Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 6,238
- 8,194
Kwanini Wakristo hawajitakasi kwa maji, yaani kuosha viungo vya mwili (uso, kichwa, mikono na miguu) kabla ya kusali au kufanya ibada? Mbona katika kitabu cha Yohana 13 imeandikwa kwamba Yesu alipokuwa pamoja na wanafunzi wake, alijifunga taulo kiunoni, akamimina maji katika chombo, akaanza kuwaosha wanafunzi wake miguu?
Baada ya kuchunguza Maandiko, nimegundua kwamba Yesu aliwatawadha miguu wanafunzi wake ili kuwafundisha unyenyekevu, sio kuwaamuru waoshe miguu kabla ya ibada. Nyakati za Yesu, miguu ilichafuka sana kwa vumbi njiani. Hivyo mtu akifika nyumbani, kabla ya kuingia ndani, mtumishi wa nyumbani ndiye aliyekuwa akifanya kazi ya kumuosha miguu bwana wake. Ndio sababu katika hicho kitabu cha Yohana, tunasoma kwamba Petro alikataa kuoshwa miguu na Yesu, kwakuwa alijua Yesu ni Bwana wake.
Katika tukio hilo, Yesu aliamua kuwatawadha miguu ili kuwafundisha unyenyekevu; kwamba aliye mkubwa anatakiwa kujinyenyekesha na kuwahudumia hata wadogo. Petro alipoelewa maana ya kiroho ya kutawadha akakubali Bwana Yesu amuoshe miguu.
Umeelewa? Wakristo hawatii udhu kabla ya kusali kwa sababu Yesu hajawaagiza kufanya hivyo. Alichoagiza ni kunyenyekeana na kuhudumiana. Mkubwa awe tayari kumhudumia hata aliye chini yake.
Kama kutawadha lingekuwa jambo muhimu, Yesu asingesema "heri wenye moyo safi maana hao watamuona Mungu," (Mt 5:8) angesema heri walioosha miguu, mikono na uso...
Kwahiyo mtu aliye na moyo mchafu - moyo uliojaa mawazo ya uzinzi, uuaji, hasira, chuki, udanganyifu, kulipa kisasi - hata akiosha viungo vyake au kuoga mwili mzima, bado mbele za Mungu anaonekana mwenye dhambi.