Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mbunge wa Viti Maalum (Mkoa wa Njombe) kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Sigrada Mligo amesema madai ya kwamba Bunge la sasa ni "Bunge haramu" yanatokana na namna uchaguzi mkuu ulivyoendeshwa, akieleza kuwa hata yeye na wabunge wengine wa upinzani hukumbana na kauli zinazowaita "wabunge wa mchongo" wanapotekeleza majukumu yao.
Sigrada alisema licha ya kuwepo kwa mitazamo hiyo, wao waliamua kuingia bungeni kwa makusudi ili kuhakikisha hawawaachii nafasi waliowaita "maharamia" kuendelea kufanya maamuzi bila uwepo wa sauti mbadala. Alisisitiza kuwa kuingia bungeni ni njia ya kufuatilia na kupinga kile wanachoamini hakikuwa sahihi katika mchakato wa uchaguzi.