Sijajutia kabisa safari yangu ya Morogoro kuangalia maeneo (ardhi) ya uwekezaji

Kweli wewe unaijua Moro, mimi naifahamu Mvomero ngoja mtoa mada aje kutoa ushuhuda muda siyo mrefu! Eti wenyeji wavivu!Ameendeshwa na mhemko,papara,ushamba,ulimbukeni,kiburi n.k! Rudi tena kwa wenyeji wako wa Mvomero!
Swadaktaaaa, Mimi Mara ya kwanza nilishangaa sana, nikasema mbona maeneo mengi, watu wapowapo tu. Nikaambiwa kaa kwa kutulia ndugu. Kuanzia hapa, hadi kuleeeeeee, eneo la mtoto wa mukulu aliyegoma kustaafu, alafu hapa hadi kuleeeeeeeeee la kamanda yule mstaafu, kuanzia hapa hadi unaikuta lami, la wale wenye mabasi ya red red.

Nikachoka. Imagine robo3 ya kijiji unakuta ya watu wawili, robo ndio wabagawana wanakijiji wote.
Ndio maana sijambishia mleta mada, ardhi waliyomwambia ipo ni ndogo kwa wengi. Kifupi hakuna usawa.
 
Mkuu mimi nalima miwa Vijiji vya Dihinda na Kaole, mbele kidogo ya shamba la mitiki la Mtibwa. Nataka kuja huko Mkulazi/mbigiri aiseee maana Mtibwa Sugar wanasumbua sana kwenye kununua miwa yetu kwa wakati, nitakurafuta.
 
Bei ya shamba kwa ekari moja ni kiasi gani huko kwa wastani?
 
Aiseee 😂😂
 
Bei ya shamba kwa ekari moja ni kiasi gani huko kwa wastani?
Inategemea unataka kulima nini
Mashamba ya mpunga Yana bei zake na yapo ya kawaida ya kutegemea mvua lakini pia yapo yenye mifereji ya maji (skim), mashamba ya vitunguu yana bei yake pia lakini mahindi,alizeti na mbaazi sana sana hukodishwa kwa elfu 40 Hadi 50 kwa heka kwa msimu mmoja
 
Mkuu nakushauri nmezaliwa morogoro na kukulia morogoro wilaya ambayo sikushauri uwekeze kilimo ni gairo kilimo nenda kilombero mlimba malinyi na mvomero na kilosa baadhi gairo n ufugaji basi
Acha hizo za negativity. Mwaka 2009 nilitaka kuwekeza kwenye biashara ya mbao maeneo ya Mkolani au Buhongwa hapa Jijini Mwanza. Nikaenda kuomba ushauri kwa ndugu yangu mmoja ambaye alikuwa mwekezaji na mkazi wa maeneo hayo. Alinikatisha tamaa sana, nikaacha kuwekeza kipindi kile.

Ninachojua, kwenye dunia hii hakuna free milk. Maisha popote pale ni kupambana. Wacha tumpe moyo kijana apambane.
 
Hongera sana Kuna sehemu umetaja nimewahi kuishi miaka ya nyuma, umenikumbusha mbali sana
Difinga
Dihinda
Lusanga
Madizini
Turiani
Kidudwe
Mtibwa
Upande wa tanga nimetoka 2022 hapo kikunde mafulila Kuna mgodi wanapaita seita
 
Huyo kama kazaliwa pale ndo wale wale wavivu. Achana nae na asikupunguzie mwendo.
 
Kweli wewe unaijua Moro, mimi naifahamu Mvomero ngoja mtoa mada aje kutoa ushuhuda muda siyo mrefu! Eti wenyeji wavivu!Ameendeshwa na mhemko,papara,ushamba,ulimbukeni,kiburi n.k! Rudi tena kwa wenyeji wako wa Mvomero!
Hakuna mbadala mkuu wenyeji ni wavivu 90% utajua yote hayo nakwambia na mengine mengi ambayo hujayaandika ukweli ni kwamba ninyi ni wavivu.

Hapo hapo Mvomero nimekutana na wasukuma Hadi mawasiliano Yao ninayo wanapiga kazi. Ukishindwa wewe na mke wako usidhani wote watashindwa mkuu. Tulizana wewe na mke wako mengine waachie wanaume. Nimetoka kahama Hadi hapo sijakurupuka Wala mhemuko ama papara la hasha!

Unapajua Pwani kisarawe (mto ruvu)? Upande huu ni morogoro na ng'ambo ni pwani?


Huko pia nishafika mkuu napajua Nje ndani vigogo Wana mashamba na mapori ya kutupwa lkn kipindi hicho hicho mjomba alipata Heka 70 Nenda gwata sehemu Moja inaitwa vizembe.

Kama ungesema hamna soko hapo ningekuelewa lkn Kwa uharo ulio andika nakuona ni Moja ya watu walioshindwa Kwa 100% unataka na wengine washindwe. Nimenunua heka5 trh16/11/2024. Tusitishe watu. Cha kuogopa ni kupoteza maisha tu na sivingine!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…