Sijaona mahala Spika Tulia Ackson alipoisigina Katiba ya JMT. Mnaolalama mnalalama bila kutumia busara

Sijaona mahala Spika Tulia Ackson alipoisigina Katiba ya JMT. Mnaolalama mnalalama bila kutumia busara

Kwa taifa letu katiba ndio mwanzo na mwisho juu ya uendeshaji wa nchi. Kugawa madaraka ya mihimili na kuwapa wananchi haki zao.

Hii ni kwa sababu taifa letu lina katiba iliyoandikwa. Yaani written Constitution.

Haina ubishi kuwa ni kwa mujibu wa katiba ya JMT mbunge akifutwa uanachama basi ubunge wake unakoma. Na hii ni kwa mujibu wa ibara ya 71(1)(e) ya katiba ya JMT.

Lakini ibara ya 107A(1) ya Katiba ya JMT inasema wazi kabisa na kutanabaisha kuwa Mahakama ndio kitakuwa chombo pekee cha kutoa haki.

Sasa mlitaka Spika Tulia ndio aseme Mdee na wenzake sio wabunge? Suala lipo mahakamani?

Muwe mnatumia akili sometimes.
Mbona cuf mliwafuta siku hiyo hiyo hamkusubiria hata hukumu ya mahakama

Sent from my TECNO KG6 using JamiiForums mobile app
 
Wewe kweli changi wa malunde
Nini kilitangulia kati ya kufukuzwa uanachama, kutolewa bungeni na kwenda mahakamani????.
Ivi jambazi akiwa jela huku anatumika kufungua Afu akaamua kukata rufaa huwa anatolewa kwanz jela rufaa yake ikisikilizwa?
Bado Mahakama ina wajibu wa kutafsiri utaratibu uliotumika na CHADEMA
 
Mahakama kuu tarehe 22 ilisemaje?
Hivi we una akili na ulienda shule? Nini hii
Screenshot_20220627-161006.jpg
 
Kwa CHADEMA tu ndiyo mahakama inakuwa na wajibu wa kutafsiri utaratibu ila kwa CUF,CCM na vyama vingine mamlaka ya mahakama hayapo?
Kuna watu wa hovyo sana Tanzania. Nimempiga spana kaishia kudai sijapenda shule namtajia nilipopita Nate ataje anauliza ili iweje???
Vinajidai vinajua wakati viliiba mitihani
 
Kuna watu wa hovyo sana Tanzania. Nimempiga spana kaishia kudai sijapenda shule namtajia nilipopita Nate ataje anauliza ili iweje???
Vinajidai vinajua wakati viliiba mitihani
Wanajidai waelewa kumbe ni janja isiyokuwa na tija.
 
Unachokisema wewe ni kuhalalisha uvunjifu wa sheria! Unafanya hivyo kwa sababu unazozijua na wanaokutuma ! Japo mm siyo mpuuzi kama unavyoniita.

Alifukuzwa wabunge kina Ngwali wa Cuf pale bungeni. Waliachwa waendelee na ubunge huku rufaa zao zikisikilizwa?
Akikujibu niite mbwa nimekaa paleeee!
 
Hawakuchelewa kukata rufaa. Lengo la siasa za wakati huo ilikuwa ni kukigawa Cuf lipumba na maalimu
Sisi sote ni watanzania tunafuatilia mambo tupo hapa hapa nchini na shule tulienda bila kufeli wala kuiba mitihani.
Nasari alifukuzwa ubunge na alienda mahakamani? Aliruhusiwa kuingia bungeni akingoja maamuzi ya mahakama?
Hawa vichwa maji watakupotezea muda bure. Wamechagua kujifanya hawaelewi kama mazuzu vile!! Kama kulikuwa na makosa kuwaondoa waliokuwa wabunge wa CUF wakati ule, mbona hatusikii kuwa watalipwa fidia ya uonevu kwa kuondolewa bungeni wakati walikata rufaa mahakamani?
Huu uhuni hata Tulia mwenyewe anajua ni uhuni,alikuwa ni Naibu spika wakati huo. Mahakamani, hukumu/ maamuzi hutolewa kwa kurejelea hukumu/maamuzi ya kesi za nyuma zenye madai/jinai yanayofanana na kesi ya wakati wa Sasa.
Kwa bunge letu itategemea na aina ya spika,Rais aliyeko madarakani na ccm ya wakati huo. Unaweza kuona bunge jingine kwa issue ya hivi hivi wakaamua tofauti na sasa.
Wao kuvunja katiba na sheria ilimradi Rais au CCM inataka nini kwao siyo hoja kabisa.
Na ukilitazama sakata la kina Halima,mtu mwenye akili timamu, jina pekee linalowafaa ni mamluki wa ccm. Ilijulikana na wengi kama ilivyokuwa ahadi ya Ndugai kuwa bunge lijalo wataangalia namna ya kuondoa ukomo wa muda wa urais na ni bunge hili la sasa, kama siyo Mungu kuingilia kati, leo tungekuwa na Rais asiye na kikomo. Mabadiliko ambayo akina Halima wangeshiriki. Hawa ni wasaliti hawastahili kuonewa huruma na yeyote. Hao wanaowatetea ni sehemu ya kundi la uovu na wanafanya hivyo baada ya mission yao kufeli 17/03-
 
Back
Top Bottom