Sidanganyiki - Leo ndio mnajua Tanzania inahitaji katiba mpya?

Sidanganyiki - Leo ndio mnajua Tanzania inahitaji katiba mpya?

Lo!
Hakika Gwa kumyitu umeongea jambo la maana sana.
Mkapa, kwanini hakuona kuwa katiba ina mapungufu kipindi cha utawala wake? Kaondoka madarakani ndio analeta kilimilimi

Na ndio desturi ya viongozi wa kiafrika wakiwa madarakani hataki kuambiwa kitu esp Ben khaaa alikuwa mbogo akikosolewa analipiza kwa visasi mwakumbuka alicho mtendea Jenerali Ulimwengu??? Mwajua ni viongozi wachache sana hutaka kufanya mabadiliko na ndio hao huwa twawaita mashujaa wetu unaingia IKULU na unabadiri KATIBA hapo hapo uone kama wananchi watakusaahau hiii biashara ya SI HA SA ndio inaharibu viongozi ati kunaitekeleza ilanio ya CCM atii ilani ya CCM jamani na ndio maana twataka KATIBA mpya kiongozi aingiae na Ilani yake hapo ajue KATIBA inataka maendeleo na sio polojo za ilani ya Chama fulani hapa period

KUna watu walikuwa wanasema "upinzani uungane"; tukawauliza "kwanini?" wakasema "ili waiondoe CCM madarakani". Tukasema "Waiondoe CCM ili kiwe nini?" wakatuambia "haijalishi itoke tu tutajua mbele ya safari". Wenyewe walifikiri wanazungumza hekima.

Sasa wameibuka watu wengine leo wanatuambia "Katiba Mpya", tunawauliza "Upya kivipi"; wanasema "haijalishi tunataka Katiba Mpya". Tunawaambia ili imnufaishe nani wanasema "watanzania wote" tunauliza kwani iliyopo ina matatizo gani? "tunataka Katiba Mpya".

Kama CCM wanadai kweli Katiba Mpya ni lazima wakubali klwanza kabisa kuwa hii iliyopo haifai na imetuletea matatizo na watuambia ni matatizo yapi ambayo hayawezi kuondolewa kwa kufanyia mabadiliko tu ya kawaida ya Katiba. Kwani kilichotokea kwenye uchaguzi mkuu ambabcho hawataki kukitaja ndicho kiini cha madai haya. Wakiseme kwanza.
 
mzeemwanakijiji, siku zote huwa nasema wewe ni pumba nyingi tu, hamna lolote: Hujidai kuwa ni mawazo yako tena mapya! Fuata hii link uone ni gazeti lipi na tangu lini lilikuwa linapigia kelele katiba mpya, na mpaka (aina) mapendekezo ya katiba wakawasilisha: ]an-nuur na. 168[[/COLOR]/quote]

hapo kwenye an -nuur umechemsha magazeti kama hayo nyumbani kwangu nikiishiwa toilet paper ndio huwa natumia kuchambia. au kama sina mfuko wa kubebea kitimoto basi ndio huwa natumia hilo gazeti kufungia kitimoto yangu.
 
Uhitaji wa Katiba mpya ulikuwepo, upo na utaendelea kuwepo kwa wanaoelewa mapungufu ya katiba ya sasa na umuhimu wa kuyaondoa, ila wengi wanafuata upepo ili usiwadhuru!
 
Mzeemwanakijiji, siku zote huwa nasema wewe ni pumba nyingi tu, hamna lolote: hujidai kuwa ni mawazo yako tena mapya! fuata hii link uone ni gazeti lipi na tangu lini lilikuwa linapigia kelele katiba mpya, na mpaka (aina) mapendekezo ya katiba wakawasilisha: An-nuur Na. 168

kama hayo ndiyo mapendekezo ya Katiba Mpya.. basi tuna matatizo zaidi ya nilivyofikiria.. na ndicho ninachosema angalau hapa tumepata mfano wa mapendekezo ya "Katiba Mpya". Naamini hoja yangu hapa imethibitishwa.
 
mzeemwanakijiji, siku zote huwa nasema wewe ni pumba nyingi tu, hamna lolote: Hujidai kuwa ni mawazo yako tena mapya! Fuata hii link uone ni gazeti lipi na tangu lini lilikuwa linapigia kelele katiba mpya, na mpaka (aina) mapendekezo ya katiba wakawasilisha: ]an-nuur na. 168[[/COLOR]/quote]

hapo kwenye an -nuur umechemsha magazeti kama hayo nyumbani kwangu nikiishiwa toilet paper ndio huwa natumia kuchambia. au kama sina mfuko wa kubebea kitimoto basi ndio huwa natumia hilo gazeti kufungia kitimoto yangu.

Haujaipenda? kwa sabau tu, inaonyesha wenzenu walivo na upeo,nyie mnaanza leo, wenzenu washaanza zamani! halafu, mnajidai, katiba mpya, katiba mpya, katiba mpya kaanza kuidai Padiri Slaa. Hana uwezo wala upeo wa kuwa mwanzilishi wa chochote, labda kukurupuwa wake za watu.
 
kama hayo ndiyo mapendekezo ya Katiba Mpya.. basi tuna matatizo zaidi ya nilivyofikiria.. na ndicho ninachosema angalau hapa tumepata mfano wa mapendekezo ya "Katiba Mpya". Naamini hoja yangu hapa imethibitishwa.

Haijathibitishwa tu, bali umeona kuwa watu hawapigi firimbi na pumba kama vile wazo la katiba mpya ni la leo. Nadhani umeona watu wenye upeo toka lini wameanza kutaka katiba mpya na mapendekezo, kumbuka, MAPENDEKEZO. Sio wewe, unamwaga pumba kama vile ndio wazo jipya au ni kitu ambacho hakiongeleki au kimekataliwa. Sijui ni lini mtapata kufunguwa vichwa vyenu? wenzenu wameanza zamaaaani.
 
KUna watu walikuwa wanasema "upinzani uungane"; tukawauliza "kwanini?" wakasema "ili waiondoe CCM madarakani". Tukasema "Waiondoe CCM ili kiwe nini?" wakatuambia "haijalishi itoke tu tutajua mbele ya safari". Wenyewe walifikiri wanazungumza hekima.

Sasa wameibuka watu wengine leo wanatuambia "Katiba Mpya", tunawauliza "Upya kivipi"; wanasema "haijalishi tunataka Katiba Mpya". Tunawaambia ili imnufaishe nani wanasema "watanzania wote" tunauliza kwani iliyopo ina matatizo gani? "tunataka Katiba Mpya".

Kama CCM wanadai kweli Katiba Mpya ni lazima wakubali klwanza kabisa kuwa hii iliyopo haifai na imetuletea matatizo na watuambia ni matatizo yapi ambayo hayawezi kuondolewa kwa kufanyia mabadiliko tu ya kawaida ya Katiba. Kwani kilichotokea kwenye uchaguzi mkuu ambabcho hawataki kukitaja ndicho kiini cha madai haya. Wakiseme kwanza.

Hapa umezungumza jambo la msingi zaidi. Pamoja na kuwa kuna wimbi la kudai katiba, ni muhimu kukaa kwa tafakari ya hali ya juu ili tusiwe na katiba mpya ambayo ni maadam tumetaka katiba mpya.

Lazima iswe ya kutokana na msukumo bali na utashi wwetu watanzania wote wa kutaka katiba mpya na ambayo itakidhi mahitaji muhimu.

Na la kwanza ni kujua wapi katiba ya sasa haitoshelezi matakwa ya wakati tulionao. Hili linapaswa pia kuwepo kwenye utashi wa watawala wetu na sio tu utashi wetu wadai katiba.

Kama akili na mahitaji yetu watanzania hayatakuwa aligned na ya watawala wetu, basi twaweza angukia kuwa na katiba mpya ambayo sifa yake ni katiba mpya na wala sio kukidhi mahitaji ya nchi na wananchi wake kwa wakati huu na ujao.

Hongera MMM
 
Haujaipenda? kwa sabau tu, inaonyesha wenzenu walivo na upeo,nyie mnaanza leo, wenzenu washaanza zamani! halafu, mnajidai, katiba mpya, katiba mpya, katiba mpya kaanza kuidai Padiri Slaa. Hana uwezo wala upeo wa kuwa mwanzilishi wa chochote, labda kukurupuwa wake za watu.

This is complete absurd and immoral. Why cant you give other people their due respect even if you hate them??? Is this what your religion teaches you?? Keep on hating a person but remember to put away from you all immoral anguish and respect others and their work
 
Mzeemwanakijiji, siku zote huwa nasema wewe ni pumba nyingi tu, hamna lolote: hujidai kuwa ni mawazo yako tena mapya! fuata hii link uone ni gazeti lipi na tangu lini lilikuwa linapigia kelele katiba mpya, na mpaka (aina) mapendekezo ya katiba wakawasilisha: An-nuur Na. 168

Mdini sana wewe na MS. Akili yenu ni udini na CCM 24/7
 
naona watu mnashindwa kupata pointi yenyewe na kama kawaida mnaanza kuuliza kama niko bado na akili zangu timamu. Mnapenda mno mazingaombwe kiasi cha kushangilia mkiona sungura katolewa kwenye kofia na wengine wanaweza kuapa kabisa kuwa ni "muujiza". Sasa leo watu wanaanza kuimba "katiba mpya" basi watu wanatakiwa kushangilia:

Hawawaambii tatizo la Katiba ya sasa ni nini? - of course tunatakiwa tuwe tunajua sote
Hawasemi kwanini sasa hivi na haikuwa kabla- tunaambiwa ni muda tu
Hawasemi wanataka nini hasa - yale yale "katiba mpya" - upya wa nini?
Hawasemi ni vitu gani viboreshwe? Je wakibadilisha tu Tume ya Uchaguzi watu wataridhika? Kwanini isiwe kufanyia mabadiliko vipengele vinavyolalamikiwa halafu tukamaliza kwani hilo halihitaji siku nyingi hata kikao cha bunge kinaweza kufanya hivyo.
Ati Katiba iliyopita haikuandikwa na sisi - well kwani kuandika sisi wenyewe kunatuhakikishia vipi Katiba nzuri? Leo hii miaka 49 ya kujitawala mbona baadhi yetu hatujivunii kuoona tunavyojitawala? kwanini tuamini ati kwa vile tutaandika Katiba sisi wenyewe basi itakuwa nzuri? Jamani, kwani vyama vingine vilirudishwa vipi na leo watu hawafurahii wakati tulishirikishwa kuvirudisha?

Katiba Mpya? kwa manufaa ya nani? Siyo wote wanaosema "nyeupe" wanamaanisha "nyeupe pe" wengine wanamaanisha "rangi ya maziwa!"
Katika mahojiano na gazeti moja, Mwl Nyerere alipata kusema kuwa ilikuwa rahisi kudai na kupata uhuru lakini si kuijenga Tanganyika huru. Kwa nini? Watu walidai uhuru kwa malengo tofauti tofauti, Mwingine alimchukia mzungu tu basi, mwingine alichoka kupuuzwa na kuonewa katika ardhi yake, mwingine alijua wakiondoka wazungu weupe yeye anakuwa mzungu mweusi....ongezea. Kwa hiyo kama asemavyo MMK, ni vema tukaweka bayana haya mahitaji ya katiba MPYA ili kutohitilafiana baadae. Nawasilisha.
 
naona watu mnashindwa kupata pointi yenyewe na kama kawaida mnaanza kuuliza kama niko bado na akili zangu timamu. Mnapenda mno mazingaombwe kiasi cha kushangilia mkiona sungura katolewa kwenye kofia na wengine wanaweza kuapa kabisa kuwa ni "muujiza". Sasa leo watu wanaanza kuimba "katiba mpya" basi watu wanatakiwa kushangilia:

Hawawaambii tatizo la Katiba ya sasa ni nini? - of course tunatakiwa tuwe tunajua sote
Hawasemi kwanini sasa hivi na haikuwa kabla- tunaambiwa ni muda tu
Hawasemi wanataka nini hasa - yale yale "katiba mpya" - upya wa nini?
Hawasemi ni vitu gani viboreshwe? Je wakibadilisha tu Tume ya Uchaguzi watu wataridhika? Kwanini isiwe kufanyia mabadiliko vipengele vinavyolalamikiwa halafu tukamaliza kwani hilo halihitaji siku nyingi hata kikao cha bunge kinaweza kufanya hivyo.
Ati Katiba iliyopita haikuandikwa na sisi - well kwani kuandika sisi wenyewe kunatuhakikishia vipi Katiba nzuri? Leo hii miaka 49 ya kujitawala mbona baadhi yetu hatujivunii kuoona tunavyojitawala? kwanini tuamini ati kwa vile tutaandika Katiba sisi wenyewe basi itakuwa nzuri? Jamani, kwani vyama vingine vilirudishwa vipi na leo watu hawafurahii wakati tulishirikishwa kuvirudisha?

Katiba Mpya? kwa manufaa ya nani? Siyo wote wanaosema "nyeupe" wanamaanisha "nyeupe pe" wengine wanamaanisha "rangi ya maziwa!"

Ahsante MM,

CMM na serikali yake hawatesema sababu ya kweli na ndio maana wamekuwa wakipingana wao kwa wao. kuna ukweli kuwa wananchi wengi wameelewa kasoro za katiba iliyoko na hali haitakuwa hivi mwaka 2015 kama hakutakuwa na mabadiliko, hivyo ni wakati sahihi kwa hawa wengine kuonyesha kukubaliana na mabadiliko ya katiba sasa ingawa ni wazi kwetu sote kuwa ni WANAFIKI. wanaona aibu ndani na nje ya nchi na wanajaribu ku-save face though its too late for them!

Bravo Slaa, Bravo Chadema na wooote waliosimama nanyi wakati wa harakati (ambazo bado zinaendelea) kwani response ya hawa ndugu ni dhahiri kuwa mlikuwa sahihi tokea awali!
 
Mzee MM, kuibuliwa kwa nguvu kwa hoja ya katiba mpya mwaka huu ni matokeo ya uchaguzi uliopita. Wako wanaodai katiba mpya kwa mapenzi mema, wapo pia wanaodai kwa maslahi binafsi. Miaka 20 iliyopita hakukuwa na vuguvugu kubwa za siasa za kupingana, maisha katika kipindi hicho yaliendelea kuwa fikra sahihi za kiongozi, wanaoongozwa ni watekelezaji wa fikra. Jambo la msingi la kuangalia hapa ni nyakati, tunao raia wengi wa nchi hii ambao katika kipindi hicho ama walikuwa watoto wadogo, ama walikuwa hawajazaliwa kabisa. Kumbuka miaka 20 ni umri wa kuzaliwa hadi utu uzima kamili. Chachu ya katiba mpya imekuwa ikikua kila kipindi na zile zama za zidumu fikra zinazidi kuyeyuka.
Mzee MM, dalili za kupoteza taifa zimeanza kujitokeza kwa mapana yake mwaka huu, hii ni kutokana na kasoro za mfumo wa namna ya kupata viongozi wa watu wote. Mfumo unaotumika bado ni uleule wa zidumu fikra, na rais aliye madarakani lazima amalize vipindi vyake. Kana kwamba huo ni mfumo sahihi, wale wanaonufaika nao wanaukuza kwa juhudi kubwa na kauli mbiu ya chama tawala milele.
Watu wenye mapenzi mema wametumia dalili za mvua vya mwaka huu kutoa angalizo la miaka mitano ijayo. Janga kuu liko njiani kutokea kwa takwimu sahihi kabisa. Mfano; ongezeko la wapiga kura toka milioni 9 mwaka 2005 hadi milioni 20 mwaka 2010, limesababisha hali ya sintofahamu maeneo mengi nchini. Miaka mitano ijayo kuna uwezekano wa wapiga kura walioandikishwa kufikia milioni 30 (La msingi hapa kijana wa darasa la sita mwaka huu umri miaka 13, ni mpiga kura 2015). Kama wale ambao miaka 20 iliyopita hawakuwa na umri wa utu uzima wameonesha changamoto kubwa ya kudai mabadiliko 2010, hali itakuwaje 2015?
Kama tunalihitaji taifa huru lenye amani, tufikirie mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa nchi, kinyume cha hapo hatakuwepo wa kusema mimi nilifanya hivi ama nilipenda iwe hivi, ila ni maafa tu.
 
Asante muanzishaji mada.

Nao hao nao ni WaTz, hivyo wana haki ya kutoa maoni yao kama vile mimi na wewe. Ila swali kubwa ni nini hasa nia yao? Kwa nini sasa? Kwa manufaa ya nani?

We need an unadulterated Constitution. Not an Appeassing Constitution. We should be clear and objective in this....not to take whatever is given in any form as "new" constittion when it isn't. I seriously doubt both political willingness and political mechanism in place so to arrive where Tz must be. The road ahead is so tricky, tough and narrow. It demands guts, sweats and sacrifices. Mark my words.
 
Watu wenye mapenzi mema wametumia dalili za mvua vya mwaka huu kutoa angalizo la miaka mitano ijayo. Janga kuu liko njiani kutokea kwa takwimu sahihi kabisa. Mfano; ongezeko la wapiga kura toka milioni 9 mwaka 2005 hadi milioni 20 mwaka 2010, limesababisha hali ya sintofahamu maeneo mengi nchini. Miaka mitano ijayo kuna uwezekano wa wapiga kura walioandikishwa kufikia milioni 30 (La msingi hapa kijana wa darasa la sita mwaka huu umri miaka 13, ni mpiga kura 2015). Kama wale ambao miaka 20 iliyopita hawakuwa na umri wa utu uzima wameonesha changamoto kubwa ya kudai mabadiliko 2010, hali itakuwaje 2015?

Kama tunalihitaji taifa huru lenye amani, tufikirie mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa nchi, kinyume cha hapo hatakuwepo wa kusema mimi nilifanya hivi ama nilipenda iwe hivi, ila ni maafa tu.

Mundali, nadhani unaongelea watu waliojiandikisha kupiga kura tu. Ndio, walikuwa milioni ishirini. Lakini watu waliojitokeza kupiga kura ni takribani milioni 8... (Unaweza ukajadili zile sababu kama majina ya watu kukosekana kwenye madaftari ya wapiga kura; lakini haifiki milioni 10!)
 
naona watu mnashindwa kupata pointi yenyewe na kama kawaida mnaanza kuuliza kama niko bado na akili zangu timamu. Mnapenda mno mazingaombwe kiasi cha kushangilia mkiona sungura katolewa kwenye kofia na wengine wanaweza kuapa kabisa kuwa ni "muujiza". Sasa leo watu wanaanza kuimba "katiba mpya" basi watu wanatakiwa kushangilia:

Hawawaambii tatizo la Katiba ya sasa ni nini? - of course tunatakiwa tuwe tunajua sote
Hawasemi kwanini sasa hivi na haikuwa kabla- tunaambiwa ni muda tu
Hawasemi wanataka nini hasa - yale yale "katiba mpya" - upya wa nini?
Hawasemi ni vitu gani viboreshwe? Je wakibadilisha tu Tume ya Uchaguzi watu wataridhika? Kwanini isiwe kufanyia mabadiliko vipengele vinavyolalamikiwa halafu tukamaliza kwani hilo halihitaji siku nyingi hata kikao cha bunge kinaweza kufanya hivyo.
Ati Katiba iliyopita haikuandikwa na sisi - well kwani kuandika sisi wenyewe kunatuhakikishia vipi Katiba nzuri? Leo hii miaka 49 ya kujitawala mbona baadhi yetu hatujivunii kuoona tunavyojitawala? kwanini tuamini ati kwa vile tutaandika Katiba sisi wenyewe basi itakuwa nzuri? Jamani, kwani vyama vingine vilirudishwa vipi na leo watu hawafurahii wakati tulishirikishwa kuvirudisha?

Katiba Mpya? kwa manufaa ya nani? Siyo wote wanaosema "nyeupe" wanamaanisha "nyeupe pe" wengine wanamaanisha "rangi ya maziwa!"

Nikubaliane na wewe hasa kwenye QUOTE. Wapo wanaosubiri mchakato uanze ili ndoto za mahitaji yao ziweze kutimizwa. kuna wale wanaohitaji Mahamaka ya kadhi na suala la OIC liingizwe kwenye katiba mpya. Kuna mafisadi watapressurize masilahi yao au katiba iwe na mianya ya wao kuendelea kuhujumu na kuna wale wenye nia nzuri wanaoitakia mema nchi yetu nao watapigania cake yao iweze kuonekana kwenye katiba mpya. Kama agenda ya katiba mpya itakubaliwa basi tutegemee kuona vionja vingi vikitokea.
 
Busara za CHADEMA zimesaidia otherwise yangetukuta ya Ivory Coast
 
Mzee Mwanakijiji,

Kwa muda kama wa wiki mbili hivi nimekuwa nikifikiria sana hili suala la katiba mpya; kila nikitaka kuandika nakosa muda shauri ya kutingwa na mambo mengine. Nimekuwa nikijiuliza katiba mpya itawasaidia nini Watanzania mbalimbali wale wanaosumbuka kila siku kwa umaskini na magonjwa? Je kweli tatizo la Tanzania ni ukosefu wa katiba mpya au tuna matatizo mengine makubwa sana?

Kama nchi tuna sheria mbalimbali ambazo zimetungwa kupitia bunge. Katika sheria hizi zipo nyingi tu ambazo ni nzuri sana lakini je zimetusaidia nini sisi kama Watanzania? Kwanini tumeshindwa kuzitekeleza kwa vitendo? Kwanini tunaendelea kuwa maskini na wajinga wa kutupwa pamoja na juhudi za watu mbalimbali kujaribu kusaidia?

Mfano kuna sheria mbalimbali za rushwa ambazo hazifanyi kazi. Kuna sheria ya gharama za uchaguzi ambayo baadhi ya sisi tulioshiriki siasa za 2010 tuliona ingefaa lakini tukashuhudia hao hao walioitunga wakivua nguo zao na kuivunja bila hata aibu. Je tuna uhakika gani hiyo katiba mpya haitavunjwa hivyo hivyo?

Binafsi naamini katiba mpya sio suluhisho na wala haitatusaidia. Tupiganie elimu na uchumi bora kwani ndio vitu pekee ambavyo vitamfanya Mtanzania ajikomboe na kuwa huru hata kuona katiba aliyo nayo haimfai. Kwasasa ni wasomi wachache na wanasiasa ambao wanaona umuhimu wa katiba mpya lakini watu wetu wengi wako busy kuhangaika na watakula nini? Watatibiwa wapi? na watapeleka watoto wao wapi kusoma? Watu kama hao hata wakipata katiba nzuri sidhani kama wako katika nafasi ya kuilinda na kuhakikisha inafuatwa.

Ni sawa na uhuru, watu wengi walianza kudai uhuru miaka mingi sana nyuma lakini sio wote walioelewa umuhimu wa uhuru mpaka miaka ya 60 na matokeo yake wananchi wengi walikuwa tayari kuutetea na kuulinda uhuru wao huo. Hivyo hivyo vyama vingi kwa Tanzania.

Kwa Tanzania, uchaguzi wa mwaka huu umeonyesha wazi wananchi wamechoshwa na uchumi duni na siasa za ubabaishaji. Wanataka mabadiliko katika maisha yao. Wanataka chakula nyumbani, wanataka hospitali, wanataka shule. Labda ni muda muafaka kuleta uhuru wa kiuchumi kwa wananchi wetu kabla hata ya kuleta katiba mpya. Labda tupiganie haki ya wananchi wetu kushiriki kwenye uchumi wao, kuhakikisha ajira zinatolewa kwa Watanzania. Kama hayo mambo hayawezi kufanyika mpaka tuwe na katiba mpya basi labda kuna haja ya hiyo katiba mpya. lakini kwa mimi naona leo hii hata tuletewe katiba iliyoandikwa vizuri namna gani, kama hatuna watu wengi ambao wako tayari kuitetea na kuilinda bado tutaendelea kukwama pale pale.
 
This is complete absurd and immoral. Why cant you give other people their due respect even if you hate them??? Is this what your religion teaches you?? Keep on hating a person but remember to put away from you all immoral anguish and respect others and their work

Respect? Adulterer? What nonsense! And you have voted for him to be a leader? Go and your bible and see what is penalty of an adulterer! And you want us to respect him? My religion teaches me whip an adulterer, do you know what your religion teaches on adultery? If you do, please let us know. Unless he repent and regrets on his mistake he is not to be left alone.
 
Upupu mtupu, anataka kujifanya kana wazo la katiba mpya ni lake! Hakumbuki kuwa miaka michache ya nyuma lilishaundiwa tume chini ya uongozi wa ccm? Nawe pia hukumbuki?

Msitake kujidai ni wazo lenu. Na muelewe, hiyo katiba iliyopo imesharekebishwa mara ngapi? Chini ya uongozi wa ccm. Katiba si msahafu itakwenda ikibadilika, kuundwa mpya, kurekebishwa, kuongezwa, kupunguzwa maisha yote.

Mimi nawashangaa mnaojifanya kuwa mnashinikiza wakati mnajuwa wazi kuwa katiba mpya ni kwa maslahi ya Tanzania, no matter ni wa chama kipi! CCM chini ya Kikwete itahakikisha inafanya mabadiliko ya Katiba ua japo kuanzisha tu mabadiliko ya Katiba. Hicho ni kitu ambacho si siri wala hakina ubishi. Naona ni wabunge wenu tu ndio wazembe kwa kutopeleka mswada siku zote walizokuwa bungeni.

Haya fanyeni hima, pelekeni mswada bungeni, tupate katiba mpya. Sio kupayuka tu hapa JF.

short sighted person!
 
Back
Top Bottom