MINOCYCLINE
JF-Expert Member
- Apr 2, 2015
- 8,018
- 16,802
Mchezaji wa Simba, Dejan Georgejevic kupitia akaunti yake ya Instagram amesema mkataba wake umevunjwa kuitumikia klabu hiyo.
Na kama leo hii ( hasa CEO ) Barbara Gonzalez uliyemleta huyu Mzungu umeona hafai ni kwanini hapo mwanzo Mimi MINOCYCLINE na Yule mwana Jamiiforums Maarufu GENTAMICINE tulipopiga mno Kelele hapa kuwa asisajiliwe na asajiliwe Ceaser Lobi Manzoki kwakuwa huyu Mzungu tulikuwa hatumjui na aliyekuwa akimjua ni Kocha aliyeondoka Zoran Maki mlitupuuza na mkatuaminisha kuwa ni bora zaidi ya Manzoki?
Sitaki kuwa Mnafiki Kiufundi ( Kimpira ) huyu Mzungu Dejan ni mzuri tena hata zaidi ya Sakho na Okra aliyegombana nae Majuzi ila mmeamua Kuachana nae kwakuwa tu aliletwa na Kocha Zoran mliyeshindwana nae na wenye Akili tulipoona tu Kocha Zoran Maki mmeshindwana tulijua kuwa hata Maisha ya Mzungu Dejan ndani ya Simba SC lilikuwa ni Suala la muda tu ila nae mngeachana nae na hatimaye leo limetokea.
Sikatai wala sipingi Kuachana nae Mzungu Dejan ila kama ameondoshwa kwa Chuki na sababu zisizo na Mashiko nawahakikishieni kuwa Laana yake kwa kile tulichomfanyia kwa Kumtumia Okra amchokoze na amdhalilishe ili awe Frustrated na Confused ndani ya Simba SC itatutafuna Kimafanikio kama ile ya kula Rambirambi ya Kiungo wetu wa Kikongo Patrick Tabu Metesa Petit Mafisango ( Baba Crespo ) na kuja Kujuta.
Pole sana Mzungu Dejan usijali Waswahili ( hasa Sisi Miafrika ) ndivyo tulivyo, tunashukuru kwa hiki kidogo ulichotupa na wenye Kuujua hasa Mpira tunajua Wewe ni Mchezaji Fundi hasa na unaujua Mpira hivyo tunakutakia Kila la Kheri huko uendako na Binafsi kama MINOCYCLINE nakuombea upate Klabu Kubwa zaidi ya Simba SC ili Utuumbue tulioachana nawe Kimajungu na Kiuswahili hii leo.
Nimesikitika na kusikia vibaya sana.