Yep! Malkia Hangaya nyota yake imeng'aa kwa kipindi kifupi kutokana na ubunifu, umakini na uchapa kazi wake.
Tatizo sasa kuna watanzania wengine wenye sifa zinazoshabihiana na zile za malkia Hangaya ila tatizo lao tu ni kwamba nyota zao hazing'ai.
So inabidi uwatafute kwa tochi ili kuweza kuwaibua.
Mmoja wa watanzania hao ni Ndg Pascal Mayalla. Ni kijana mzalendo, mchapa kazi na mwenye kuitumikia nchi hii kwa hali na mali.
Maadam imetokea pengo la nafasi ya ukuu wa wilaya kule Arusha, ningependa kumsihi malkia Hangaya kuwa ikimpendeza 'amfitishe' Pascal Mayalla kwenye nafasi hiyo ili aendelee kuitumikia nchi yetu kwenye viwango vingine.
Nitafurahi iwapo malkia Hangaya atazingatia maombi haya ambayo yamekuwa yakitolewa na watanzania wengi kwa kipindi kirefu.
Yadumu maamuzi ya mwenyekiti. Na Mungu baba wa Mbinguni azidi kumuinua malkia Hangaya aweze kuiendesha nchi yetu kwa viwango vya kipekee!