzwa leo. Mkapa hajalikalia kimya enzi zake kama mwanakijiji anavyotaka ieleweke.

Katiba mpya imezungumzwa sana na karibu vyama vyote, kwa miaka kadhaa.

Msilete uzishi.
 

Salamu wakuu,
Mimi nadhani hii mada ni muafaka sana kwa wakati huu kwa vile kuna hatari kubwa ya hii hoja kuwa "hijacked" na "Wadandia hoja" i.e CCM. Sababu ni kuwa hivi sasa baada ya CDM kujinadi kwa ahadi ya kuanzisha mchakato wa kuandika katiba mpya na wananchi kuwaunga mkono kwa kiasi kikubwa kuliko watawala walivyotarajia wameona kuwa public opinion iko in favour of these changes.So kinachotokea ni kujaribu kuiba hoja hii ya CDM ili kuwa preempt,Lakini pia tofauti na CDM ambayo ilitaka kuoverhaul the Constitution,hawa wasanii wanataka kumanage hii process ili kufanya patch up job kwenye katiba ambayo itaendelea kulinda na kustawisha maslahi na uimla wa kiutawala kwa CCM and cronies wake.Na hapa ndipo ninapoona hatari kubwa sana.Kwamba hawa watu watajipa jukumu la kusimamia huu mchakato kiusanii kama walivyofanya kwa masuala mengine makubwa na nyeti kwa taifa.Matokeo yake ni kutulazimisha kukubali a watered down version ya katiba mpya isiyo na mabadiliko ya msingi na hivyo kutokuwa na tija.
Na hapa ndipo CDM na wapenda mabadiliko wote,ndani na nje,tunapotakiwa kuwa vigilant na kushinikiza meaningful involment and participation ya broader section ya public ili kuzuia hii charade ya CCM na cronies wake.


"True freedom must be expressed through the human ability to think critically, to analyze and to make informed decisions about oneself, his society and the world "- Sidanganyiki2010
 
Mwanakijiji nimekupata..

nami hii kasi ya kudai katiba MPYA, has kutoka kwa viongozi wa zamani waandamizi wa CCM na serikali yao ndo inanishangazaa zaidii. leo balozi mstaafu, brigedia Hashim Mbita kupitia gazeti la mwananchi (10/12/2010) anadai katiba MPYA!!!. Kanishangaza kwamba msukumo wake ni kwamba katiba ya sasa inawapa wahisani NGUVU ya kutupangia nn cha kufanya na kutokufanya..shame on him! huu ni unafiki kwani hii sababu aliyoitoa sio chanzo cha kudai katiba MPYA...Ila ndo hivyo naye ameingia kwenye kundi la walilia KATIBA MPYA 2010..

Kinachowasukuma wengi kutoka ndani ya CCM viongozi wa waastafu ni majerahaa ya uchaguzi 2005-2010,2010 -2015. makundi yamewafikisha hapo na sasa kunyoosheana kidolee kwa masilahi binafsi zaidi kupitia hoja za umma.
 
Acheni wenye sauti waongee. Sote tunaona KATIBA ya sasa inavyotutenda. Na Mwalimu au mtu wa hadhi na heshima yake hatuna. Mzee Mbita na Prof Mpangala jana pale TBC1 walijitahidi kueleza kwa nini tunahitaji KATIBA MPYA. Tena tusipoteze muda kuunda Bunge au Mahakama ya KATIBA. Kenya wameandika vizuri sana KATIBA yao kwa sehemu kubwa. Sio vibaya tukiitumia ile kwa kuondoa yale ambayo yamekaa KiKenya na kuingiza ya KiTanzania
 
Kwenye msafara wa mamba na kenge wapo,hatutegemei kila Kiongozi anayeongelea sasa hivi katiba mpya anamaanisha ile wanayotaka wananchi kama mchakato wa kupata maoni utaanza ndio hapo tutakapojionea nani ni kweli alimaanisha Katiba ya maslahi ya Taifa na nani alitaka Katiba ya kulijali kundi fulani.Hizi tunazozisikia sasa ndo wale 70% aliyosema Kikwete...fuata upepo.
 
Swala la katiba limeonekana kitambo sana. Sababu za wana ccM kudai katiba ni kuchafua akili za watu wahame kwenye msitari. Tusipokua macho ajenda itavutwa hadi uchaguzi 2015. Wanafuata upepo na najua wanatafuta trick ya kutokea ili warudi kwenye chart
 
kwanini sasa hivi tunahitaji sana "katiba Mpya"? nini kimetokea ambacho hao wanaodai Katiba Mpya hawataki kukisema. Kwa sababu as a matter of fact yote wanayoyasema yalikuwa kweli kwa miaka mitano iliyopita; why now?

NAFIKIRI THE PUSH COMES FROM CHADEMA MP'S WALK OUT AMONG OTHER THINGS:angry::angry:
 

Hiyo ndiyo tofauti iliyopo kati ya Mzee Mwanakijiji na Malaria Sugu.
 
Hiyo ndiyo tofauti iliyopo kati ya Mzee Mwanakijiji na Malaria Sugu.

Upupu mtupu, anataka kujifanya kana wazo la katiba mpya ni lake! Hakumbuki kuwa miaka michache ya nyuma lilishaundiwa tume chini ya uongozi wa ccm? Nawe pia hukumbuki?

Msitake kujidai ni wazo lenu. Na muelewe, hiyo katiba iliyopo imesharekebishwa mara ngapi? Chini ya uongozi wa ccm. Katiba si msahafu itakwenda ikibadilika, kuundwa mpya, kurekebishwa, kuongezwa, kupunguzwa maisha yote.

Mimi nawashangaa mnaojifanya kuwa mnashinikiza wakati mnajuwa wazi kuwa katiba mpya ni kwa maslahi ya Tanzania, no matter ni wa chama kipi! CCM chini ya Kikwete itahakikisha inafanya mabadiliko ya Katiba ua japo kuanzisha tu mabadiliko ya Katiba. Hicho ni kitu ambacho si siri wala hakina ubishi. Naona ni wabunge wenu tu ndio wazembe kwa kutopeleka mswada siku zote walizokuwa bungeni.

Haya fanyeni hima, pelekeni mswada bungeni, tupate katiba mpya. Sio kupayuka tu hapa JF.
 
kibaya zaidi wote hawa wanamtwisha zigo JK, ilhali walipokuwa wanafyonza kama yeye anavyofyonza leo walikuwa hawasikii kilio cha katiba mpya. Shame on them.

Kila mtu analia na katiba mpya, kuanzia mimi wa kalumbalesa mpaka aliye wizarani. kinachochekesha hadi jaji mkuu. Really hata jaji mkuu na majaji?? can't they seek audience na mkuu wa nchi na kumweleza kinagaubaga, badala ya kulia lia na waandishi wa habari?
 

Hivi wewe MM hoja zako mbona zinatuchanganya? Wewe unaunga mkono Mkono au unapinga swala la katiba Mpya? Unamtetea nani hapa JK au CCM? Hueleweki, unatumia akili nyingi kuhisi utadhani utafiti wa kisayansi kumbe siasa! Haya mambo ni rahisi, tunataka katiba mpya....upya tunaoutaka utajadiliwa baada ya kukubaliana kwamba tuko tayari kuanza mchakato. Hatutaki Kuongeza vilaka kwenye katiba ya sasa kama unavyotaka wewe pamoja na Waziri wako kombani. Acheni kuchukulia swala hili kwa uzito mdogo tumechokaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa! Hatudanganyikiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii. Peoples pawaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.
 
Mzee M/Kijiji, hongera kwa kuchokoza swali hili hapa JF. Bahati mbaya wachangiaji wengi wameshindwa kulenga shabaha ya swali lako! Upo uwezekano baadhi ya wanaookuunga mkono na wanaotofautiana na wewe hawajaelewa kwa kina swali. Inawezekana, (kama ulivyosema), hata hao viongozi waliotamka uwepo wa haja ya Katiba Mpya (KM), huenda hawana jibu la swali lako, au wana malengo tofauti tofauti.

Kwahiyo ipo haja, kwa wana JF na wa-Tz wote kwa ujumla, kuelewa kwa mapana yake haja hii ya kuwa na KM. Wale wanaodai kwamba ni swala la wakati umefika, sidhani kama ni kweli… kwani hata Mwl. Nyerere alikuwa anafahamu ubovu wa katiba tuliyo nayo, na aliwahi kusema kuwa katiba inampa madaraka makubwa kiasi kwamba kama akiyatumia madaraka hayo atageuka kuwa dictator. Nyerere aliitumia katiba iliyopo kwa kusaidiwa na maadili ya uongozi, sera za Kijamaa, hekima yake na mapenzi yake kwa watu wake. Hivyo watu wengi waliridhika na uongozi wake na haja ya KM haikuwa hitaji la lazima sana wakati wake.

Katika kipindi ambacho misingi ya kijamaa imetupwa, uadilifu umepoteza nafasi na ufisadi kuchukua nafasi yake, watu wamepoteza imani na viongozi. Viongozi wanatumia baadhi ya vifungu dhaifu vya katiba kubaki madarakani, lakini kwa manufaa ya wachache, na walio wengi wakiendelea kubaki masikini.

Watu wameamka na wanaonesha kukataa hiyo hali. Njia ya kukataa hali hiyo ni kura, kwenye uchaguzi, lakini bahati mbaya katiba iliyopo haitoi fursa ya uchaguzi huru! Mwaka huu watu walitaka kufanya mabadiliko ya uongozi na katiba imewanyima fursa hiyo !

Baada ya uchaguzi wa mwaka huu, inaonekana wazi kuwa hamkani si shwari tena, dalili za wazi zinaonesha hitaji la watu. Watu walewale, waliomwamini Nyerere, sasa wanaona kiti cha Nyerere kimekaliwa na Ngedere, na hawako tayari kutoa imani yao kwa Ngedere!

Agenda ya KM ilitumiwa na CDM kwenye election manifesto yao, imeonesha kupokelewa vyema na wananchi wengi. Sera za CDM zilikubalika zaidi kuliko sera za CCM. Kutokana na hali hiyo, yafuatayo ymejitokeza:

(1) CCM haiwezi kuendelea kuizima haja ya KM
(2) CCM imeona dalili za kukataliwa na mwelekeo wa kutoweka kwa utulivu wa zamani
(3) CCM haina uwezo wa kuzalisha sera/agenda mwafaka zaidi ya kudandia sera za upinzani ili kuweza kuwapa imani na kuwatuliza wananchi
(4) CCM ina aibu kubwa na ya kweli kwa matokeo ya sera zake zilizozaa ufisadi,
(5) CCM imefanya vibaya kwenye uchaguzi wa mwaka huu kuliko wakati wowote

Kwahiyo matamko ya viongozi kuhusiana na KM yanatokana na hali hiyo na yataendelea na viongozi wengi zaidi watayasema hata Katibu Mkuu Mzee Makamba atatoa tamko lake very soon.
 
Mwanakiji
Jibu ni rahisi sana.Huko nyuma suala la katiba mpya halikupew uzito sana kama wakati huu kwa sababau haikuwahi kutokea viongozi wa dini kutengeneza ilani za uchaguzi na kuingilia siasa kama ilivyofanyika mara hii.Akina Mkapa na wengine wameona kuna hatari inalinyemelea taifa kwani viongozi wa dini wameanza kuwaadhibu wafuasi wao kwa sababu za kisiasa.Katiba mpya lazima iweke uzio kati ya shughuli za dini na siasa
 
Pia kwa vile sera ya katiba mpya iko kwenye ilani ya cuf ambayo alipew jk
 
Maskini mwanakijij ni kupe pole na wanachama wote wa cdm,sasa mbona mnanyan'anywa mtaji wenu?
Msikubali maana mtaji huu mkiukosa cdm inakufa
Hata hivyo hiyo ndio siasa,na mchezo wa siasa una kanuni zake mnapaswa kuzijua ili muweze kufunga magoli
 
Mzeemwanakijiji, siku zote huwa nasema wewe ni pumba nyingi tu, hamna lolote: hujidai kuwa ni mawazo yako tena mapya! fuata hii link uone ni gazeti lipi na tangu lini lilikuwa linapigia kelele katiba mpya, na mpaka (aina) mapendekezo ya katiba wakawasilisha: An-nuur Na. 168
 

Answar suna
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…