Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,307
- 25,932
Ujumbe wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan, kabla ya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri, ulikuwa wazi. Ni kuwa mabadiliko ya Baraza yamefanyika ili 'kubaki' na wa kwenda nao pamoja 2025 na 'kuwapa nafasi' ya maandalizi wenye nia na 2025. Ndiyo kusema, waliotarajiwa kuachwa na Rais Samia ni wale ambao walikuwa wakitingwa na maandalizi yao ya mwaka 2025, mwaka wa uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani. Baada ya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri, kukatokea mjadala mkubwa. Mjadala ni sehemu na ndiyo utamu wa siasa.
Tupo tuliosema kuwa walioachwa ndiyo hasa waliopewa nafasi ya kuendelea na maandalizi yao ya mwaka 2025. Tupo tuliosema kuwa walioachwa ndiyo waliokuwa wakimkwamisha Rais Samia katika utekelezaji wa majukumu yake kiserikali na kusimamia ipasavyo utekelezaji wa Ilani ya CCM. Tupo tuliojaribu kumulika hili na lile lililopelekea huyu au yule kuachwa kwenye Baraza la Mawaziri. Sote tulikuwa sahihi kwakuwa ni maoni yetu.
Nafasi ya Spika ni nafasi kubwa. Spika ni kiongozi wa mhimili wa Bunge. Spika ndiye anayeongoza na kuratibu mijadala Bungeni wakati wa uundwaji wa sheria na hata wakati kujadili na kupitisha bajeti.
Spika hapaswi kuwa na mambo mengi (kama hayo ya kujiandaa na uchaguzi mkuu wa 2025). Spika anapaswa kuwa ni mtu asiyeweza 'kumkwamisha' kwa namna yoyote Rais- sheria zipite na bajeti zipite. Spika anapaswa kuwa pamoja na Rais.
Sisi tulioona kana kwamba walioachwa ndiyo waliosemwa na Mhe. Rais kabla ya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri, hatuoni nafasi yoyote ya Mhe. William Vangimembe Lukuvi au yeyote aliyeachwa akipenya kwenye chujio la kumpata mgombea wa Uspika kupitia CCM. Itakuwa ni kama kuhamisha pesa kutoka mfuko wa shati kuweka wa suruali.
Ikumbukwe kuwa aliyebadili Baraza la Mawaziri kwa sababu alizoueleza umma ndiye pia Mwenyekiti wa CCM Taifa. Ndiye atakayeongoza vikao vya kimaamuzi katika kumpata mgombea wa Uspika.