witzone2
JF-Expert Member
- Jan 14, 2022
- 797
- 1,739
Mbona cuf mliwafuta siku hiyo hiyo hamkusubiria hata hukumu ya mahakamaKwa taifa letu katiba ndio mwanzo na mwisho juu ya uendeshaji wa nchi. Kugawa madaraka ya mihimili na kuwapa wananchi haki zao.
Hii ni kwa sababu taifa letu lina katiba iliyoandikwa. Yaani written Constitution.
Haina ubishi kuwa ni kwa mujibu wa katiba ya JMT mbunge akifutwa uanachama basi ubunge wake unakoma. Na hii ni kwa mujibu wa ibara ya 71(1)(e) ya katiba ya JMT.
Lakini ibara ya 107A(1) ya Katiba ya JMT inasema wazi kabisa na kutanabaisha kuwa Mahakama ndio kitakuwa chombo pekee cha kutoa haki.
Sasa mlitaka Spika Tulia ndio aseme Mdee na wenzake sio wabunge? Suala lipo mahakamani?
Muwe mnatumia akili sometimes.
Sent from my TECNO KG6 using JamiiForums mobile app