Sidhani kama Diamond Platnumz anamsaidia Marioo

Sidhani kama Diamond Platnumz anamsaidia Marioo

Mtuflani Official

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2019
Posts
1,952
Reaction score
4,416
Nimeona picha huko Instagram Marioo akiwa na Diamond Platnumz huko Nigeria.

Wengi wetu tunaamini Platnumz anamsaidia Marioo kumpeleka international ila mi naona kama anamharibia.

Kitachotokea ni Marioo sasa kuanza kuimba kama Wanigeria kitu ambacho kitamuharibia. Atapoteza identity ya muziki anaofanya kama tulivyomzoea na kumpenda.

Diamond siku hizi amekuwa ni mtu wakuimba na beat za Nigeria kitu ambacho mimi binafsi kinanichukiza sana. Amepoteza kabisa identity na ndo maana ni vigumu yeye kupata tuzo siku hizi.

Huwezi kupata tuzo kwa mfano ya “Best East African” artist wakati unaimba kama Wanigeria.

IMG_4170.JPG
 
Navyojua nyimbo ambazo zimempa diamond coverage na tuzo ni zile alizoimba kinaija (Afro beatz). Kuhusu Marioo sidhani kama kuna ubaya maana dogo kapewa nomination na akipata association na brand kubwa kama Diamond nadhani atafika mbali kwa wepesi zaidi.
 
Wabongo majungu sana asingeenda naye pia mngesema hasaidii wenzake.
Kweli bongo bahati mbaya.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Mkuu acha tu, Diamond amefanya move nzuri. Lango la WCB saa hii lipo wazi maana hakuna main act mwingine pale na kama akimkuza marioo, itampa faida zaidi maana tayari ana jina na pia ni talented.
 
Navyojua nyimbo ambazo zimempa diamond coverage na tuzo ni zile alizoimba kinaija (Afro beatz). Kuhusu Marioo sidhani kama kuna ubaya maana dogo kapewa nomination na akipata association na brand kubwa kama Diamond nadhani atafika mbali kwa wepesi zaidi.
Yes ni Afro beatz hakuna 9ja music identity hata Ghanaians wanasema hiyo style ni yao.
 
Mtuflani Official,

View attachment 1325893[/QUOTE]
Umesema unachukizwa wewe binafsi, sasa hayo ni mawazo yako!
Usidhani wengine wote wanaomkubali wanachukizwa, kati ya watu 100,000 pengine ni wewe tu mwenye maoni kama haya uliyotoa!
...unadhani pengine wale waliompa show kwenye caf awards waliona nini kwake?
...lakini pia kama unachukizwa anavyoimba hujalazimishwa kusikiliza nyimbo zake, ukizisikia weka pamba kwenye masikio au zima huo mziki, au sikiliza hao wabana pua kila saa wanasema yooh, sijui yeeh mama!!





Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom