Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Imekuwa ni mtindo wa kawaida kabisa hivi sasa, katika Kila mkutano wa hadhara anayoifanya Rais Samia, wateule wake wanampa sifa nyingi, ambazo nyingine hazimstahili.
Huwa najiuliza, katika miradi mingi ya maendeleo huko mikoani, sifa zote anapewa Rais Samia na kitu ambacho naamini hakiko sawa ni hao wateule kumshukuru Rais kuwa ndiye aliyetoa pesa za miradi hiyo, utadhani kuwa Rais Samia, anazitoa mifukoni mwake!
Hivi kama hao wateule wanampa sifa hizo za kutoa pesa za miradi, huwa najiuliza, hivi vile vikao vya Bunge, vinavyoketi Kwa kipindi kirefu Kila mwaka, Ili kupitisha bajeti za wizara mbalimbali, huwa inakuwa ni kiini macho, iwapo pesa zote anazitoa Rais, pale anapojisikia??
Najua hicho wanachofanya hao wateule wa Rais, ni mkakati ambao wamekubaliana kama chama, katika vikao vyao.
Sasa niwaeleze hao wateule wa Rais, kuwa hicho mnachokifanya kina ",impact" mbaya sana Kwa siku zijazo.
Kwa kuwa huo mchezo mnaoucheza, Kwa mawazo yenu, mkidhani mnafanya vyema katika kukiimarisha chama chenu na mkidhani hiyo ndiyo njia Bora nzuri ya kutafuta kura Kwa mwaka ujao wa uchaguzi.
Hivi hao wapiga kura mnaowapiga "fix" kuwa Fedha zote ametoa Mama kutoka "mifukoni" mwake, watakapowauliza, pale mtakapokuja kwao kuomba kura Katika uchaguzi Mkuu huku mkijieleza kuwa mnaomba kura zao Kwa kutoa orodha ya miradi, ambayo mtadai kuwa mmetekeleza nyinyi, swali litakalowarudia, ni Kwa vipi nyinyi wabunge mdai kuwa miradi hiyo mmetekeleza nyiye, wakati majuzi tu mlitamka kuwa miradi hiyo ameikamilisha Rais Samia, baada ya kumshukuru yeye, kama vile pesa hizo anazitoa toka "mifukoni" mwake?😚
Jambo lingine ambalo nadhani linafanywa Kwa kuvunja sheria ni Kwa huyo Mkuu wa nchi kufanya ziara hizo, ikionekana wazi kuwa kaanza kampeni ya uchaguzi Mkuu wa mwakani, mapema kabla "kipyenga" hakijapulizwa
Tunaonba Tume ya uchaguzi, imkemee Rais na kumwambia kuwa, Kwa mujibu wa ratiba yao Tume ya uchaguzi, muda wa kuanza kampeni bado kuanza na inategemewa kuanza mwakani 2025
Vile vile katika ziara hizo, yanatumika mabilioni ya pesa, ambazo ni pesa zetu walipa Kodi, mathalani ni hizo ziara "kukusanya" karibu mawaziri wote wa JMT, Kwenye misafara ya magari yasiyopungua 100, ambayo ni matumizi mabaya kabisa ya pesa ya Umma
Yaani Kwa tafsiri nyingine, ni kama hizo wizara zimeajiri "watoro" makazimi mwao😚
Mungu ibariki Tanzania