Sifa za kujiunga Chuo Kikuu

Sifa za kujiunga Chuo Kikuu

Ili Tanzania ipate wanafunzi bora wataoweza isaidia nchi Kiuchumi, Kiteknolojia, Kibunifu, haina budi kuacha siasa kwenye elimu.

Serikali ijiwekee malengo, itengeneze walimu bora kabla ya kuanza sumbuka na wanafunzi bora, ni walimu pekee ndo wataweza isaidia Tanzania kufanikiwa au kutofanikiwa.
Huwezi chukua watu waliofeli na kuwapa wafundishe wanafunzi, watawafundisha kilicho kwenye kitabu tu, hawatataka utofauti, na ndio maana ukiandika utofauti na ulichofundishwa darasani, unakoseshwa

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Binafsi nilipata E somo moja, na huenda ingekuwa mbaya nikaangukia huko kwenye F. Sema kingine matokeo ya mwisho huenda yasimaanishe uwezo wa mtu. Huenda ukafanya vizuri miaka yote ukiwa shuleni ukaja ukazingua kwenye mtihani, na dunia ikakujadili kwa kile ulichokionesha mwishoni. Sema yote kwa yote huwa kuna vitengo vyangu ambavyo navionea. Chuoni na hata kazini vimenipa credit sana. Na kama ni Masters nitaenda piga kuhusu vitu ninavyovipenda. Serikali kupitia TCU imeona hayo madaraja yanafaa ndio maana wameyaacha. Wewe mwenye madaraja makubwa labda utuchambulie kwa kina, tuandikie proposal:
  • Nini kifanyike zaidi yasipatikane
  • Maono yako kwa nini madaraja ya juu tu
  • Hao wa madaraja mengine wapelekwe wapi
  • Hiyo itasaidia nini
  • n.k... wewe ni jembe utatuletea kitu cream
 
Pepa likikutaa basi utaangukia D kama sio E ila sio F, kupata F maana yake hilo somo hukulielewa kabisa, kwahiyo hao watu inabidi waoende level ya chini kuanzia Diploma ili wapikwe vuzuri kisha wakienda chuo kikuu wanakua competent
 
Ajira hakuna wewe unalalamika watu kuwa na DDF ,hayawani wewe,badala ya kusema kwa kuwa hakuna ajira serikali iwasomeshe bure watoto wetu na ufaulu wa kumwezesha mtu kuwa chuo kikuu uwe EEE. Weee waleta mbambamba!!?
 
Upate F ya chemistry halafu unaenda somea Nursing, au F ya hesabu unaenda somea engineering unatakiwa urudi chini utakaswe kigezo cha kukupeleka chuo kikuu kiwe diplom a sio form 6 tena
 
Ajira hakuna wewe unalalamika watu kuwa na DDF ,hayawani wewe,badala ya kusema kwa kuwa hakuna ajira serikali iwasomeshe bure watoto wetu na ufaulu wa kumwezesha mtu kuwa chuo kikuu uwe EEE. Weee waleta mbambamba!!?
Ili iongeze wasomi uchwara wa EEE
 
Mwenye AAA ameweka historia ametumia nafasi yake vizuri hajachezea fursa ni role model. Tusichanganye mambo tusichanganye mambo ya maisha na shule.
Na utakuta akiumwa hapo anaulizia ni hospitali gani wanatibu vizuri( hao ma Dr sio wa F)

Atauliza ni shule gani nzuri apeleke mwanae( walimu wa hiyo shule atakuta sio wa F)

Akipata tatizo atatafuta mwanasheria mzuri ( sio wa F)

Hayo ndio mafanikio ya wasipata F, sio utajiri nk kama anavyodhani
 
Nimeshangaa katika pitapita zangu nimeona cheti cha mtu cha Advance katika masomo 3 ya combination ana DDF, halafu yupo chuo kikuu anasoma degree.

Serikali ifute kigezo cha D mbili, ama katika hizo D mbili iwepo na sifa nyingine kwamba hupaswi kuwa na F kwenye somo lolote kati ya masomo matatu. Yani hata ikitokea AAF hupaswi kwenda chuo kikuu.

Ni aibu kati ya masomo matatu una F moja halafu upo chuo kikuu unasoma degree.

Kingine ni kuhusu wanaorudia mitihani form iv na vi, hawa nao kwasababu vitu walivyovisoma ndani ya muda uliopangwa wakafeli kwenye assesment, inabidi grade zao za alama ziwe juu kuliko freshers maana wao walishavisoma hivo vitu wakafeli ndani ya scale ya awali.

Nawasilisha.
Yaani wewe unashangaa D2 wakati awali ilikuwa E2? Hivi wewe umesoma mwaka gani hata usijuwe hilo? Kuna EE wapo makazini na ni mainjinia, Madaktari halafu unajifanya kushangaa leo?

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Sina
Vigezo vipandishwe ili chuo kikuu waende watu wenye umahiri mzuri na kipimo ni mitihani ya form 6 ili tusijaze wasomi wengi wa chuo kikuu ambao hawana umahiri kwa kupata F za form 6

Kupunguza kundi kubwa la watu chuo kikuu ambao hawakustahili kuwa hapo kwa uwezo wao, wapite diploma kwanza wakajitakase huko ndio wapande chuo kikuu ila nako huko GPA ya kupanda chuo ianzie 3.5
Kigezo cha ufaulu mkubwa sio kipimo cha umahiri pekee. Kinachoangaliwa ni ujuzi ambao mwanafunzi au mwanachuo kaupata au ataupata kwa mujibu wa malengo ya mtaala.
 
Kigezo cha ufaulu mkubwa sio kipimo cha umahiri pekee. Kinachoangaliwa ni ujuzi ambao mwanafunzi au mwanachuo kaupata au ataupata kwa mujibu wa malengo ya mtaala.
Sasa mtu kupata F kuna umahiri gani kapata
 
Back
Top Bottom