Siioni Simba SC Kwenye Robo Fainali CAF

Siioni Simba SC Kwenye Robo Fainali CAF

Megalodon

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2021
Posts
3,534
Reaction score
7,866
Ninaamini kabisa Uwezo wa kuiadhibu SSC ulikuwa ni mkubwa sana na muda mwingi TP Mazembe walipokuwa na mpira walifanya mashambulizi CONSTRUCTIVE, ni vile tu walijua ni Friendly Match.

SSC kama kawaida, ni kupigiana pigiana mapasi ambayo hayafiki Robo tatu ya uwanja, ni ma pass plus plus amabayo yanachezwa kuanzia katikati ya uwanja kurudi golini kwao. Je mpira ni possession au Matokeo.?

Kikosi cha kwanza kilijitahidi ingawa hakukuwa na stricter sababishi. Baada ya hapo, kila sub iliyofanyika ilienda kubomoa kabisa chemistry ya kikosi cha kwanza na goli likapatikana.

Kifupi mpaka sasa SSC haina mtu anaeweza kufunga magoli, na bado haina stricter ya maana. Yaani stricter zilizokuwepo ni zile ambazo haziwezi kuleta matokeo, one clear Chance unatakiwa kumuadhibu kipa. Mugalu na Kibu walikuwa na clear chance na hawakuweza kuleta Matokeo.useless

Kikosi kilishabomolewa, tujiandae kwa lolote na tusiwe na expectation zozote kwenye klabu Bingwa Africa mwaka huu.

Simba ya sasa haina Chemistry wala wachezaji watakaoweza kuipeleka timu robo fainali. Nina wasiwasi sana yatatokea ya Ud Songo huku tukiwa wazuri wa kumiliki mpira kwa nyuma.

Tatizo kubwa sajili za Mo ni sajili za kimasikini na zisizo na tija; unaenda kusajili kipa wa 5, halafu unasahau striker zenye akili. Msione Ahly inachukua makombe mkadhani ni uchawi.

Hakuna uchawi kwa mpira, ni Investment.
Simba Out
 
Uzi wako umekaa kinazi sana,by the way waachie wenye Simba yao,nyie mmeshatolewa kazi iliyobaki kwenu sasa hivi ni kupokea timu ngeni ambazo zitakuja kucheza na Simba Nalog off!

Acha Utopolo kaka , Unazi Upo wap
 
Hata VPL mwaka huu,simba kuchukua ubingwa itakuwa ni Bahati.

Kuna wachezaji kama kina Luis wale walikiwa ni fighter na walikuwa na dream zao kichwani ndio maana walitaka kuonekana sana

Mtu kama Mugalu, Boko, Kagere wale wamesharidhika na mil 7 za MO. Hawana future yoyote . Mwaka huu kazi ipo

Yaani STRIKER wanacheza offside hatari . Mbona TP MAZEMBE hawakuwa na ofiside. Ni kwa sababu wanajua mpira
 
Sema sijaelewa STRICTER kwenye uzi wako ina maana gani.Is this new terminology in football? afu mambo ya chemistry kwenye mpira ni maneno ya mashabiki wa UTO.Anyway,thank you! possibly one day you will understand that being a football analyst isn't something meant for you.
 
Sema sijaelewa STRICTER kwenye uzi wako ina maana gani.Is this new terminology in football? afu mambo ya chemistry kwenye mpira ni maneno ya mashabiki wa UTO.Anyway,thank you! possibly one day you will understand that being a football analyst isn't something meant for you.

Ha ha relax , it is just spelling errors, son !

Did I even mention that I am football analyst? You have put words in my mouth, Bwanamdogo.
 
Ninaamini kabisa Uwezo wa kuiadhibu SSC ulikuwa ni mkubwa sana na muda mwingi TP Mazembe walipokuwa na mpira walifanya mashambulizi CONSTRUCTIVE, ni vile tu walijua ni Friendly Match...
Na wakifika mbali utatujibu nini mkuu hapa .??
 
Back
Top Bottom