Niwe muwazi mimi binafsi nina amini katika mabadiliko, mabadiliko ndiyo chachu ya maendeleo sehemu yoyote ile.
Nimeona na nimekuwa nikifatilia mikutano yote ya mgombea wetu hapa Dar na kuna afadhali kidogo japo mkutano wa segerea na kawe ulikuwa hauna watu sana, atleast kule Mbagala.
Naanza kupata picha, pengine kuna kitu hakipo sawa Chadema.
Tusi-conclude kuwa wanaoenda kwenye kampeni za CCM wanafata wasanii tu, hapana.
Ila kama wanafata wanancho wengi wanafata wasanii huko ccm basi sawa, ila pia basi kwa uwingi huohuo na kwa aina ya kukubalika kwa chama chetu basi walitakiwa pia wafate/waje kwa wingi kwenye kampeni zetu.
Kuna mikoa hadi sasa sinaelewa nini hasa kimetokea kutokana na uchache wa watu waliohudhuria tena kwenye viwanja vidogo sana ambavyo tumwchagua kufanyia kampeni.
Tuliona watu kule mwanza na tulifarijika sana na hilo na hadi tukatumia ndege nyuki
(drones) kupiga picha za kampeni zetu. Ila baada ya hapo sikuona tena picha za juu (za
drone) kwenye kampeni zetu.
Kilichotokea shinyanga, tabora na sasa dodoma ni aibu. Chama kitafute namna au kubadili mbinu ya kampeni ili tuweze kuvuta watu wengi waje kusikiliza sera.
Chini ni picha ya watu waliohudhuria kampeni hii leo huko Dodoma.
Wewe ni nani kwani?
Mimi nipo Tabora hivi ninavyopsti comment hii...
Jana nilikuwepo kwenye mkutano wa mgombea wa CHADEMA ndg Tundu Lissu mwanzo mwisho...
It was a clouded rally..
Mkutano ulifanyikia katika viwanja vya Chipukizi katikati ya mji wa Tabora nyuma ya makao makuu ya kanisa katoliki, Jimbo la Tabora...
Ulikuwa ni mkutano usio na wasanii wala burudani ya aina yoyote lakini umati wa watu uliohudhuria kwa hiari bila kushurutishwa ni balaa, ni wengi sana...!!
Tamaa na shauku yao ilikuwa ni kimsikia Rais wao mtarajiwa Mh. Tundu Lissu...
Na kwa kulitambua hilo, Tundu Lissu alikosha nyoyo za watu vilivyo...
Niliandika jana na leo naomba nirudie, kwamba;
Hoja ya CHATO INTERNATIONAL AIRPORT itamtesa sana Magufuli na wana CCM kuitetea...
Na kwa kuwa Tundu Lissu ana kipaji cha kufafanua na kuelezea jambo ktk lugha rahisi na kueleweka, hii iliwangia vyema wana Tabora na kuwajengea picha kuwa....
Bw. John Pombe Magufuli ni kiongozi mpuuzi, mbinafsi anayejijali yeye na tumbo lake tu, mroho na fisadi wa kutisha kuliko wenzake wote waliomtangulia yaani Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete...
Kwa sababu ktk akili ya kawaida ya mtu yeyote yule ni ngumu sana kudhani kuwa Rais anaweza kuamua kujijengea uwanja wa ndege kijijini nyumbañi kwake kwa kutumia mabilioni ya fedha kwa ajili yake mwenyewe na mama yake tu huku akiacha matatizo ya kawaida yenye kuhitaji rasrimali fedha kidogo tu kuyatatua....!!
Kwa habari ya "umati wa watu" Tabora na Shinyanga na hapa Tabora, haieleweki wewe umepata wapi hizi picha na lengo lako ni nini tu..
Nadhani umefanya hivi kujifariji kwa propaganda uchwara kabisa....
Kama unataka kujua umati uliohudhuria mkutano wa kampeni wa Tundu Lissu, Tabora basi unaweza kuwauliza polisi na wenye Magari....
Maana ulipoisha ile saa 12 jioni, ilibidi barabara kuu ya kutoka Nzega kuingia katikati mjini ifungwe kwa dakika kadhaa ili kuruhusu watu watawanyike kwa amani. Hii ilichukua takribani dakika 30 ndipo hali ya kawaida iliporejea...
Kwa wewe naweza kusema bila wasiwasi wowote kuwa you are pretty liar...!!