Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 762
- 6,984
Ipo haja yakubadili mfumo wetu wa utendaji kazi kama nchi ikiwemo vyombo vya dola. Mkurugenzi wa TPA alikuwa na riport au matokeo ya ukaguzi toka ilipofanyika exit meeting. Alielewa Kuna maeneo kuna mianya iliyopelekea mkaguzi kutengeneza hoja zilizokosa ushahidi wakuzifuta nakupelekea hoja hizo kuingia kwenye kitabu Cha taarifa ya CAG ya mwaka 19/20.
Taarifa ile iliposomwa kwa Mhe. Rais haikuelekezwa kamata, ilielekezwa uchunguzi ufanyike na matokeo yapelekee kuchukua hatua.
Kwa suala hili lilivyokaa hakuna namna TAKUKURU wanaweza kusema ndani ya masaa machache waliweza kupata nakala ya riport, wakaangalia hoja, wakupata mapungufu au dosari zakupelekea kuhoji na kisha kumkamata Mkurugenzi kwa mahojiano na kisha kumshikilia.
Uchunguzi wa hoja za CAG nitofauti na uchunguzi wa wizi wa kawaida, CAG kabla ajatoa taarifa tayari wahusika waliokaguliwa wanakuwa wanajua tatizi lililopo na mapungufu yake.
Naamini TAKUKURU walichofanya siyo professional task waliyoelekezwa bali wamekwenda kutisha nakuonyesha makucha. Walipaswa kumpa wito afike baada ya wao kufanya ground work nakuona yeye anahusikaje na wanapohoji Basi wajikite kwenye facts.
Sitaki kuwafundisha ila naamini wanakosea sana na hii ni moja ya sababu zinazopelekea hata wanapofika mahakamani wanakwama kwa technicalities. Unamkamata mtuhuma Leo ukijua ujaandaa hoja za mahojiano, unalazimika kumweka mahabusu nje ya muda wakisheria uliowekwa na mwisho wa siku unajikuja umeandika maelezo mara tano wakati ungetumia taaluma vizuri ungeandika maelezo once na ukafile case panapohusika.
Kwanini nimeweka andiko ili hapa, nataka kuvikumbusha vyombo vya dola visiwekeze kuzuia watu mahabusu bali viwekeze kukusanya ushahidi kabla yakukamata. Kama huyu boss wamekimbilia kumkamata then waanze uchunguzi, vipi kuhusu wanyonge wana Hali gani mahabusu za polisi na Magereza?
Tubadilike, tumewajaza wenzetu wasio na hatia mahabusu kwa sababu yakukimbilia kukamata then ndipo tuanze uchunguzi. Madhara yake tunapeleka holding charges mahakamani tukitapatapa kutafuta makosa nakuwaacha watu wanasota mahabusu bila dhamana na bila tuhuma zinazoeleweka.
Tupige Vita kauli mbiu ya uchunguzi unaendelea huku watuhumiwa wakiwa mahabusu. Fanyeni kwa taaluma siyo kwakutaka mwonekane mnajua kutesa watu.