Sigara "Clipper" aliyokuwa akivuta Mwalimu Nyerere miaka ya 1950's

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
SIGARA "CLIPPER" ALIYOKUWA AKIVUTA MWALIMU NYERERE
Picha hiyo hapo chini imepigwa mwaka wa 1955 Magomeni Mapipa Mtaa wa Jaribu kwenye Tawi la TANU alilofungua Ali Msham nyumbani kwake.

Ali Msham ni huyo upande wa kulia aliyekuwa katika ya vijana wawili wamepiga lubega za kaniki mmoja ana shoka begani.

Hawa walikuwa Bantu Group wahamasishaji umma na walinzi wa viongozi wa TANU.

Waliokaa kulia ni Zuberi Mtemvu, Julius Nyerere na John Rupia.

Ukimwangalia Nyerere utaona ameshika paketi ya sigara na ana sigara mkononi.

Mwalimu katika ujana wake alivuta sigara na sigara yake ilikuwa "Clipper," sigara maarufu enzi hizo. Paketi yake ni hiyo hapo juu.

Mwalimu aliacha kuvuta mwaka wa 1962 baada ya kifo cha rafiki yake kipenzi Hamza Mwapachu kufariki kwa maradhi ya moyo yaliyosababishwa na uvutaji sigara.




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumbe mwalim nae alikua anatumia mmea
Uvutaji wa sigara na kiko vilikuwa ni fasheni kwa miaka ya hamsini, sitini, na sabini kabla madhara ya tumbaku hayajajulikana. Sehemu kubwa ya vijana wa miaka hiyo walikuwa wanavuta sigara sana tena hadharani tu, hata mbele za watu wengine.


John F Kennedy: Rais wa Marekani Enzi hizo

Nelson Mandela: Rais wa kwanza Mwafrika wa Afrika ya kusini enzi za ujana wake

Winston Churchill: Waziri Mkuu wa Uingereza enzi hizo.


Ronald Reagan: Rais wa Marekan enzi za Ujana wake


Fidel Castro: Rais wa Cuba enzi za ujana wake



Leopold Senghor: Rais wa Senegal enzi za ujana wake



Nafikiri unamjua huyo

Hakuna mtu wa karne hii asiyemjua mtu huyu

Hapo ni General Yitzhak Rabin na General Ariel Shalon wakiwa katika maandaliaiz ya vita ya siku sita iliyofuta majeshi yote ya Misri, Syria na Jordan kwa siku sita tu. Wote Rabin na Sharon baadaye walikuwa mawaziri wakuu wa Israel kwa nyakati tofauti.
 
Safi sana 👍
 
Hili wala halina ubishi mkuu!sijajua lengo la mleta mada lilikuwa ni lipi maana dunia hii mapito katika kila kizazi
 
Kuna baadhi ya maamuzi yanakuaga yanaitaji stimulation ya brain kwaiyo uwa naamini ukiskia tramp anavuta sonyo au kim anakula ugoro usishangae #wanadamshi😅
 
Kuna baadhi ya maamuzi yanakuaga yanaitaji stimulation ya brain kwaiyo uwa naamini ukiskia tramp anavuta sonyo au kim anakula ugoro usishangae #wanadamshi[emoji28]
Kabisa mkuu mi mwenyewe nakuwaga at the best sana Nikitumia walau Alcohol kidogo
 
Hili wala halina ubishi mkuu!sijajua lengo la mleta mada lilikuwa ni lipi maana dunia hii mapito katika kila kizazi
Mtoto...
Nimekutana na picha za vitu vya zamani hapa mtandaoni vitu ambavyo vimenikumbusha historia niijuayo katika vitu hivyo.

Ndipo nikaamua kuwa nitaandika historia hizo kwa nia ya kuweka kumbukumbu na nikaanza na Mwalimu Nyerere na sigara Clipper.

Katika picha hizo kuna picha ya Aspro.

Niliamua baada ya sigara niandike makala kuhusu Aspro ambayo inawahusu watu watatu muhimu sana katika Afrika ya Mashariki na Kati katika miaka ya 1950 hadi 1960 - Peter Colmore, Mwenda Jean Bosco na Eduardo Massengo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 



Sent using Jamii Forums mobile app
 

Attachments

  • ASPRO.jpg
    6.8 KB · Views: 61
  • EDUARDO MASSENGO IN STRIPES.jpg
    12 KB · Views: 52
  • MWENDA JEAN BOSCO.png
    31.7 KB · Views: 59
kuna picha moja inamuonesha mwl. J.K NYERERE akicheza pool table huku pembeni yake akiwepo kamanda mmoja wa polisi. hivi ktk kile kipindi mchezo uo ulikuwepo TZ & MWL amewahi ucheza kweli?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…