Sifurahishwi na kiwango cha Aziz Ki kwa sasa

Sifurahishwi na kiwango cha Aziz Ki kwa sasa

Kamgomoli

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2018
Posts
1,896
Reaction score
4,058
Jana kwenye mechi kati ya KMC na Yanga nimemshuhudia Aziz Ki akionesha kiwango kibovu kabisa. Ni kweli inawezekana jana alikuwa na siku mbaya kazini lakini Aziz ana matatizo yanayojirudia rudia, ambayo ni kupokonywa mpira kirahisi,kupiga pasi mkaa na kukosa magoli ya wazi tena akiwa karibu kabisa na goli.

Kwa "profile" yake sitarajii kumuona akifanya makosa ya kizembe km hayo. Kama namba 10 unapoteza mpira mara kwa mara ni dhahiri namba 9 atakosa hudumu. Ndicho kilichomkuta Clement Mzize jana. Kiwango cha Aziz kimekosa kabisa mwendelezo na lazima ashituke. Amebaki kuwa mchezaji wa "moment" na sio "Whole Match."

Namuona Aziz akiungana na kina Ambundo,Zawadi,Gushi,Tuisila na Bryson kwenye kundi la wachezaji wenye kiwango kibovu pale Yanga.

Kinachonishangaza si mashabiki wa Yanga wala wachambuzi wanaoongelea kiwango kibovu cha Aziz anachokionyesha sasa tofauti na wanavyowasema kina Ambundo.
 
Jana kwenye mechi kati ya KMC na Yanga nimemshuhudia Aziz Ki akionyesha kiwango kibovu kabisa. Ni kweli inawezekana jana alikuwa na siku mbaya kazini...

Master Ki ni talented usitegemee kiwango kudrop najana kila mchezaji alikuwa akicheza kwa tahadhari alimradi asiumie..

Jumapili utamuona Master Ki mwenyewe kule Mali
 
Jana kwenye mechi kati ya KMC na Yanga nimemshuhudia Aziz Ki akionyesha kiwango kibovu kabisa. Ni kweli inawezekana jana alikuwa na siku mbaya kazini...
Kweli ameshuka kiwango aisee, si kwa kupoteza mipira na nafasi vile. Ila jana timu yote ilikuwa ovyo ukiacha Diarra, Nondo na Bacca the rest walikuwa wanatukaruka tu.
 
Jana kwenye mechi kati ya KMC na Yanga nimemshuhudia Aziz Ki akionyesha kiwango kibovu kabisa. Ni kweli inawezekana jana alikuwa na siku mbaya kazini lakini Aziz...
Nimeshangazwa pia, chama pamoja na kazi kubwa anayofanya bado wanasema ameshuka kiwango ila huyo kiyande anaruka ruka tu hapo utopoloni na wamekaa kimya..
 
Aziz K anaweza akapotea Kwa gemu mbili tatu ila yeye yupo kwenye daraja la pekee. Akiwa kwenye daraja lake unaona kabisa uyu Kwa umri wake Kuja kucheza uku kwetu ni jambo la kushangaza!!.
 
Aziz K anaweza akapotea Kwa gemu mbili tatu ila yeye yupo kwenye daraja la pekee. Akiwa kwenye daraja lake unaona kabisa uyu Kwa umri wake Kuja kucheza uku kwetu ni jambo la kushangaza!!.
Kwenye game gani alikuwa kwenye daraja lake, kiasi kikakushangaza kuja kucheza soka Tanzania?
 
Huyo unayemsema bado yupo kwenye majeraha ya mguu,pia kushuka kwa kiwango cha mchezaji ni jambo la kawaida Sana katika mpira.
 
Tatizo la Azizi K ni kutumia mguu moja tu wa kushoto, kwa namba anyocheza (10) ni ngumu sana kuonyesha kiwango cha juu. Mimi ni mpenzi wa Yanga ila kwa kweli sijavutiwa sana na huyu mchezaji.
😅😅😅 Asee ko chama anatumia miguu 6?, Messi anatumia miguu 10?.
 
Mtazamo wangu kuhusu viwango vya wachezaji mbalimbali wa Simba ikiwemo hao uliowataja unajulikana wazi. Tofauti ya Aziz na Sawadogo ni foul za kudunda tu na kukunja bukta.
Unga ni kitu kibaya Sana... Ona unavyotapika upuuzi.
 
Back
Top Bottom