Sielewi kwanini mtu aliyechakachua msaada wa serikali na kujimilikisha enzi za Kikwete, akaondolewa leo anateuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa

Nikujibu kwa kifupi mkuu 'Philipo Bukililo'.

Mimi sioni 'strategy' (mkakati) wowote katika teuzi hizi.

Kama ni kumfurahisha Kikwete ndiyo 'strategy', basi hapo nitakuwa nimepoteza dira katika uoni wangu.

Mimi nadhani sasa inaonekana mama anajipigia tu, mradi liende, na siku zisonge.
 
Tatizo kubwa la watanzania ni UBINAFSI, nchi hii ina watu wana hali ngumu sana kiuchumi na wengine ni wazee sana na hawana msaada.

Viongozi wengi kazi yao kubwa in kulipana posho za vikao na marupurupu mengine hivyo wapo tayari kujipendekeza, kuua, kuroga na hata kuhonga ili wapate madaraka au waendelee kuwa kwenye madaraka.

Kuna Watanzania wenzetu ni maskini wa kutupwa.
 
Kulikua na ulazima wa kutuletea MTU kama Batilda Buriani kweli??

Au mkuu wa mkoa wa Dar??

Hii recycling ya viongozi wale wale Kila awamu mpaka lini

Watuweke wazi tu kuwa kuna Tabaka la watawala na watawaliwa.
 
Nadhani hata kazini kwako wanapata tabu sana na wewe. " majungu, majungu, majungu tu na wivu".

Post yako hii imekaa kimajungu
Ufupi wa mawazo yako unajidhihirisha wazi. Kazini kwangu wananijua wakitaka kufanya ujinga wafanye mie sipo. Kuwasema watu waliochakachua mali ya serikali ni majungu, kwamba tuache tu kwa kuwa wao walipata fursa? Kwa hiyo wewe ukiona mtu anahujumu mali za serikali utakaa kimya kwa kuwa kumsema ni kuleta majungu? Hujakaa vizuri kichwani.
 
Kurudisha team JK sio tatizo, hata akitaka achanganye na team Mkapa. Suala ni kwamba, kwa nini urudishe watu wenye madoa yasiyofutika? Kwa nini usiibue watu wako wapya na na awamu nyingine zije zichukue team yako?
 

..salama yetu inatakiwa iwe kwenye KATIBA.

..vilevile tuwe na bunge lenye utashi wa kuisimamia serikali.
 
Kurudisha team JK sio tatizo, hata akitaka achanganye na team Mkapa. Suala ni kwamba, kwa nini urudishe watu wenye madoa yasiyofutika? Kwa nini usiibue watu wako wapya na na awamu nyingine zije zichukue team yako?
Hakujiandaa na jukumu la urais akitegemea atabakia na umakamu mpaka 2025. Ni mipango ya Mungu kifo, hivyo naamini amefanya kazi ngumu baada ya kifo cha JPM ili apate watu sahihi.

Na ni kwa kigezo hicho cha kifo cha rais, mzee Kikwete ndipo anapoingia kazini kumsaidia ili mambo yaende. Miradi imalizike kwa wakati huku nchi ikibakia imara pasipo kutetereka.
 
Mkuu umeongea point sana. Nakumbuka teuzi za JK zilivyokuwa na ukakasi mara nyingine kwa kuwa zilikuwa ni teuzi za Mama na Mwana. Hawa kina Makonda walianzia mgogongozi mwa Ridhiwani - baba mteue huyu Mkuu wa Wilaya, ameniomba sana. Honey huyo mtoto wa ndugu yanug amemaliza Masters degree mpe ukurugenzi pale Wizara ya Elimu!
 
Yupo kiongozi mmoja wa Yanga alibembelezwa cheo lakini akakataa, ni ndugu yake JK ni mwanasheria maarufu.
 
" jina lake nani, au baba yake nani" kama ni underground, kwa heli!!!
Watu wa vetting ndio chanzo cha haya
 
Kama sio majungu kwanini usimtaje sasa
 
Taja jina la huyo mtuhumiwa.vingenevyo nyamaza.
 
Kwa hiyo kwa upande wako nyakati zimebaki vilevile, hakuna kilichobadilika toka wakati huo wakati huu, kiasi kwamba yaliyovumiliwa wakati ule ndiyo yavumiliwe wakati huu?
nyakati zimebadilika, ila huyo unknown is known na ni maarufu pande za arusha, sasa watu bado wanalazimisha mtoa mada amtaje...
 
JF is the place "WHERE WE DARE TO TALK OPENLY".

Sema ni nani huyo na alichakachua msaada gani na kwa sasa ni RC mkoa upi...?

Don't hide anything because there's no reason to do so....
 
" jina lake nani, au baba yake nani" kama ni underground, kwa heli!!!
Watu wa vetting ndio chanzo cha haya
Hii habari ya "vetting", nadhani tunaaminishwa kitu kisichokuwepo; na kama kipo, basi hicho ni kifaa kisichokuwa na manufaa yoyote, bali kina hasara kubwa kwa taifa.
 
nyakati zimebadilika, ila huyo unknown is known na ni maarufu pande za arusha, sasa watu bado wanalazimisha mtoa mada amtaje...
Maarufu pande za Arusha huku ni Gidbless Lema tu, wengine HAPANA hakuna kitu....SIYO MAARUFU...

Amtaje au mtaje wewe kwa kuwa umeshamjua. Wengine sure kabisa, bado hatumjui...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…