Sijaelewa sababu ya mlinzi huyu kumshika mkono Afande Sele alipokuwa anasalimiana na Dr. Magufuli

Sijaelewa sababu ya mlinzi huyu kumshika mkono Afande Sele alipokuwa anasalimiana na Dr. Magufuli

Inasemekana kila atakachofanya president kinakuwa kwenye ratiba, na kusalimiana na Afande sele haikuwemo kwenye ratiba, na hiyo inakuwa katika malengo ya ku-control mazingira ili kuhakikisha usalama.
Kuna matukio mengi tu Rais huwa anafanya na hayako katika ratiba....mfano yule mama aliyekabidhiwa pesa na Rais hakuwa katika ratiba na alisalimiana na Rais baada ya kupewa pesa na watu wengine lakini hatukuona mkono wa mlinzi ukimzuia.

Ndiyo maana nataka hasa kujua Sele alitaka kufanya nini mpaka akamatwe mkono. hili jambo ni very serious ingawa kuna watu wanaona ni jambo la wanausalama na ni la kawaida tu.
 
Swali la msingi Afande Sele alitaka kufanya nini au kulikuwa na ishara gani mpaka ashikwe mkono mmoja.
elimu inahitajika mkuu.

hivi hujui kama usalama wana sheria zao zinawaongoza katika kazi zao??

sasa je ikiwa kama kile kitendo ni sheria ya kazi yao ndo inawaelekeza we unahoji kitu gani?
 
elimu inahitajika mkuu.

hivi hujui kama usalama wana sheria zao zinawaongoza katika kazi zao??

sasa je ikiwa kama kile kitendo ni sheria ya kazi yao ndo inawaelekeza we unahoji kitu gani?
Tueleze wewe unayezijua hizo sheria zao kwa kitendo kile...
 
Changemoto kubwa kwa walinzi wa viongozi ni matukio yasiyokwenye ratiba.
 
Kuna matukio mengi tu Rais huwa anafanya na hayako katika ratiba....mfano yule mama aliyekabidhiwa pesa na Rais hakuwa katika ratiba na alisalimiana na Rais baada ya kupewa pesa na watu wengine lakini hatukuona mkono wa mlinzi ukimzuia.

Ndiyo maana nataka hasa kujua Sele alitaka kufanya nini mpaka akamatwe mkono. hili jambo ni very serious ingawa kuna watu wanaona ni jambo la wanausalama na ni la kawaida tu.
Aisee, wewe kijana mbona msumbufu sana?
 
Changemoto kubwa kwa walinzi wa viongozi ni matukio yasiyokwenye ratiba.
Ni kweli nakumbuka hata mazishi ya Mfalme Hassan II wa Morocco wakati wa mazishi yake mwaka 1999 mwezi July Rais Clinton alitakiwa kuishia kwenye swala ya mazishi na si kufika eneo la mazishi lakini kuna kiongozi wa Morocco aliyemwambia twende kuzika ni eneo la kutembea kwa miguu kama km 2 hivi hapa walinzi wa Clinton walipata shida sana kwasababu watu walikuwa wengi sana na hakukuwa na maandalizi yoyote lakini ndo Clinton amesimama na kuendelea na matembezi mpaka makuburini.

Hiyo ilitolewa na mmoja wa walinzi wake ambaye alipewa kazi siku hiyo ya kuwa mlinzi no 1 wa Rais baada ya kustaafu hiyo kazi.Na walishamwambia toka awali Clinton kuwa aishie palepale kwenye swala tu.Lakini alinyanyuka na kuanza kutembea na wale viongozi wengine kuelekea makaburini walinzi wote walichanganyikiwa lakini ilibidi wafanya kazi ngumu sana na ya ziada kwenda mazishini.

Aliongea hayo kuwa ndiyo siku pekee katika kazi ya ulinzi wa Rais alipokuwa na wakati mgumu sana toka ameajiriwa mpaka anastaafu hiyo kazi.Na alikuwa African American yaani ngozi nyeusi.
 
Uyo bodyguard alihisi kwakua mibange ya zamani bado Iko kichwani kwa afande. isijemlipuka afu akaharibu.
 
Akili ya kawaida tu inakwambia alishikwa huo mkono ili kuepusha possibility ya yeye kurusha kofi zito.
 
Back
Top Bottom