Sijajutia kabisa safari yangu ya Morogoro kuangalia maeneo (ardhi) ya uwekezaji

Sijajutia kabisa safari yangu ya Morogoro kuangalia maeneo (ardhi) ya uwekezaji

Kweli wewe unaijua Moro, mimi naifahamu Mvomero ngoja mtoa mada aje kutoa ushuhuda muda siyo mrefu! Eti wenyeji wavivu!Ameendeshwa na mhemko,papara,ushamba,ulimbukeni,kiburi n.k! Rudi tena kwa wenyeji wako wa Mvomero!
Acha mikwara. Mvomero ni wavivu nikimaanisha Mvomero kama kijiji na kata toka hata haijawa Wilaya ikiwa chini ya Morogoro DC enzi za akina mzee Mbilu, mzee Joka diwani yule mwarabu ambaye mtoto wake ni DAS kule Mbeya na refa wenu maarufu alikuwa anaitwa Ombopa.

Wakati nasoma Lusanga Sekondari nilikuwa nakuja kucheza ndondo hapo naichezea Asec ile ya waarabu akina Seifu kabla sijasajiliwa Mtibwa Sugar. Msalimie Ramadhani Lundenga na Salum wa Gheto kama wapo hai na wapo hapo Mvomero.

Watu wa pale wanaendekeza majungu tu. Mleta uzi ni msukuma wao wanapiga kazi tofauti na nyie wazigua na wasangazua😀😀😀
 
Hapa kijiji gani Mkuu?

Kama inawezekana, chini ya kila picha ukàandika Jina la kijiji ulopopiga.

Ahsante, Kwa kushare utajiri wa nchi hii.View attachment 3155699
Mkuu vijiji ni vingine na vina ufanano sana nashindwa kudadavua ni wapi hasa lkn ramani inakuja kati ya vijiji hivi
masimba,Difinga,Apendae,
Kwa kwempe,magotwe,Kwa Dole.
Ni barabara Ile Ile ya kuja Turiani mkuu
 
Mvomero ni wavivu nikimaanisha Mvomero kama kijiji na kata
Usipende kukurupuka,punguza mhemko na papara.Wewe bado unaishi kwa kufuata historia, hujui kuwa historia hubadilika?? Haya njoo sasa uone Mvomero ya sasa kama Wilaya! Halafu uliza ardhi kubwa na zenye rutuba wamiliki ni nani.
 
Haya ni mawazo ya kilofa zaidi kuwahi kuyasoma hapa JF.

Imenisikitisha. Kijiji gani kina hayo mambo?
Hizo ni story na sababu za hovyo za vijana wanaokimbia kwao na kwenda Dar kuuza leso pamoja na karanga kwenye mataa Dar.

Utakuta mtoto ni wa huko vijijini tena vijiji vizuri hataki kilimo anasingizia kulogwa ili aje Dar kuuza leso na kufuta vioo vya magari kwenye foleni.

Kimsingi huku Tanzania kijana ukijitambua na kuamua kufanya kilimo kwa kumaanisha unatika kimaisha. Tumewaona wengi nikiwemo mimi.
 
Ukishindwa wewe na mke wako usidhani wote watashindwa mkuu
Nilisema wewe unaendeshwa na papara,mhemko na jazba.
Tulizana wewe na mke wako mengine waachie wanaume
Nimenunua heka5 trh16/11/2024. Tusitishe watu
Nafikiri wewe ni :

limbukeni

mtu anayeanza kutumia au kupata kitu kwa mara ya kwanza

Usipende kukurupuka,punguza mhemko na papara.Wewe bado unaishi kwa kufuata historia, hujui kuwa historia hubadilika?? Haya njoo sasa uone Mvomero ya sasa kama Wilaya! Halafu uliza ardhi kubwa na zenye rutuba wamiliki ni nani.
Nimemuelewa jamaa hapo juu kuhusu uvivu. Anasema Ukweli. We unamaanisha mvomero yote au hapo Kijijini?

Kimsingi katika Wilaya ambayo ardhi inamilikiwa na wakubwa ni Wilaya ya Mvomero. Nimezaliwa na kukulia huko. Najua kuna maeneo ya akina Sumaye pale Mvomero kijijini sijui hadi sasa kama bado analimiliki lile shamba. Kuna ardhi inamilikiwa na familia za Hayati Mkapa kule Turiani bila kusahau mzee Mwinyi na Bakhresa pale Wami Luhindo.

Mi marehemu mzee wangu alikuwa na shamba pale Kijiji cha Milama tukaliuza tokana na migogoro baina yetu kwa Masai pia Abood ana shamba hapo hapo Milama sijui kama bado analimiliki. Sasa akina Jafo, Bashe, Mpina n.k nao wameingia kununua na kumiliki mashamba Mvomero na hiki ndio chanzo cha migogoro ya wafugaji na wakulima
 
We unamaanisha mvomero yote au hapo Kijijini?
Jamaa alimaanisha Mvomero ya zamani kipindi haijawa wilaya. Nimemaanisha Mvomero yote ya sasa.
Kimsingi katika Wilaya ambayo ardhi inamilikiwa na wakubwa ni Wilaya ya Mvomero
Huu ndiyo ukweli, halafu hawayaendelezi,ukienda kichwa kichwa kama mtoa mada unaambiwa ardhi ipo ya kutosha!
 
Hizo ni story na sababu za hovyo za vijana wanaokimbia kwao na kwenda Dar kuuza leso pamoja na karanga kwenye mataa Dar.

Utakuta mtoto ni wa huko vijijini tena vijiji vizuri hataki kilimo anasingizia kulogwa ili aje Dar kuuza leso na kufuta vioo vya magari kwenye foleni.

Kimsingi huku Tanzania kijana ukijitambua na kuamua kufanya kilimo kwa kumaanisha unatika kimaisha. Tumewaona wengi nikiwemo mimi.
Mkuu Kuna Uzi wangu niliileta kwenye jukwa la kilimo unasema Nimelima nyanya heka 1 nimepata milioni 15.

Wengine walikataa kata kata. Hata huku kwetu vijana wacheza pull wapo mida kama hii wanacheza Tyr!.

Nimepapenda nitalima huko
 
Back
Top Bottom