Sifa za kujiunga Chuo Kikuu

we ushasikia serikali imechoka? Imesema wapi? Au wewe ndo msemaji wake?
Ingekua inachukua wanaostahili tuu ,hata isingewakopesha bali ingewasomesha kama zamani
 
Ili Tanzania ipate wanafunzi bora wataoweza isaidia nchi Kiuchumi, Kiteknolojia, Kibunifu, haina budi kuacha siasa kwenye elimu.

Serikali ijiwekee malengo, itengeneze walimu bora kabla ya kuanza sumbuka na wanafunzi bora, ni walimu pekee ndo wataweza isaidia Tanzania kufanikiwa au kutofanikiwa.
Huwezi chukua watu waliofeli na kuwapa wafundishe wanafunzi, watawafundisha kilicho kwenye kitabu tu, hawatataka utofauti, na ndio maana ukiandika utofauti na ulichofundishwa darasani, unakoseshwa

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Binafsi nilipata E somo moja, na huenda ingekuwa mbaya nikaangukia huko kwenye F. Sema kingine matokeo ya mwisho huenda yasimaanishe uwezo wa mtu. Huenda ukafanya vizuri miaka yote ukiwa shuleni ukaja ukazingua kwenye mtihani, na dunia ikakujadili kwa kile ulichokionesha mwishoni. Sema yote kwa yote huwa kuna vitengo vyangu ambavyo navionea. Chuoni na hata kazini vimenipa credit sana. Na kama ni Masters nitaenda piga kuhusu vitu ninavyovipenda. Serikali kupitia TCU imeona hayo madaraja yanafaa ndio maana wameyaacha. Wewe mwenye madaraja makubwa labda utuchambulie kwa kina, tuandikie proposal:
  • Nini kifanyike zaidi yasipatikane
  • Maono yako kwa nini madaraja ya juu tu
  • Hao wa madaraja mengine wapelekwe wapi
  • Hiyo itasaidia nini
  • n.k... wewe ni jembe utatuletea kitu cream
 
Pepa likikutaa basi utaangukia D kama sio E ila sio F, kupata F maana yake hilo somo hukulielewa kabisa, kwahiyo hao watu inabidi waoende level ya chini kuanzia Diploma ili wapikwe vuzuri kisha wakienda chuo kikuu wanakua competent
 
Ajira hakuna wewe unalalamika watu kuwa na DDF ,hayawani wewe,badala ya kusema kwa kuwa hakuna ajira serikali iwasomeshe bure watoto wetu na ufaulu wa kumwezesha mtu kuwa chuo kikuu uwe EEE. Weee waleta mbambamba!!?
 
Upate F ya chemistry halafu unaenda somea Nursing, au F ya hesabu unaenda somea engineering unatakiwa urudi chini utakaswe kigezo cha kukupeleka chuo kikuu kiwe diplom a sio form 6 tena
 
Ajira hakuna wewe unalalamika watu kuwa na DDF ,hayawani wewe,badala ya kusema kwa kuwa hakuna ajira serikali iwasomeshe bure watoto wetu na ufaulu wa kumwezesha mtu kuwa chuo kikuu uwe EEE. Weee waleta mbambamba!!?
Ili iongeze wasomi uchwara wa EEE
 
Mwenye AAA ameweka historia ametumia nafasi yake vizuri hajachezea fursa ni role model. Tusichanganye mambo tusichanganye mambo ya maisha na shule.
Na utakuta akiumwa hapo anaulizia ni hospitali gani wanatibu vizuri( hao ma Dr sio wa F)

Atauliza ni shule gani nzuri apeleke mwanae( walimu wa hiyo shule atakuta sio wa F)

Akipata tatizo atatafuta mwanasheria mzuri ( sio wa F)

Hayo ndio mafanikio ya wasipata F, sio utajiri nk kama anavyodhani
 
Yaani wewe unashangaa D2 wakati awali ilikuwa E2? Hivi wewe umesoma mwaka gani hata usijuwe hilo? Kuna EE wapo makazini na ni mainjinia, Madaktari halafu unajifanya kushangaa leo?

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Kigezo cha ufaulu mkubwa sio kipimo cha umahiri pekee. Kinachoangaliwa ni ujuzi ambao mwanafunzi au mwanachuo kaupata au ataupata kwa mujibu wa malengo ya mtaala.
 
Kigezo cha ufaulu mkubwa sio kipimo cha umahiri pekee. Kinachoangaliwa ni ujuzi ambao mwanafunzi au mwanachuo kaupata au ataupata kwa mujibu wa malengo ya mtaala.
Sasa mtu kupata F kuna umahiri gani kapata
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…