Sijapenda Roboti wa Bungeni kutumia jina la mzazi wangu

Sijapenda Roboti wa Bungeni kutumia jina la mzazi wangu

Unaweza kufungua kesi ya madai mkuu.mshitaki nape nauye Kwa kutumia jina la mama Yako pasipo idhini Yako.
Sijamaanisha kuwa siruhusu mtu yeyote kutumia jina hilo.

Mafadhaiko yangu yapo kwenye kulitumia jina hilo kwa lisanamu.

Ikitokea siku nikakutana na ex wangu lazima atanikejeri kwa kuniita mwana wa robot, hebu pima mwenyewe madharau kama hayo yakianza si nitalala selo mkuu!

Sijapenda kwa kweli
 
Eh shughuli ipo wafungulie mashtaka wanakuzoea au nenda bungeni ukimwona huyo robot mbomoe bomoe hutamsikia tena
Sina hasira zenye kuzaa hasara, hivyo siwezi peleka hasira zangu bungeni.

Nimemwachia Mungu ashughulike na hao waabudu sanamu,ashughulike pia na hilo lisanamu lao.

Mungu hadhihakiwi.
 
Hapa simlaumu Roboti aliyepewa jina la Eunice bali namlaumu mwanadamu aliyempatia huyo robot jina hilo ambalo mama yangu amelitumia kwa muda mrefu.

Mama alipewa jina hilo baada ya kubatizwa na kuwa mkristo kamili, huu ni mwaka wa 75 tangu mama aanze kulitumia jina la Eunice.

Yaani nimeumia sana kwa hilo lisanamu kupewa jina la mama yangu kipenzi na mcha Mungu kama bibi yake Timotheo yule mtoto wa kiimani wa mtume Paulo.

Ombi langu kwa sasa ni Mungu aingilie kati kushughulika na hao wote walioshiriki huo ujinga wa kugawa jina la mama mcha Mungu, litumike kwa lisanamu.

Dhihaka zikafike tamati kwa kuharibu kila kilichotumika kutengeneza hilo lisanamu.

Na iwe hivyo.
 

Attachments

  • IMG-20240519-WA0064.jpg
    IMG-20240519-WA0064.jpg
    111.1 KB · Views: 2
Back
Top Bottom