Kwanza, kama baadhi ya wenzangu walivyosema, binadamu kubadili msimamo ni sifa ya all objective people. Siyo kushikilia msimamo hata pale umepata ufahamu mpya tofauti na ulivyofikiri mwanzo.
Pili, mkapa na JMkuu ni objective persons, hivyo wamefanya sawa.
Tatu, huu uchakachuaji wa 2010 haukupa sifa kutoka jamii za kimataifa kama ule wa chaguzi zilizopita. Jamii za kimataifa zilijua mapungufu haya yote lakini zilichagua kusifia chaguzi kwa sababu zao binafsi. Sasa hili lina athari kwa serikali yetu ombaomba. Serkali inayoamini kwamba rasilimali zetu tuwakabidhi wazungu kisha tuwaombe msaada.
Nne, propaganda zilizoenezwa awali kwamba upinzani ni vita, mauaji, uasi, uchu wa madaraka, siyo uzalendo, ni kupinga maendeleo, yote sasa yameonekana ni uongo. Ushahidi umepatikana kwamba kinyume cha hizo propaganda ndiyo uhalisi wa chama tawala. Wanadhulumu wananchi, wanamwaga damu, wanapora wananchi ardhi yao, wanafisadi mali na pesa za umma, na wana uchu wamadaraka. Hivyo, upinzani umekua kwa hoja na idadi ya wanachama wanaothubutu na kwamba katiba ya leo inaweza kupelekea umwagaji wa damu. Mifano ilikuwa Nyamagana, arusha mjini, ubungo, kawe, n.k.
Hii ina maana kwamba viongozi wakuu wa ccm walioanza kudai katiba mpya ni mkakati wa ccm kutidhatiti kwa chaguzi zijazo, lakini wanaamua kupitia kwa mkapa na JMkuu ili mwanzoni mwa 2011 ccm iseme ni mchakato ulioanzia kwao, kama walivyodai kuhusu ufisadi. Ikiwa hivyo upinzani utabweteka na kuona wamefaulu. Lakini Nia ya ccm ni kuandika katiba mpya itakayodhibiti changamoto walizopambana nazo tangu 2006. Tukumbuke kwamba ccm ndiyo yenye wabunge wengi bungeni na katiba hupitishwa kwa kura siyo sauti zilizoafiki.