Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
SIGARA "CLIPPER" ALIYOKUWA AKIVUTA MWALIMU NYERERE
Picha hiyo hapo chini imepigwa mwaka wa 1955 Magomeni Mapipa Mtaa wa Jaribu kwenye Tawi la TANU alilofungua Ali Msham nyumbani kwake.
Ali Msham ni huyo upande wa kulia aliyekuwa katika ya vijana wawili wamepiga lubega za kaniki mmoja ana shoka begani.
Hawa walikuwa Bantu Group wahamasishaji umma na walinzi wa viongozi wa TANU.
Waliokaa kulia ni Zuberi Mtemvu, Julius Nyerere na John Rupia.
Ukimwangalia Nyerere utaona ameshika paketi ya sigara na ana sigara mkononi.
Mwalimu katika ujana wake alivuta sigara na sigara yake ilikuwa "Clipper," sigara maarufu enzi hizo. Paketi yake ni hiyo hapo juu.
Mwalimu aliacha kuvuta mwaka wa 1962 baada ya kifo cha rafiki yake kipenzi Hamza Mwapachu kufariki kwa maradhi ya moyo yaliyosababishwa na uvutaji sigara.
Sent using Jamii Forums mobile app