Nikifa MkeWangu Asiolewe
JF-Expert Member
- Feb 26, 2024
- 6,944
- 14,351
- Thread starter
- #21
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu hata sisi ni walozi vilevile.ukija kilokole tuna dili kilokole ukija kichawi vivyohivyo. (Sikuuliza mkuu)Walozi vipi
Ahsantee mkuuNimesoma mpka mwisho inavutia
Lucas Mwashambwa unadhani angeishije na unajua wazi kabisa uchawa ndo unamuweka mjini😆😄 Ukishaona kidongo chekundu tu basi jua upo Tanzania vijijini. Kwa aina ya hizo nyumba CCM walitakiwa wawe washaondoka madarakani!
Mkuu katika pita pita zangu sikuona Kwa wingi ila pale Turiani zipo Hadi zinamwagikia.Pisi zpo
Huu mti ni nyara za serikali,ukiukata ni kesi ya kuhujumu uchumiNaomba jina la mti huu Tafadhar iwe kilugha ama Kwa kiswahili nahifadhi kumbukumbu.
View attachment 3155020
Alafu mimi hapa natafuta eneo la kufugia karibia miaka miwili sasa bila mafanikio. Nitaenda huku.Heshima kwenu wakuu!
Niliazimia siku Moja nitembelee morogoro wilaya ya Gairo na Mvumero! Hatimae ikawadia na ikaenda sawa sawia kabisaa...
Kutoka kahama Hadi Gairo morogoro safari ilianza saa2:30.
Gari ilikuwa na changamoto kadhaa hasa kuharibika na Hadi kufika saa9 arasiri nikawa nimewasili salama Gairo.
Fuatana Nami nikupitishe Kwa machache kati ya mengi niliyoyaona.
Nilianza kuangalia Fursat zilizopo kandokando ya barabara kuu ya yaani ya kwenda Dar.
Fursat za uwekezaji zilizo Nje Nje nilizo ziona.
Maeneo hayo unaweza Jenga shule, ufugaji na kilimo Cha umwagiliaji japo itakupasa uchimbe kisima Kwa maji ya Uhakika
Safari yangu ndefu Sasa imetoka Barabara kuu na kushika barabara ya IYOGWE barabara hii itanipeleka hadi mpakani kati ya Morogoro na Tanga(Gairo &Tanga)
Nikiwa na usafiri wa pikpik Mimi pamoja na mwenyeji wangu. Sikuwa na budi ya kuweka full Tank maana nilihakikishiwa sitajutia kabisa na safari.....
Tukaanza ardhi yenye rutuba kiasi baridi kiasi likituandama huku milima ya uluguru ikiwa imefunikwa na wingu zito na mwonekano maridhawa kabisa.View attachment 3154970
Safari yetu iliendelea vizuri kabisa Na Hivi ndivyo vijiji nilivyo vipita Gairo ukielekea mpakani.
Br ya iyogwe:-
chakwale,
Nguyami,
Idibo,
itaragwe,
makuyu na Iyogwe.
(Kuna baadhi ya vijiji sikuona ubao) Pikipiki ilikuwa masaa....
Vijijini Hivi vipi wilaya ya Gairo morogoro
Na vinafaa sana Kwa ufugaji ila mifugo kama kuku,nguruwe ama ng'ombe wa maziwa kwani ni makazi ya watu.
Ukifuga mbuzi bila shaka utasumbuana na wakazi.
Nimefika mpakani Sasa
Sasa unaingia Mkoa wa Tanga..
View attachment 3154977
Baada tu ya kutoka mpakani Kuna mto nahisi ndo unatenganisha Gairo na kikunde.
Hapo unakutana na mto na wakazi wake waliendelea na shughuli za kilimo Cha mwagilia.
Kwa namna nilichoona pale jinsi ya eneo lilivyo na kinachofanyika pale niliona ni mzaha mkubwa. Maji ni ya lutekenya tu lakini kinacholimwa ni kidogo sana ardhi Ina rutuba Hali ya hewa nzuri.
Nilipofika KIKUNDE SENTA Nilikuta vijana wamekaa wanaotoa moto hawana habari na wengine nikawaona wanaranda tu mtaani kwenye vijiwe nilisitikika sana kuona vijana hawana habari kabisa na fursa nilizo ziona Mimi!!
Ukweli ni kwamba pamoja na ardhi kuanzia kikunde nk Inakubali sana Kwa mazao kama mahindi, maharage,mihogo, Kwa kifupi karibia Kila zao la nafaka linakubali maeneo hayo
Wenyeji watatusaidia hapa.
Tu
View attachment 3154979
View attachment 3154981
Ardhi yenye rutuba mito yenye maji lakina hakuna mazao ya umwagiliaji!
View attachment 3154983
Ardhi inalipa sana Kwa kilimo Cha matunda kwani Kwa macho yangu nimeona miti ya miembe(kienyeji) imestawi sana na Bahati nzuri lazima bondeni kuwe na mto
Ardhi ni nzuri Kwa uwekezaji wa kilimo na huku Sasa hata ufunge ng'ombe wa kwenda kuchunga na jioni uwarudishe panastahili!
Shauku Bado ikiwa inahitaji kuendelea kusonga mbele zaidi na kuona namna halisi ya Nchi ya maziwa na Asali
Baada ya kutoka Kikunde Kuna vijiji kama..
kikunde,
ludewa,
mafulila,Tunguli,
Lusane
Hapo Tunguli Kuna pori kubwa na zuri Kwa kilimo na ufugaji barabara ya uhakika japo ni vumbi.
Tunguli ni pazuri sana Kwa uwekezaji mkubwa.
Nimeona Kwa macho yangu watu wakifyeka pori Kwa ajiri ya
kilimo nk.
View attachment 3154985
View attachment 3154986
Hatimae kipande Cha Tanga nikakimaliza na kuingia wilaya ya Mvumero (morogoro)
Swadakta kabisaa mazingira & Hali ya hewa ilinivutia kuliko kifani!!!
Ikanilazimu kutoka moyoni nipambatize Kwa jina jipya la Thailand.
Kwani sehemu hii ni sehemu ambayo kijogorafia imekaa kama ughaibuni(Thailand japo sijafika)
Misitu minene yenye ukijani kibichi kabisa kama paradiso! Ukiangalia baadhi ya clip za Thailand utakubaliana Nami pasina shaka yoyote Ile!
Kwa wale wafanyakazi unayependa mazingira kama Yale ni muda wako Sasa wa kwenda kuona huko kwenye vijiji Hivi...
kibati,
kibogoji,
masimba,
Difinga,
Apendae,
Kwakwempe,
magotwe,
Kwa Dole
Lusanga
Tuliani,
manyiga,
mlaguzi.
Dakawa,
Hembeti,
Magole,
Dumila feli,
Dumila,
Hapa Kwa Retirement panafaa mnoo Kuna baadhi ya sehem nzuri,nzuri sana,na nzuri kabisa!!!
Ni juu Yako wewe Sasa wapi utapapenda
Hapo nimeunganisha Hadi Dumila.. maeneo yote hayo unalima muda wowote ukitaka
Niliona Kwa macho yangu Nchi hii Ina Tiririka maziwa na Asali.
************************
Pamoja na hayo yote nilichojifunza nikuwa
Vijana wa maeneo Tajwa ni wavivu usipime!
Nilicho shangaa nikaenda kupata supu halafu tukakoswa limao na kuletewa limao la unga zile zinauzwa kwenye pakiti Ili Hali ardhi Ile ukipanda mti haihitaji hata kumwagilia Cha ajabu limao ni anasa na vijana wapo tu.
Vijana nawaomba tutoke mjini kama huna issue ya maana.
Manyanza Toka magetoni Toka Dar uachane na biashara ya kupiga chabo wazaramo wakimwanga ladhi.
Niishie hapa nitaendelea kwenye comment
View attachment 3154987
Haya ndiyo mazingira murua kabisa ya baadhi ya vijiji/vitongoji Tajwa hapo juu.View attachment 3154988
Fenesi hili nilijipatia Kwa Tsh1000 hapo ni Kwa Apendae.
View attachment 3154989
Ardhi yenye maziwa na Asali.View attachment 3154992View attachment 3154993
Sehemu tulivu sana huku sauti ndege za ndege zikiimba utukufu wa Mungu!!View attachment 3154998hapo passion3 zinauzwa Kwa 200 ndizi2 sh 2000 embe2 dodo og zinauzwa500.View attachment 3155001View attachment 3155000
Tafadhar Endelea kubaki hapa.
View attachment 3155002
Nyumba hizi uzionazo ni kando kando ya barabara.uzuri ni kwamba njia inapitika Kwa Uzuri bila shida yoyote.
NB: Picha zote hizi zimepigwa kiangazi 17/11/2024.
Kama mahitaji video zipo nzuri kabisaa!! Niwezeshe vocha iwe ya jero ama buku niweke hapa nitumie Pm.
Ahsanteen sana.
Ndio jina lake huo mti? Pia ni dawa huo mti, ukichanjiwa nyota inang'aa kibiashara na kila kitu,kama unavyovutia wenyewe huo mti (kwa wale waswahili wenzetu)Huu mti ni nyara za serikali,ukiukata ni kesi ya kuhujumu uchumi
Umejuaje ardhi ina rutuba kama hujaa na kuishi ukalima ukaona kinachotoka.....mkuu unaangalia kwa macho?Kwa namna nilichoona pale jinsi ya eneo lilivyo na kinachofanyika pale niliona ni mzaha mkubwa. Maji ni ya lutekenya tu lakini kinacholimwa ni kidogo sana ardhi Ina rutuba Hali ya hewa nzuri.
Jina sulijui ila imejaa huo ukanda kuanzia chalinze ,Tanga,MorogoroNdio jina lake huo mti? Pia ni dawa huo mti, ukichanjiwa nyota inang'aa kibiashara na kila kitu,kama unavyovutia wenyewe huo mti (kwa wale waswahili wenzetu)
Wewe mkuu umejiandaa safari ukiwa na kibunda chako. Lakini jmeleta dhsrau etu vijans ni wavivu.Vijana wa maeneo Tajwa ni wavivu usipime!
Huo unaitwa Mgude . Kuna methali yake inasema " Asali ya Mgude - huliwa kwa macho" unateleza sana hivyo ni mgumu kuupanda.Naomba jina la mti huu Tafadhar iwe kilugha ama Kwa kiswahili nahifadhi kumbukumbu.
View attachment 3155020
Ahsantee sana mkuu. Ubarikiwe mnoHuo unaitwa Mgude . Kuna methali yake inasema " Asali ya Mgude - huliwa kwa macho" unateleza sana hivyo ni mgumu kuupanda.