Sijaona sababu za TAKUKURU kumshikilia Mkurugenzi TPA

Sijaona sababu za TAKUKURU kumshikilia Mkurugenzi TPA

Kama unakula kuleni wote, ili iwe ngumu kufunga staff wote ni ngumu kuwafunga wafanyakazi wote, kinachofachika watafukuza, hamisha na kusimamisha.. kama mnapiga 100%.. unachukua hata 8% au 10% izo tisini hakikisha kila mtu anailamba 😀😀😀.. ili kikinuka muone kama wafafunga wote.. ila sasa ubinafsi mtu anataka ale 95%.. lazima kinuke tu.. utajiri mzuri ni ule wa kidogo kidogo
Good thinking
 
Mkuu wa TAKUKURU anasema uchunguzi uko hatua za mwisho maana ulianza tangu mwaka jana around mwezi March, leo ndio wanamkamata Top Boss, hivi waliwezaje kufanya uchunguzi kwa ukamilifu ilhali mmoja wa watuhumiwa tena boss kubwa akiwa ofisini anaendelea na majukumu yake?

Je! Siku zote hizo hawakuona kuna umuhimi wa hata kurecomend huyu mtu awekwe pembeni ili wafanye kazi yao kwa uhuru na ukamilifu, hadi Madam President aliposema akae pembeni uchunguzi ufanyike ndio wanamdaka?

Je! Sasa ndio wamefanya uamuzi sahihi na hapo kabla walikosea, au hapo kabla ndio walifanya uamuzi sahihi na sasa wamekosea? Au ndio maana Madam President akawahimiza juu ya kuboresha sheria wafanye mchakato iende Bungeni labda bado viko "in middle lower freedom category" sasa ni wakati muafaka vipande hadi " middle upper freedom category au upper category kabisa".
 
wewe uliyeandika haya madudu umeisoma ripoti ya CAG? nina hakika hujasoma,kama ni hivyo haya unayaandika kutoka wapi. Acha hisia
 
Tuacheni Unafiki hakuna Mtanzania ambaye akiwekwa katika Nafasi fulani au akipata Wadhifa kwenye Sekta yenye Pesa hatoiba.
Wacha uwongo labda wewe ndio mwizi na umezaliwa mwizi. Kuna Watanzania wengi tu waadilifu wamekuwa Accounting officers wa miradi na shughuli mbalimbali za serikali na hawajafanya wizi wowote. Je kama ingekuwa unavyoandika hapa si CAG angeripoti zaidi ya 90% ya bajeti kila mwaka imeibwa? WENZAKO NI WAADILIFU IM SORRY FOR YOU.
 
Tuacheni Unafiki hakuna Mtanzania ambaye akiwekwa katika Nafasi fulani au akipata Wadhifa kwenye Sekta yenye Pesa hatoiba.
Ni kweli mkuu hata mimi lazima nitaiba ila kwa akili sana msijue, shida huanza nikishanogewa nitajidhihirisha tu
 
Nakubaliana na wewe.

Huku kwetu badala wachunguze ndio wakamate, wao wanakamata huku hawajaanza uchunguzi, wanakusumbua na mwisho wa siku wanakosa ushahisi wanakuachia...
Hilo swala amewahi kuulizwa huyu Boss wa TAKUKURU akasema shida ni 2

1. Kuna watu wanatumia uwepo wao mtaani kutishia mashahidi au kuharibu ushahidi
2. Kuna watu wameachiwa na wakakimbia(flight risk)

Kama kuna justification, sio shida mtu kuwekwa mahara salama ikiwa kuwepo kwao nje kunaweza kuzuia justice isifanye kazi
 
Kachukue nafasi yake ya kukaa ndani sio kila jambo linaloandikwa nawe unakopi tu!
Waimba mapambio ya kusifu na kuabudu wamebadili gia angani , aiseee maisha haya .
Screenshot_20210329-172251.png
 
Kama anatuhuma za kuchukua pesa za umma na kuweka kwenye mambo binafsi, kwanini asishikiriwe?
Tuanze kuogopa kuiba kwa kutumia nyadhifa zetu. Mwizi wa kuku anawekwa ndani. Mwizi wa mali ya umma tena billions anaachwa atembee kifua mbele? Ndio shida ya kumtumainia mtu na kuacha Mwenyezi Mungu.
 
Gazeti moja leo limeandika ati kakutwa na $ 3000, sasa $3000 ni ajabu? hizo ni sh 7,500,000? la ajabu lipi kuwa na sh 7,500,000? Mungu atusaidie
 
Wacha uwongo labda wewe ndio mwizi na umezaliwa mwizi. Kuna Watanzania wengi tu waadilifu wamekuwa Accounting officers wa miradi na shughuli mbalimbali za serikali na hawajafanya wizi wowote. Je kama ingekuwa unavyoandika hapa si CAG angeripoti zaidi ya 90% ya bajeti kila mwaka imeibwa? WENZAKO NI WAADILIFU IM SORRY FOR YOU.

Absolutely Rubbish from you Imbecile.
 
Hilo swala amewahi kuulizwa huyu Boss wa TAKUKURU akasema shida ni 2

1. Kuna watu wanatumia uwepo wao mtaani kutishia mashahidi au kuharibu ushahidi
2. Kuna watu wameachiwa na wakakimbia(flight risk)

Kama kuna justification, sio shida mtu kuwekwa mahara salama ikiwa kuwepo kwao nje kunaweza kuzuia justice isifanye kazi
Hii ni chaka la kutumia kuonea watu, kuweka satu ndani miaka unasema ushahidi haujakamilika.
 
Hii ni chaka la kutumia kuonea watu, kuweka satu ndani miaka unasema ushahidi haujakamilika.
Ni kweli, kama hakuna proper justification, ni loophole ya uonevu. Lakini pia ni kweli kuna watu huwa wanakimbia, na kuna watu huwa wanaua mpaka mashahidi.
 
Back
Top Bottom