Sijaelewa sababu ya mlinzi huyu kumshika mkono Afande Sele alipokuwa anasalimiana na Dr. Magufuli

tatum

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2018
Posts
5,786
Reaction score
4,491
Rais Magufuli alipokuwa anafungua kiwanda mjini Morogoro alipata nafasi ya pia ya kumpokea Mwanamuziki maarufu mjini hapo Afande Sele kutoka chama cha ACT na kujiunga na CCM.

Lakini wakati Afande Sele akishikana mkono na Rais Magufuli mkono mwingine ulishikwa na moja ya walinzi wa Rais....nini hasa kilipelekea mlinzi huyo kumshikana mkono mwingine Afande Sele?
 
hakuna lolote basi tu ili mradi mlinzi naye aonekane anapiga kazi
 
Kuna mambo ya msingi ya kuliza lakini siyo hili

Kwahiyo hujui sababu za huyo mlinzi kumzuia?

Elimu ya Tanzania kweli magumashi...
Wanaosalimiana na Rais Magufuli wote wanashikwa mkono mmoja.
 
Mashambulizi kwa yule unayemlinda huwa sio lazima yawe ya kibunduki.
Yapo pia ya kikemikali, na mengineyo.

Ni standard procedures tu.
Afande Sele alionyesha threat yoyote?
 
Usimwamini kila mtu anayemsogelea rais
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…