Kwanza nikiri kuwa kama kuna kitu najitahidi sana niendelee kukiepuka ni kamari ya aina yoyote. Nikiwa mdogo sana mtaani kwetu jamaa aliliwa pesa, shati, viatu, suruali, kofia na saa kwenye zile kamari za wahuni za karata za kawaida wala sio karata tatu. Jamaa alitoka kijiweni anakatiza mtaani na chupi kongwe ya VIP mpaka nyumbani kwao. Tokea wakati huo niliichukia kamari mpaka kesho sijawahi kujihusihsa na hiyo michezo na numuomba sana Mungu anijalie niendelee hivi hivi.
Ila ninachokiona sasa hivi kwenye betting ni tofauti sana. Kamari ime advance sana na vijana kwa wazee wanajua namna ya kumla Kanjibai. Kuna watu mtaani wamejiajiri kwenye betting wana maisha mazuri sana kuliko hata watu waliojiriwa na wenye kazi nzuri. Niliwahi kufanya utafiti usio rasmi mtaani sikuamini kwa kweli. Kuna watu wamefanikiwa pakubwa kwenye betting ila pia wapo waliopotea mazima. Unakuta mtu wa kawaida mtaani alianza betting na laki moja lakini sasa hivi ana mtaji wa milioni zaidi ya ishirini kwa muda mfupi tu.
Hitimisho langu ni kuwa kama mtu anaamini kuwa betting ni nzuri aachwe aendelee kwani sasa hivi kuna watu nawafahamu mtaani kwangu wanaendesha familia zao, wanasomesha watoto, wanajenga majumba, wananunua viwanja, magari, n.k. Lakini mtu anyeamini betting ni mbaya naye maamuzi yake yaheshimiwe. Na kama una roho nyepesi hayo mambo usijaribu kabisa labda upate wataalamu waliobobea ambao wao kila week end wanampuna kanjibai bila wasiwasi. Ukiingia kichwa kichwa bila ya kuwashirikisha wabobezi wenyewe wanajiita "wakamaria" aisee ujue unaenda kuisambaratisha familia na huenda ukauza kila kitu na kuiacha familia inahangaika. Na wapo watu wameadhirika hapa mtaani kwetu walikuwa na maisha mazuri tu lakini sasa wamekuwa mafukara kabisa.